VIDEO
Kitu kinachonifurahisha katika dhana ya mihimili ya Dola
ni ile kuwepo kwa kila mhimili kuwa huru katika kutekeleza majukumu yake katika
kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo. Unapotazama bunge likiendelea pale
Dodoma, inafurahisha kuona jinsi wabunge kutoka pande zote mbili, ule wa Chama
tawala na Upinzani wanavyoikosoa na kuishauri serikali katika mambo ya msingi
kama ya haya ya uchumi. Linapokuja suala la kuondoa umasikini wa Watanzania
Wabunge huweka tofauti zao kando.
Serikali ya awamu ya 5 inafanya mambo makubwa sana,
lakini haiwezi kufikia malengo yake yote kikamilifu kama haya ya kulifanya
taifa kuwa na uchumi wa viwanda peke yake bila ya ushauri kutoka kwa wadau wengine, mtu mmoja, chama kimoja, au
mawazo ya upande mmoja tu hayataweza. Ni kwa njia ya kukosoa na wakati mwingine
kukubaliana na mawazo mbadala ndiko kutakako tufanya kama Taifa kutoka pale
tulipo.
SOMA: Dr. Slaa, Professa Lipumba, Ujasiriamali wa Kisiasa upo wapi?
SOMA: Dr. Slaa, Professa Lipumba, Ujasiriamali wa Kisiasa upo wapi?
Rais wetu na serikali yake tunaweza kumsaidia kufikia
malengo yetu sote kwa kujenga utamaduni wa kutoa mawazo mbadala yenye tija bila
kuchukuliwa kama usaliti, kama anavyofanya Bashe na wengineo wengi katika Bunge
la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Nadhani mchango kama huu wa Hussein Bashe
na hata wabunge wengine kama Mheshimiwa Sugu wa Mbeya mjini, Peter Serukamba wa
Kigoma Kaskazini, Mh. Freeman Mbowe wa Hai na Richard Ndassa wa Sumve si ya kubomoa hata kidogo yana
uwezo wa kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha tunafika kule tunakotaka
kufika kama Taifa. Wabunge hao walikuwa wakichangia katika mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa
mwaka 2017/2018.
Hapa ni mchango wa Mheshimiwa Hussein Bashe, Mbunge wa
jimbo la Singida Mjini, hotuba yake nzima tarehe 9 November 2017 akichangia kwenye
Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2017 kuelekea 2018 uliowasilishwa na Mh. Waziri
wa fedha na mipango Dr. Phillip Mpango;
"Mweshimiwa mwenyekiti, kwanza nitumie fursa hii,
kuwapongeza waheshimiwa mawaziri ambao wamebaki kwenye nafasi zao, na mawaziri
wapya na manaibu waziri walioteuliwa na mheshimiwa rais katika mabadiliko ya
baraza la mawaziri la hivi karibuni niwatakie kila la heri katika kutimiza
wajibu wao.
Mh. Mwenyekiti, mwaka 2016 wakati tunajadili mpango ndani
ya bunge hili, nilimtahadharisha waziri wa mipango, nikimwambia kwamba mpango
unaouleta, hautofikia economic growth ya
7%. Kwa sababu mpango huu unaacha sehemu
kubwa ya Watanzania nje, siyo mpango inclusive. Mwaka 2017, mwaka 2016 wakati
tunajadili bajeti nilirudia maneno haya, na mwaka huu wakati tunajadili bajeti nilimwambia, kuna conflict
kati ya fiscal policy ambazo Wizara ya fedha inazisimamia na Monetary
policy, these two policies zinapambana
zenyewe na matokeo yake yataonekana.
Mheshimiwa Mweneyekiti naomba ninukuu takwimu zifuatazo,
kama alivyosema ndugu Serukamba, “Uchumi wowote Duniani una mirror, kioo na kioo cha uchumi wowote unaokua, ama unaosinyaa, ama unaoshuka, moja ni financial institution, mbili ni trade, tatu ni stock
exchange. Mh. Mwenyekiti, personal
lending mwaka 2015 illikuwa ni asilimiaa 25%, today ni 8.9%, trade ilikuwa ni
asilimia 24%, this is a lending to trade,
ilikuwa ni asilimiaa 24%, leo ni
asilimia 9%, na maneno haya siyatoi kwingine, ni ripoti za BOT na quarter
report ya BOT inayoishia June, lakini taarifa
zingine ni muongozo wa bajeti alioleta
yeye, na ni mpango wake alioleta yeye.
Agriculture, leo ni negative nine (-9)%, from 6% lending capacity ya mwaka 2015. Manufacturing,
from 30% lending to 3%. Transport and communication, from 24% lending to
negative twenty five(-25)%, building, from 22% to 16%. Mh. Mwenyekiti, our
economy it is said inakua, ukisoma projections
ni 6.8%, lakini taarifa ya mwisho ya economic bulletin for the quarter ending June 2017 imetuambia ni
5.7%, siyo maneno yangu.
Food inflation, let’s go categorically, it is 10.1%, siyo
maneno yangu, taarifa ya Septemba ya BOT hii hapa. Mh. Mwenyekiti, why are we facing
this, it’s not a rocket science, Waziri
wa fedha ukurasa wa sita wa mpango, unasema
Export, na Mwenyekiti naomba iingie kwenye hansadi ya Bunge, nimeangalia taarifa za
monthly za BOT toka mwaka 2011 mpaka Septemba mwaka huu, for the first time in the history, hamjaweka
performance ya export and Imports, why, mnaficha nini?.
SOMA: Hotuba ya Rais Obama nchini Kenya akifungua kongamano la Wajasiriamali.
SOMA: Hotuba ya Rais Obama nchini Kenya akifungua kongamano la Wajasiriamali.
Alisema ndugu Abdurahaman Kinana Mwenyekiti, wakati
anaongea katika function ya Kigoda pale University of Dar es salaam, alisema hivi, namnukuu katibu wa
chama chetu; “Jambo muhimu la kiongozi ni kusikiliza watu wake, viongozi hamna monopoly right ya wisdom, viongozi
hawana monopoly right ya truth, viongozi
hawana monopoly right ya wao wako sahihi kila siku” Na Mheshimiwa
Mwennyekiti hakuna jambo muhimu katika
kupanga mipango yeyote duniani kama takwimu. Ukurasa wa 7 wa document ya
mapendendekezo ya mpango, unaonyesha mwenendo wa ukuaji wa pao la Taifa, toka
mwaka 2011 mpaka 2017. 2011 our growth was 9.1%, today it is projected 6.8%
lakini as per this report ni 5.7%.
Mwenyekiti naomba ninukuu maneno yafuatayo, ukurasa wa 7
unasema; “Kufikia June 2017 export zilikuwa zimeshuka kwa asilimia 29.8%,
lakini Waziri anatupa a consoling statement
kwamba matarajio ni kurejea kwa exportation kuongezeka, eti kwasababu
tunajenga kukuza viwanda, sasa twendeni
tukasome hivyo viwanda vya export. Siyo
maneno yangu, kwenye mpango Waziri ametaja viwanda, ukurasa wa 26, kiwanda cha kuchenjua madini kilichopo Geita, kusindika nyama Kisivani, Shinyanga, Mitobotobo Farmers
company ltd, kuzalisha mafuta ya kula,
kuchambua pamba, kiwannda cha kuzalisha vifungashio- Global packing, kiwada cha
kuzalisha vinywaji baridi Sunny food company-Sayona. Hivi ndiyo tuta export kurudisha asilimia 29%. Kuzalisha bidhaa
za ujenzi, brother! tumeahidi kuondoa umasikini wa watu,
Mwenyekiti siyo maneno yangu, mimi naquote maneno ya Waziri wa Mpango.
SOMA: Mjasiriamali unawahitaji wateja wote, CCM na UKAWA
SOMA: Mjasiriamali unawahitaji wateja wote, CCM na UKAWA
Twendeni ukurasa wa 68, sekta ya kilimo, look at this,
hii ndiyo sekta imeajiri asilimia 65% - 70% ya
wananchi wetu, na kwa tafiti zillizofanyika ndugu Mwenyekiti, Watanzania
zaidi ya asilimia 80% walioko kwenye sekta ya kilimo, yaani ile 70%, 80% ya
hiyo 70% inafanya kazi mbili, duo, inalima na inafuga kama siyo ng’ombe, mbuzi, kuku, bata, na vitu
vya namna hiyo, anafanya duo, now look at these two things ndugu Mwenyekiti, Sekta ya mifugo, serekali imepanga
kufanya uhimilishaji wa mifugo laki nne, tunahimilisha, kufanya insemination,
ng’ombe laki nne na elfu hamsini na kitu. Lakini tunapanga kuzalisha chakula, hey,
Mwenyekiti, hey ni yale majani ya
ng’ombe. Tunapanga kuzalisha chakula kwa mwaka laki nne na elfu arobaini na
tano, hey kaki nne na elfu arobaini na tano. Kitakwimu hey moja ina uzito wa
kilo 25. Chakula hiki ukikigawa kwa siku 360, kinalisha ng’ombe 1600 huku unapanga kuzalisha ng’ombe kaki nne, lakini
unaandaa mpango wa chakula cha ng’ombe 1600.
Mwenyekiti hapa Wabunnge wamejadili suala la kilimo, hakuna
sehemu Waziri wa kilimo anaplan on the, kuanzisha price stabilization ya mazao
ya chakula. Leo kuzalisha kilo moja ya mahindi, gharama ya shambani, ni
shilingi 357, haya siyo maneno yangu, it’s scientifically proved, halafu huyu
mkulima anayetumia shilingi 357 kuzalisha kilo moja ya mahindi, bado gharama ya
kupeleka stoo, gharama ya kuweka mifuko, gharama ya kuweka dawa, halafu
atakapoweka stoo yake, kuna kauli inasemwa hapa walanguzi ndio wana mahindi.
Mwenyekiti, this is total misconception ya business principle, kote duniani,
kuna producer, kuna distributer, kuna retailer, kwahiyo unataka kuniambia mimi
ninayelima Nzega na hata mahindi yangu niyabebe niende nikayauze Nairobi?. Kuna
Intermediaries, and this is the duty of your fiscal policies, kufanya
intermediaries wafanye biashara.
Mwenyekiti nataka nikupe mfano mwingine, nataka nikupe
mfano mwingine, profitability ya financial institution imeshuka over 50%.
Waziri ana hoja moja dhaifu sana anaitumia ndani ya mipango, money circulation
imepungua, Mwenyekiti, kutoka billion 222 mpaka bilioni 12, na hoja anayosema
ni nini, matumizi yasiyokuwa ya lazima ya serikali yamepungua. Sasa, najiuliza, bajeti ya reccurent
imepungua? Kutoka 2011,12, 13 imepungua recurrent bajeti? No, spending ya
government ipo kwa hiyo nilitarajia
kwamba itakuwa wisely tutaiona imeleta positive impact, lakini hakuna. Sasa mimi
ushauri wangu kwa Waziri wa fedha Dr. Mpango, narudia, this is a third time, naheshimu your academic
background, sijawahi kudoubt, kaka, hauwezi kuondoa umasikini wa nchi hii bila
kuwekeza kwenye kilimo, never, hauwezi kuleta mapinduzi ya viwanda, mapinduzi
ya viwanda, bila kuwekeza kwenye kilimo.
SOMA: Wajasiriamali wataka mwakilishi Bunge la katiba.
SOMA: Wajasiriamali wataka mwakilishi Bunge la katiba.
Mwenyekiti, mkulima wa nchi hii, ndio kageuka punching box
ya nchi hii, tunacontrol inflation ya chakula kwa gharama ya mkulima. How come,
haiwezekani, hatuwezi kufanikiwa kwa namna hii. Yaani sisi tunadhibiti mfumko wa
bei kwa kumtia umasikini mkulima. Aina gani za economy hizi? Mwenyekiti nataka nikupe
mfano mdogo tena, aangalie, hatuwezi kuondoka kwenye umasikini kama mawazo ya
wizara ya fedha hayatokuwa ni productive oriented, badala ya kuwa tax based
approach, Mwenyekiti angalia mpango huu unakuwa financed namna gani.
Waheshimiwa wabunge tuchukue document ya mpango musome how are we going to
finance mpango, page namba 29 ya Muongozo wa maandalizi. (Mwnyekiti niilindie dakika zangu dk. moja tu.)
Mh. Mwenyekiti, Waziri anasema kwamba how to finance,
anazunguzia kwamba ata improve EFD
mashine, ataanzisha maabara ya TRA. It is all about Tax based approach. Haumsikii
anasema kwamba tutawekeza bilioni moja kwenye kilimo cha mahindi, ili tuweze
kuyield X, hausikii. Hauwezi kukamua maziwa ng’ombe usiyemlisha. Mh. Mwenyekiti,
ukiangalia VAT, pay as you earn, zimeshuka, hazifikii target aliyojiwekea
kwenye bajeti ya 17, na hapa anasema, kwamba makampuni yamepunguza wafanyakazi,
na unajua ni kwanini?. It’s not a rocket
science Mwenyekiti, tulimshauri kwenye kamati ya bajeti, kwamba, unaongeza
excess duty kwenye TBL, utapunguza uwezo wa uzalishaji wa hawa watu, hakusikia,
tumemwambia kwenye kamati ya bajeti, I was there, tumemwambia Waziri wa fedh,
unaua viwanda vya soft drink, kwa kuimpose 10% eti kwa udhaifu wao TRA wa
kusimamia sukari inayoingia, wameweka asilimia 10% tena on top. Kwa hiyo cocacola
akiingiza sukari kwenye nchi hii analipa 25%, instead of 15%, what kind of
economy is this. Serekali, serekali Mwenyekiti, na mimi nataka niwaambie
waheshimiwa wabunge hasa wa chama changu, tumepewa dhamana ya nchi hii na
Watanzania, let’s not allow mistakes za Waziri Mpango kuharibu nafasi ya
kuchaguliwa kwa rais wetu mwaka 2020.
Mwenyekiti samahani, nikupe mfano mdogo, kampuni zote za
vinywaji baridi, zilikuja mbele ya kamati ya bajeti, na sisi tukawaita Wizara
ya fedha, hawana capacity ya kwenda kukagua bonded ware house, hawana capacity
hiyo madhara yake unajua wamefanya nini Mwenyekiti?, wameamua kuanzisha kodi
mpya ya kuwithhold, sasa hivi private sector inadai TRA over eight hundred
billion shiliing, za returns on Tax, hawalipi, wanasuffocate, this is very wrong,
na mimi nimalizie niseme Mwenyekiti samahani, kama Waziri wa fedha
hatabadilika, hatuwezi kutoka hapa. Asante."
Credit:
Picha na Mtandao wa Mtanzania, video by AyoTV
0 Response to "KUONDOA UMASIKINI, MAPINDUZI YA VIWANDA BILA KUWEKEZA KILIMO NI KAZI BURE-HUSSEIN BASHE"
Post a Comment