SEHEMU
YA II
Katika makala nyingine kwenye blogu hii iliyosema, Hatua10 za kuanzisha biashara ya duka la rejareja, Sehemu ya kwanza, tulizitaja hatua 6 peke yake, jambo
lililosababisha wasomaji wengi kutaka kuzijua hatua nyingine 4 zilizobakia. Leo
tutamalizia hatua nyingine 4 zilizobakia kusudi kuwaondolea dukuduku wasomaji
na wafuatiliaji wa blogu hii.
7. Kuchagua eneo la biashara (duka)
Watu
husema “Biashara ya duka la
rejareja ni eneo” Eneo utakalochagua
kuweka duka lako, litaathiri kila kitu utakachofanya katika biashara yako yote.
Mafanikio au kuanguka kwa bishara ya duka la rejareja kunategemea kwa asilimia kubwa sana sehemu ulipoiweka
biashara hiyo.
SOMA: Mbinu hizi 2 za uendeshaji duka la rejareja kwa mafanikio hazipo mahali pengine popote pale.
SOMA: Mbinu hizi 2 za uendeshaji duka la rejareja kwa mafanikio hazipo mahali pengine popote pale.
Usikurupuke
wakati wa kufanya uamuzi wa eneo utakaloweka biashara yako ya duka, chukua
muda wa kutosha kufanya utafiti na kuwa
mvumilivu. Ukigundua eneo halifai, basi ni bora ukaahirisha na kuangalia
uwezekano wa eneo jingine kuliko baada ya muda mfupi kuja kuanza kuzozana na
mwenye nyumba akurudishie kodi au hata biashara yako kufia njiani.
Usikubali presha za madalali ambao hutumia
ujanja kwa kukuambia eti, eneo/fremu fulani inagombewa na watu zaidi ya watatu
na wewe ni wa nne, hivyo ukichelewa kidogo tu hutaikuta. Zifuatazo ni baadhi ya
dondoo za kuzingatia wakati ukitafuta eneo utakaloweka duka lako la rejareja;
Wateja:
Hakikisha eneo lina wateja wa kutosha; bidhaa
utakazouza zitategemea aina ya wateja walioko pale. Mara nyingi sana maduka ya
rejareja huhitaji maeneo yaliyokuwa na wakaazi wanaoishi majumbani, wapita njia
kwa mfano eneo la stendi ya basi au sokoni panapokusanyika watu wengi. Kila
kundi lina aina zake za bidhaa tofauti na lingine, kwa mfano duka la mtaani kwenye makazi ya watu
utahitajika uweke zaidi vyakula kama nafaka na mahitaji ya nyumbani, na stendi utaweka zaidi vinywaji
baridi na vitafunwa “bites” kushinda vitu vingine.
SOMA: Tumia siri hii kuongeza mauzo x2 ya soda, maji, juisi na sigara.
SOMA: Tumia siri hii kuongeza mauzo x2 ya soda, maji, juisi na sigara.
Chagua eneo ambalo
unajua kabisa wateja wako unaolenga watanunua bidhaa unazokusudia kuzipa
kipaumbele, mathalani, usije ukachagua eneo la stendi halafu ukajaza mchele na
unga, wapita njia na wasafiri siyo rahisi wakanunua vitu hivyo.
Eneo
kuwa na idadi kubwa sana ya watu siyo ishara kuwa na wateja nao ni wengi, la
hasha, inawezekana pale wanapita njia tu, kwa mfano maeneo ya posta mpya Dar es
salaam kuna umati mkubwa sana wa watu, lakini hauwezi ukaenda kukita duka lako
la nafaka pale ukamuuzia mtu, vitakudodea….
Uwezekano wa kufikika na
kuonekana kwa urahisi;
chagua eneo wateja wanaweza kufika bila matatizo, iwe
ni kwa miguu ama usafiri kama wa gari, pikipiki, bajaji n.k. Je, panaonekana
kwa urahisi na wateja? Pasiwe ni mahali palipojificha itakusaidia hata
kimatangazo, patakuwa panajitangaza penyewe vitu kuonekana na kuwavutia wateja
kwa urahisi.
SOMA: Mchanganuo wa biashara ya duka la rejareja.
SOMA: Mchanganuo wa biashara ya duka la rejareja.
Taratibu za mipango miji.
Wapo watu wamewahi kulia machozi na hata wengine
kufikia hatua ya kuzimia baada ya kutakiwa wavunje mabanda yao waliyokuwa wamejenga
maeneo ya mji ambayo serikali imepiga marufuku. Hata ikiwa unapanga sehemu,
ulizia kwanza kwa kina kama eneo lile halina marukufu yeyote iliyowekwa na
serikali za mitaa au serikali kuu.
Majirani na washindani wako.
Biashara
za majirani wako zinazofanana na ya kwako zina uwezo wa kuathiri biashara yako
kwa namna moja ama nyingine. Chunguza eneo unalotaka kufungua duka lako. Maduka
mengine yanayokuzunguka yakoje?
Ukigundua
pana ushindani mkali sana, na uwezo wako kiushindani pengine kimtaji ni mdogo,
basi ni bora hata ukaangalia uwezekano wa eneo jingine lenye ushindani kidogo
zaidi. Vilevile angalia eneo lenye
biashara ambazo zitategemeana na ya kwako kwa mfano kama pana mama ntilie wengi
au migahawa basi duka la rejareja la vyakula ndiyo mahali muafaka.
Masuala
binafsi.
Jiangalie binafsi ikiwa wewe ndiye
utakayeuza mwenyewe dukani, umbali kutoka unapoishi, masuala ya chakula n.k.
Mathalani eneo ulilochagua ni mbali sana na unapoishi jambo litakalokufanya upoteze muda mwingi
njiani pamoja na foleni, kama ni mjini
basi ndiyo balaa kabisa.
SOMA: Biashara ya duka inavyoweza kukutoa kimaisha ukiwa mjanja.
SOMA: Biashara ya duka inavyoweza kukutoa kimaisha ukiwa mjanja.
Jaribu kuchagua eneo la karibu na
unapoishi, vilevile suala la chakula lina athari kubwa katika matumizi yako ya
kila siku. Athari hizo husababisha faida
kuwa kidogo, hakikisha unapata njia nafuu ya kujipatia mlo wako wa mchana uwapo
dukani aidha kwa kununua mahali ambapo bei siyo kubwa sana au uletewe kabisa
kutoka nyumbani. Kwa hiyo utaona ikiwa eneo ni karibu na unapoishi, itakuwa ni
jambo rahisi sana.
Huduma
za Kijamii.
Chunguza vitu kama umeme, maji na sehemu
ya kujisaidia(choo), uwezekano wa kupita gari la kuzima moto “fire” ikiwa moto
utazuka kwa bahati mbaya pamoja na mahali ambapo wateja wanaweza wakapumzika au
hata kujificha mvua na jua. Hakikisha pana umeme wa uhakika kwani duka la
rejareja friji ni kitu muhimu sana, ulizia ikiwa nyumba ina deni Tanesco kwani
wenye nyumba wengine wanapoleta mpangaji siku hiyo hujiunganishia umeme wa wizi
kinyemela na baada ya siku mbili tatu unakatika kama kawaida.
SOMA: Aina za bidhaa za duka zilizo na faida ndogo lakini zinaotoka haraka haraka.
SOMA: Aina za bidhaa za duka zilizo na faida ndogo lakini zinaotoka haraka haraka.
Usalama.
Angalia matukio ya uhalifu katika eneo
husika ukubwa wake ukoje.
Yapo
maeneo mengine huwezi ukaweka duka na kisha jioni ukalale nyumbani, ni lazima
wezi usiku na wasipovunja mlango basi watachimba ukuta kwa nyuma na kuzama ndani kisha kukomba kila kitu. Vilevile usalama
wako binafsi wakati wa kurudi nyumbani usiku, je, hamna wimbi kubwa la vibaka
kama “watoto wa mbwa mwitu” n.k.?.
8. Nunua bidhaa kwa jumla.
Ili
duka la rejareja liweze kufanikiwa ni lazima bidhaa zinunuliwe kutoka maduka ya
jumla kwa bei ya chini na kisha ziuzwe kwa bei ya juu kidogo kusudi kupata
faida. Ni lazima uyafahamu maduka yanayouza bidhaa utakazouza yanayouza kwa bei
nzuri, linganisha bei za maduka tofauti kubaini ni lipi lenye bei nafuu zaidi
ukizingatia pia ubora wa bidhaa zenyewe isije kuwa rahisi kumbe ni bidhaa feki
za “mchina”.
9. Weka sera na taratibu za duka lako.
Hata
kabla hujafungua duka lako ukiwa bado upo kwenye hatua ya mipango, huu ndio
wakati mzuri wa kuweka taratibu na sera zitakazoongoza duka lako. Kwa kuanisha
matatizo kabla hayajajitokeza kutakusaidia kuja kukabiliana nayo kwa urahisi
zaidi kuliko yanapokuja kukushitukiza. Amua kabla, jinsi utakavyotatua matatizo
mbalimbali yatakayohusiana na wateja, mfanyakazi/wafanyakazi ikiwa kama
utawaweka na wadau wengine wowote wale
ili kuzuia makosa pindi yatakapokuja kujitokeza. Baadhi ya mifano ya
sera/taratibu unazoweza kupanga ni kama vile:-
·
Kiasi
cha faida kwenye bidhaa.
· Suala
la nyongeza kwa wateja.
· Ni
muda gani utakaoruhusu mteja kukaa na deni
· Mteja
akishanunua bidhaa ana ruhusiwa kuirudisha au la, na ni katika mazingira yapi
ataruhusiwa kurudisha?
· Utakubali
mteja kuweka fedha kidogo kidogo kabla hajachukua bidhaa?
· Muda
wa kufungua na kufunga duka na siku za sikukuu.
SOMA: Puuza imani na dhana hizi potofu ufanikiwe katika biashara yako ya duka la vyakula.
10. Tangaza duka lako.
10. Tangaza duka lako.
Unaweza ukasema “nitalitangaza vipi duka?”
ukiwa na maana kwamba ukishafungua ni basi, wateja watajileta wenyewe tu. Ni
kweli kuwa duka la kawaida hauhitaji kwenda kwenye TV, Redio au magazetini
kulitanganza, lakini unaweza ukalitangaza
duka lako hata kwa majirani watakaokuzunguka tu na ukashangaa kuona tofauti
kubwa.
Baadhi ya njia unazoweza kutumia
kulitangaza duka lako la rejareja ni kama hizi zifuatazo;
· Weka
mpangilio mzuri na unaovutia wa bidhaa zako pamoja na kutengeneza mandhari
nzuri itakayowavutia wateja.
· Weka
bango juu ya paa la duka lenye maandishi ya jina la duka au weka kibao mbele ya
duka kinachoonyesha pana duka.
· Unaweza
pia kugawa vipeperushi kwa watu walio karibu na duka kuwajulisha aina za bidhaa
unazouza, bei pamoja na punguzo kama lipo.
· Kuwa
na mkakati wa kutoa huduma nzuri kwa wateja kusudi wakija waende kuwaambia na
wenzao.
Je, unataka kuanzisha biashara ya rejareja au tayari unayo na ungependa kuifanyia mapinduzi makubwa ndani ya muda mfupi iwezekanavyo?
Kama jibu ni ndiyo, basi kitabu hiki hapa chini kitakuwa msaada mkubwa katika safari yako hiyo ya kuibadilisha biashara yako au kuianzisha...
Asante sana bro nimekupata vzr sanaa
ReplyDeleteUbarikiwe Sana!
DeleteNashukuru kaka, kwa ushauri wako
ReplyDeleteUbarikiwe sana na wewe
Deletethanks
ReplyDeleteAnd yuo too!
Delete