KIWANDA
NI NINI?
Maana ya kiwanda ni kwamba, bidhaa huzalishwa
kwa kutumia mashine, kwa kiasi kikubwa na kwa gharama nafuu katika muda mchache
zaidi kuliko kama vile ambavyo mikono ya binadamu ingeliweza kuzalisha.
Mapinduzi ya viwanda yalianza huko Ulaya hususani nchini Uingereza katika karne
ya 18 na 19 na baadaye kusambaa karibu maeneo mengine yote ya dunia.
Leo hii baada ya karne karibu 2 kupita Tanzania
na sisi tunataka kufanya mapinduzi makubwa ya viwanda Tanzania. Hii haimaanishi
kwamba Tanzania hatuna viwanda ila unapotaja orodha ya viwanda na idadi ya
viwanda vilivyokuwepo au aina za viwanda vyetu, ni chache mno kulinganisha na
zile nchi zilizoendelea kama za Ulaya, China na Marekani kiasi kwamba unaweza
ukafananisha na tone moja tu la maji katika bahari kubwa.
Ikiwa kama kweli Tanzania tunataka kuufikia
uchumi wa viwanda, ni lazima tukubali kwamba hakuna njia ya mkato zaidi ya
kuanza kidogokidogo. Hata Uingereza wenyewe na Uchina wakati wakianza
hawakuanza na viwanda vikubwa sana bali viwanda vidogovidogo na mwishowe
wakajikuta wakihitaji kujenga viwanda vikubwa vikubwa kwa ajili ya kukidhi
mahitaji ya vile viwanda vidogovidogo vilivyotangulia kuanzishwa.
Kwa mfano unapoanzisha kiwanda kidogo cha
juisi ya matunda baadaye utahitaji kuwa na kiwanda kikubwa cha chuma kwa ajili
ya kutengeneza spea na vinu kwa ajili viwanda hivyo vidogo. Hivyo unaweza kuona
kwamba viwanda vidogo huzaa viwanda vikubwa. Viwanda vya nguo halikadhalika na
vile viwanda vya kubangulia korosho au pamba.
MAAJABU
YA KIWANDA
Kiwanda huweza kufanya kazi ya kushangaza
sana, ndiyo maana huko Uingereza na Marekani wakati huo wanamapinduzi hao wa
viwanda walipata shida sana na hata wengine kuuwawa au kuteswa kutokana na
mapinduzi hayo kuonekana yatapunguza au kuondoa kabisa ajira za watu. Hofu hiyo
ilitawala lakini hatimaye ilikuja kuonekana haina maana yeyote sawasawa tu na
ile hofu wakati wa Y2K miaka ya 2000 au mapinduzi ya kompyuta miaka ya 70 mpaka
90.
ATHARI
ZA VIWANDA
Matokeo ya maajabu hayo ya viwanda matokeo
yake hujitokeza kwenye uchumi kwa kuleta pia mapinduzi makubwa ya kiuchumi.
Mapinduzi hayo huweza kuifanya nchi au hata mtu mmoja mmoja kubadilika kiuchumi
katika muda mchache ajabu kutoka hali duni sana ya kiuchumi kuelekea hali bora
zaidi ya kiuchumi au kutoka kuwa masikini na kuwa tajiri. Kwa hiyo tunaweza
tukasema kwamba viwanda huleta neema, viwanda huleta utajiri na kiwanda kina
uwezo mkubwa wa kumfanya mtu aondokane na umasikini wa kutisha.
Unaweza ukachunguza mifano midogo tu
mazingira yanayokuzunguka, hebu angalia watu wenye viwanda vidogo vidogo vifuatavyo,
mashine ya kukamua juisi ya miwa, mashine ya kuchonga viazi vya chipsi, kiwanda
cha chakula cha mifugo, mashine ya kusaga na kukoboa nafaka, mkulima
anayemiliki trekta au jembe la maksai, kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, mashine
ya kufyatua tofali za umeme, cherehani ya umeme, mashine ya kukorogea unga wa
kuokea keki au mikate, mashine ya zege nk.
Bila shaka shughuli au viwanda vidogo
nilivyovitaja hapo juu, huweza kufanyika kwa urahisi sana na bila shaka yeyote
ile wale wanaozifanya au kumiliki mashine hizo, hali zao za kiuchumi haziwezi
zikafanana na zile za wale wanaofanya shughuli hizo kienyeji kwa mikono bila ya
kutumia mashine.
Ingawa dhana ya kiwanda ni pana zaidi ya
mashine kwa maana ya kuhusisha michakato mingine mingi kama vile soko,
ufungashaji(packaging) na suala la biashara kwa ujumla, lakini kikubwa hapo
suala la kutumia nyenzo au mashine huwa na umuhimu mkubwa na wa kipkee zaidi.
KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA JUISI YA
MATUNDA KWA KUTUMIA MTAJI MDOGO.
Hakuna ubishi wowote kwamba changamoto iliyo
kubwa zaidi baada ya mjasiriamali kupata wazo la biashara yake ni jinsi ya
kupata mtaji wa kutosha wa kuanzisha biashara hiyo. Wajasiriamali wengi hupata
wazo la kuanzisha viwanda vya juisi ya matunda na hilo hutokana na Mikoa mingi
ya Tanzania hasa ile Mikoa ya Kaskazini kama Tanga na Morogoro na baadhi ya
Mikoa ya kanda ya Kusini kama vile Iringa na Mbeya kuwa inazalisha matunda
mengi sana na ya aina mbalimbali lakini matunda hayo wakati wa msimu hufurika sokoni
na mwishowe kuozea mashambani bila faida yeyote ile kwa wakulima.
Karibu kila tunda hutoa juisi |
Karibu kila tunda linaweza kusindikwa na
kisha kwenda kuuzwa hata baada ya msimu wake kuisha lakini tatizo mara nyingi
huwa ni gharama za kununulia mshine kwa ajili ya usindikaji. Hata hivyo wakati
mjasiriamali unasubiri uweze kupata mtaji kwa ajili ya kuanzishia kiwanda cha
kutengeneza juice ya matunda, unaweza ukaanza kutengeneza na kuuza juisi hizo
kwa kutumia mashine rahisi unazoweza kumudu gharama yake na ukakidhi mahitaji
makubwa ya wateja ambao inabidi kwanza uchunguze na kubaini ni kitu gani
wanachopendelea zaidi kwenye juisi za matunda. Anza hata na blenda na friji
yako ya nyumbani.
Aina za juice za matunda zinazopendwa sana na
watu ni kama vile juisi ya ukwaju, juisi ya ubuyu, juisi ya passion, juisi ya
miwa, juisi ya karoti, juisi ya parachichi, juisi ya limao, juisi ya papai, juice
ya tende, juisi ya ndizi, juice ya embe,
juisi ya chungwa, juisi ya zabibu, juisi ya tikitimaji, juice ya nanasi, mchanganyiko wa juice ya parachichi na passion,
parachichi na embe, mchanganyiko a juisi ya embe na chungwa nk.
SIRI KUBWA YA MAFANIKIO KATIKA KIWANDA KIDOGO
CHA KUTENGENEZA JUICE MBALIMBALI ZA MATUNDA.
Kiwanda hata kiwe kidogo kiasi gani, ni
lazima uhakikishe ile misingi mikuu ya biashara inazingatiwa ili kupata matokeo
yaliyokuwa bora kabisa. Misingi hiyo iliyoainishwa katika kitabu cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI ni kama vile, kufanya utafiti wasoko(upembuzi yakinifu), kutengeneza mpango wa biashara nk. Vitu hivi na
vinginevyo kama kutafuta soko, uwekaji wa kumbukumbu nk. ni muhimu sana katika
kuhakikisha kiwanda au biashara inafanikiwa.
Mbali na sababu mahsusi utakayobaini mwenyewe
katika utafiti wako wa soko utakaoufanya kwa mujibu wa kitabi hicho, lakini
kuna hii sababu ambayo ipo kotekote(ni universal) kwa mtu yeyote yule
anayefanya biashara ya kutengeneza na kuuza juisi ya matunda, awe ni
mtengenezaji mdogo mdogo anayetembeza na jagi barabarani au mwenye kiwanda
kikubwa kama Bakhresa na Dewji. Ni muhimu sana kuifahamu siri hii, kwamba wanywaji
wote wa juisi za matunda duniani kote wanapenda kunywa juisi SAFI, SALAMA NA
INAYOBURUDISHA.
Nayasema hayo kwa sababu katika utafiti wangu
mitaani nimewahi kuona jinsi wauzaji wengi wa juisi hizi za kutembeza na majagi,
madeli au ndoo wanavyokosa wateja bila ya wao wenyewe kujua sababu hasa ni nini.
Na mjasiriamali akishaona leo amemwaga juisi, kesho tena hivyo hivyo, hukata tamaa
na kuona biashara ya kuuza juisi ni biashara kichaa isiyokuwa na faida, huiacha
na kwenda kujaribu biashara nyingine.
Katika kuhakikisha USAFI NA USALAMA wa juisi,
vigezo ambavyo ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika biashara au kiwanda cha
juice mbalimbali za matunda, mjasiriamali ni lazima uzingatie sana suala la
KIFUNGASHIO cha juisi yako. Juisi hata iwe tamu kiasi gani lakini usafi
na usalama wake unapokuwa wa mashaka mteja huwezi kumshawishi anunue kwako
kamwe.
SOMA: Wateja wanahitaji sababu ya kununua kutoka kwako.
SOMA: Wateja wanahitaji sababu ya kununua kutoka kwako.
Hebu jiulize ni mara ngapi wewe mwenyewe
umekutana na juisi za kupima huko mitaani, ukapuuzia kununua kwa sababu tu,
wanapima kwa kikombe ambacho husuuzwa kwa maji ya kawaida pindi mteja mmoja
anapomaliza kukitumia na kuwekewa mteja mwingine?. Wakati mwingine unaweza
ukaona juisi nzuri sana inayovutia machoni lakini unashindwa kununua kwa sababu
tu juisi hiyo imetiwa katika chupa au kopo la maji ambalo muuzaji aliliokota
baada ya mtumiaji kumaliza kunywa maji na kulitupa, je usalama wake ni wa
kuridhisha? Je, unafikiri ikiwa muuzaji wa juisi hiyo kama anashindwa kuwa na
kifungashio cha uhakika basi na uandaaji wake utakuwa makini?
Kama mjasiriamali mwenye malengo na maono ya
kuja kumiliki kiwanda chako cha kusindika juisi za matunda mbalimbali ndani ya
Tanzania ijayo ya viwanda, basi huna budi kuhakikisha wateja unaowauzia juisi
yako unawaondolea mashaka yote yaliyoainishwa hapo juu. Ikiwa utashindwa
kuwaondolea mashaka wakati huu ukiwa na kiwanda kidogo basi ujue hata
utakapomiliki hicho kiwanda kikubwa hautaweza pia.
VIFUNGASHIO BORA VYA JUISI KWENYE KIWANDA
CHAKO KIDOGO CHA JUICE ZA MATUNDA.
Ikiwa juisi yako unauzia dukani, mgahawani au
kwenye kioski, hakikisha vyombo unavyohifadhia juisi na kuwapimia wateja ni
visafi muda wote na kila siku unaviosha kwa maji ya moto na sabuni. Jitahidi
uwawekee wateja juisi katika vikombe au glasi zile za kutumia na
kutupa(takeaway) kwa usalama zaidi. Kama unatumia mashine ya kuchanganyia na
kupoozea juisi(juice dispeser), usafi wa mashine uwe ni wa hali ya juu sana
kila siku.
Ikiwa unatembeza juisi yako barabarani,
jaribu kuwa mbunifu kidogo, ni ukweli kwamba wapo wateja wasiojali kuhusiana na
swala la usalama au usafi na hivyo kutumia juisi hata kama kifungashio chake ni
makopo ya kuokota barabarani, lakini ukumbuke pia kwamba kuna idadi kubwa tu ya
wateja wale wanaojali zaidi afya zao.
SOMA: Kufungua kiwanda kidogo cha kusindika & kufungasha nafaka, naomba ushauri.
SOMA: Kufungua kiwanda kidogo cha kusindika & kufungasha nafaka, naomba ushauri.
Hivyo unaweza ukawa na vifungashio vya aina mbili,
aina ya kwanza hayo makopo ya bei ‘chee’ ya kuokota na aina ya pili ukawa na
makopo yako au vyupa spesho vya kununua kutoka SIDO au kokote kule vinakopatikana
na kuwaeleza wateja kwamba unazo chupa safi maalumu kwa ajili ya juisi. Au
unaweza pia kutumia mikebe au vikombe vya kutumia na kutupa(takeaway) pamoja na
mirija.
Vifungashio hivyo maalumu na visafi vinaweza
kugharimu kiasi fulani cha fedha na hivyo kufanya bei ya juisi yako kuwa juu
kidogo, lakini hiyo haiwezi kumzuia kununua juisi mtu anayejali afya yake. Hiyo
ni mbinu au njia sahihi kabisa itakayokuhakikishia wateja wa uhakika na wa
kudumu wa biashara yako ya juisi mpaka pale utakapopata mtaji wa kutosha
kuagiza mashine zako kutoka China kwa ajili ya kufungua kiwanda kidogo cha
kutengeneza au kusindika juisi za matunda mbalimbali ndani ya Tanzania mpya ya
uchumi wa viwanda.
...........................................................................................
Kitabu chako hiki cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, kitakuwezesha kuyafahamu mambo yafuatayo kwa ufasaha katika kuifanya biashara yako kuwa yenye tija na ya kisasa zaidi;
SOFTCOPY ya kitabu hiki kwa njia ya email ni sh. 10,000/=
uunatuma pesa na anuani yako ya email kupitia moja kati ya namba hizi; 0712202244 au 0765553030 jina: Peter Augustino Tarimo.
HARDCOPY ni sh. 20,000/=, njoo stendi Mbezi kwa Msuguri au uletewe kwa shilingi, 22,000/= ukiwa jijini Dar es salaam. Mkoani tunatuma kwa mabasi kwa shilingi,30,000/= au unaweza kuagiza mtu anayekuja Dar akuchukulie.
VITABU VINGINE KUTOKA SELF HELP BOOKS TANZANIA NI HIVI HAPA chinni.
SOFTCOPY 5,000/=
HARDCOPY 10,000/=
SOFTCOPY 3,000/=
HARDCOPY 5,000/=
Au tembelea, SMART BOOKS TANZANIA kupata maeelezo na vitabu zaidi.
...........................................................................................
Kitabu chako hiki cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, kitakuwezesha kuyafahamu mambo yafuatayo kwa ufasaha katika kuifanya biashara yako kuwa yenye tija na ya kisasa zaidi;
·
Maana halisi ya ujasiriamali,
·
Jinsi ya kuanzisha biashara,
·
Mbinu bora za kufanya utafiti wa masoko na
biashara,
·
Namna ya kusajili biashara yako Brela, TRA,
Manispaa nk.
·
Hatua kwa hatua jinsi ya kuandaa na kuandika -mchanganuo/mpango
wa biashara yako,
·
Michanganuo halisi na kamili ya biashara
zinazolipa,
·
Jinsi ya kuweka kumbukumbu na hesabu za
biashara,
·
Namna ya kutoa huduma bora kwa mteja.
·
Kufanya mauzo kitaalamu na
·
Njia kuu wanazotumia matajiri kutajirika.
uunatuma pesa na anuani yako ya email kupitia moja kati ya namba hizi; 0712202244 au 0765553030 jina: Peter Augustino Tarimo.
HARDCOPY ni sh. 20,000/=, njoo stendi Mbezi kwa Msuguri au uletewe kwa shilingi, 22,000/= ukiwa jijini Dar es salaam. Mkoani tunatuma kwa mabasi kwa shilingi,30,000/= au unaweza kuagiza mtu anayekuja Dar akuchukulie.
VITABU VINGINE KUTOKA SELF HELP BOOKS TANZANIA NI HIVI HAPA chinni.
SOFTCOPY 5,000/=
HARDCOPY 10,000/=
SOFTCOPY 3,000/=
HARDCOPY 5,000/=
Au tembelea, SMART BOOKS TANZANIA kupata maeelezo na vitabu zaidi.
Good
ReplyDeletethank you very much!
Delete