Msomaji wa blogu hii kutoka Songea Mkoani Ruvuma ameuliza maswali yake matatu, pia kuna maswali mengine kadhaa ya wasomaji wengine ambayo yote kwa pamoja nitayajibu kwa mfululizo katika makala zinazoanza leo mpaka pale maswali yote yatakapomalizika. Swali lake la kwanza kutoka Songea aliuliza hivi;
SOMA: Kufungua kiwanda kidogo cha kusindika & kufungasha nafaka. naomba ushauri.
“Hivi
kuweka rehani kiwanja, nyumba au ardhi kwa ujumla ili kupata mkopo ni sahihi na
inawezekana?”
JIBU:
Ndugu msomaji, umenikumbusha mbali sana ulivyotaja kuwa
unatokea Songea, Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla una fursa nyingi sana na nzuri za
kiuchumi hasa katika shughuli za biashara ya mazao ya chakula na hata biashara
nyinginezo, nasema hivyo kwani niliwahi kuishi mkoani humo na nilijihusisha na
kilimo cha mbogamboga na matunda kama nyanya pale Ruhuwiko japo kwa kiasi
kidogo, najua jinsi mazao mengi yanavyostawi huko hasa mahindi mihogo na mazao
mengine yote, kwa ujumla Songea kila zao hustawi.
Kuhusu iwapo ni jambo zuri kuweka rehani rasilimali zako
kama dhamana ya mkopo, hilo ni jambo sahihi kabisa na duniani kote mikopo hasa
ile ya mabenki mkopaji huwezi ukapewa mkopo pasipo kuonyesha kwanza hati miliki
ya dhamana iwe ni nyumba, kiwanja, ardhi au mali nyingine yeyote itakayokuwa
kama ulinzi endapo ikatokea ukashindwa kulipa mkopo utakaopewa. Ni ukweli
mchungu kwamba hakuna mkopo rahisi popote pake ila tu urahisi wa kupata au
kuomba mkopo utategemea vigezo mbalimbali vikiwemo, ukubwa wa mkopo unaoomba,
aina ya taasisi unayoiomba mkopo, aina ya dhamana unazotumia kuombea huo mkopo
nk.
Pia ni lazima ukumbuke ya kwamba hakuna mkopo usiokuwa na
dhamana. Hata ile mikopo ya vikundi dhamana yake kubwa ni ile wakopaji kuwa katika
vikundi vya watu kadhaa marafiki wanaofahamiana vizuri na kuaminiana. Kwa
mtindo huo benki au taasisi inayokopesha hujiridhisha kuwa mmoja wao
atakaposhindwa kulipa marejesho ya mkopo basi wenzake ndio watakaowajibika
kumlipia au kukata akiba zao.
Unapoomba mkopo tuseme labda benki, ukapewa fomu ya
maombi ya mkopo,(loan application form), kuna mahali utahitajika kujaza dhamana
utakazoweka, kisha afisa anayehusika atakwenda kuzikagua ili kuzitathmini kama
zinalingana na kiasi cha mkopo unaoomba kupatiwa. Ikiwa vigezo vyote utatimiza
matokeo yake ni kupewa mkopo ambao utaingiziwa katika akaunti yako ya mkopo.
Zipo aina mbili za hatimiliki za mali, hatimiliki ya serikali na hatimiliki za
kimila
Kuna masharti katika sheria ya rehani yanayohusiana na
dhamana ya mkopo kwa pande zote mbili yaani Mkopaji na mkopeshaji ambayo
yanahitajika na sheria ya ardhi ya Tanzania ya mwaka 1999 sura ya 334 kifungu
cha 24 mpaka cha 30 kama vile mkopaji kuhakikisha anamhusisha mwanandoa ikiwa
dhamana ni mali ya familia na kutokupangisha au kuuza dhamana kabla ya kumaliza
kulipa mkopo bila idhini ya maandishi kutoka kwa mkopeshaji.
Kwa upande wa mkopeshaji naye anatakiwa kutoa taarifa ya
siku (60) kwa umma endapo kutakuwa na ucheleweshwaji wa marejesho au uvunjifu
wa masharti kwa mkopaji kabla ya hatua ya kuuza mali iliyowekwa rehani. Baada
ya hizo siku 60 nyumba au mali hupigwa mnada kwa kutoa taarifa au notisi ya
siku 10 kwa wale wanaoishi ndani ya nyumba hiyo au mmiliki. Mkopeshaji pia haruhusiwi
kununua mali iliyowekwa dhamana labda kwa kibali maalumu cha mahakama. Watu
wengine hudhani benki au taasisi ya fedha kutangaza mnada wa mali wanazoweka
rehani siyo huduma nzuri kwa mteja(bad customer care) lakini kumbuka sheria ya
nchi inawataka kufanya hivyo.
Kuweka rehani hatimiliki ya mali yako ili kujipatia mkopo
siyo jambo baya na wala hakuwezi kukupa madhara yeyote endapo utazingati
masharti yote yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na kuwa na nidhamu nzuri ya pesa ili
kuhakikisha fedha unazokopa zinafanya ile shughuli uliyokusudia tu na wala siyo
kwenda kufanyia starehe au matumizi ya kawaida ya kifamilia ambayo mishowe
fedha hupotea na huwezi tena kuzipata ili urejeshe kule ulikozikopa.
Matumizi mazuri ya fedha za mkopo ni kwenda kuziwekeza
katika mradi uliokusudia au katika vyanzo vingine vya uhakika vya mapato
ambavyo hatimaye vitakuletea faida kifedha utakayoitumia kurejesha mkopo wa
watu, riba yake na mahitaji yako mengine ya kila siku.
Huo ndio mwisho wa majibu ya swali la kwanza kutoka kwa
msomaji wetu wa Songea Ruvuma, tukutane tena katika makala itakayofuata baada ya
hii kwa ajili ya majibu ya swali lake la pili.
NJIA RAHISI ZAIDI YA KUPATA VITABU VYA SELF HELP BOOKS
TANZANIA NI KUPITIA EMAIL YAKO, SOFTCOPY NI BEI RAHISI, HUKUFIKIA HARAKA, NA
KWA UHAKIKA.
UNACHOTAKIWA KUFANYA TU NI KULIPIA KITABU/VITABU
UNAVYOTAKA KUPITIA SIMU YAKO KWA NAMBA 0712202244 AU
0765553030 JINA PETER AUGUSTINO TARIMO, TUMA NA ANUANI YAKO YA EMAIL KWA
MESEJI, HALAFU TUNAKUTUMIA KITABU/VITABU MUDA HUOHUO BILA KUCHELEWA UNADOWNLOAD.
Bei: 10,000/= softcopy
Bei: 5,000/= softcopy
Bei: 10,000/= softcopy
0 Response to "KUTUMIA NYUMBA KIWANJA AU ARDHI KAMA REHANI KUOMBA MKOPO NI SAHIHI? NAOMBA USHAURI"
Post a Comment