Unapochukua uamuzi wa kuanzisha biashara yako
mpya, kumbuka ya kwamba vipo vitu ambavyo ni wewe mwenyewe unayetakiwa
kuvigundua wakati ukiwa katika mchakato wa kuiendesha biashara yako, hakuna mtu
atakayeweza kukufundisha uvifanye na hata akitokea mtu akafanya hivyo wala
hutamuelewa.
Yapo mambo mengi ya msingi unayojifunza
kutokana na uzoefu unaoupata mbali na elimu au mafunzo rasmii ya biashara na
ujasiriiamali unayoweza kuwa uliyapata mahali kwingine mfano kama hapa katika
blogu hii unayosoma sasa. Na yale unayojifunza kutokana na uzoefu au vitendo
halisi ndiyo pengine yaliyokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukuwezesha kuiendesha
biashara yako kwa mafanikio makubwa zaidi. Miongoni mwa vitu hivyo nimeviorodhesha
hapa chini;
1. Kamwe
usije ukabweteka.
Kujisahau kunawafanya wafanyabiashara
wengi hatimaye kuanguka hata ikiwa
walishaanza kupata mafanikio. Mara nyingi watu hawategemei kama jambo dogo kama
hili ni somo kubwa wanalopaswa kujifunza mpaka bada yameshawafika ndipo huja
kugundua kumbe ni kitu muhimu.
Kumbuka hakuna mikakati
inayoweza kudumu milele, soko unaloliona leo au ulilolliona jana silo
litakalokuwepo kesho, linaweza likaanguka muda wowote, halikadhalika na bidhaa
au huduma unazooweza kuona leo hii zinafanya vizuri sokoni, muda wowote zaweza
kudorora, hivyo mipango na mikakati yako ni lazima ifanyiwe uhakiki kila baada
ya muda na ndiyo maana katika mafunzo ya jinsi ya kuandaa mpango wa biashara
yanayopatikana ndani ya kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI,
umuhimu wa kufanya ulinganisho baina ya mpango wa biashara yako na hali halisi
umesisitizwa sana. Ni sharti kila baada ya muda fulani ucheki kujua ni kipi
kimeenda kama ulivyopanga na ni kipi hakikwenda ili uweze kujua ufanye nini
zaidi au upunguze nini.
2.
Huwezi ukafanikiwa peke yako.
Kufanya biashara kama mtu binafsi haimaanishi
kwamba upo peke yako, Unaweza ukajidai kwamba mafanikio yako yametokana na
nguvu zako binafsi lakini kumbuka uungwaji mkono mkubwa ulioupata kutoka kwa
watu mbalimbali ikiwemo familia yako, mke, watoto, ndugu jamaa na marafiki,
wajomba, shangazi, mama na baba wadogo, mashemeji nk. Hata kitendo tu cha
kukutakia mema na kukuombea ufanikiwe, kisaikolojia ni msaada mkubwa kwako
katika kufanikiwa biashara yako. Usaidizi hauishii tu kwa watu bali hata
vitabu, DVD na mafunzo mbalimbali unayoyapata pia huhesabika kama usaidizi.
3.Mshindani
wako mkubwa ni wewe mwenyewe.
Kila siku unajitahidi kuwa bora kushinda siku
iliyopita, hii ni kusema kwamba wewe wa
leo unashindana na wewe wa jana na, mara zote ungependa umshinde wewe yule wa
jana.
Kuna mambo mengi unayoweza kujifunza kutokana
na uzoefu wako binafsi katika biashara, mengi ya hayo huwezi ukaelewa mantiki
yake mpaka umeingia front (msari wa mbele) mwenyewe kwenye biashara. Kama wewe
ni start up, ndiyo unaanza au
unapanga kuanza siku moja basi usisubiri kujua kila kitu kuhusiana na ABC za
biashara na ujasiriamali, wewe anza tu,mengine utajifunza mbele ya safari
kutokana na uzoefu.
……………………………………………………………………....
Masiliano yetu ni
0712202244 au 0765553030,
HARDCOPY
SH.30,000/=
SOFTCOPY
SH.10,000/=
HARDCOPY SH.15,000/=
SOFTCOPY SH. 5,000/=
HARDCOPY SH.7,000/=
SOFTCOPY SH.3,000/=
Tupo Mbezi karibu na stendi kuu ya mabasi.
Kwa vitabu zaidi na maelezo tembelea ukurasa; SMART BOOKS TANZANIA
0 Response to "UNAPOANZISHA BIASHARA YAKO, VITU HIVI (3) USITEGEMEE KUFUNZWA NA MTU YEYOTE"
Post a Comment