SOMO LA MZUNGUKO WA FEDHA TASLIMU-Cash Flow ndiyo hesabu muhimu zaidi kwenye Biashara
Ni hesabu inayotoa utambuzi ambao aina
nyinginezo za hesabu haziwezi kuutoa hususani hali ya kifedha ya biashara
/kampuni. Katika Ulimwengu wa biashara kuna aina kuu tatu za hesabu ambazo ni hesabu
ya Faida na Hasara, hesabu ya Mali na Madeni na ya tatu ni hii ya Mzunguko wa fedha Taslimu.
Mzunguko
wa Fedha Taslimu au Cash Flow ni nini hasa?
Kwa lugha nyepesi kabisa; ni fedha
taslimu zinazoingia na zile zinazotoka kwenye
biashara. IIi biashara iweze kuwa na uhai ni lazima iwe na fedha
zinazozunguka mithili ya damu inavyozunguka ndani ya mwili wa binadamu
kumuwezesha aendelee kuishi. Kwa mujibu wa wataalamu, Sababu kubwa ya biashara
nyingi ndogo kufa inatokana na wamiliki wake kushindwa kusimamia vizuri
mzunguko wa pesa.
SOMA: Uamuzi mgumu kuchukua ili biashara yako izidi kukupa faida mwaka huu.
SOMA: Uamuzi mgumu kuchukua ili biashara yako izidi kukupa faida mwaka huu.
Unaweza ukailinganisha biashara na tanki la
maji, maji huingia ndani ya tanki kupitia tundu lililopo juu na maji hayo
hutoka kupitia tundu lililopo chini ya tanki. Hivyo ili kulifanya tanki liwe
zuri na lijae zaidi inatakiwa maji yaingie ndani mengi zaidi kuliko yale
yanayotoka nje.
Fedha zinazoingia kwenye biashara zinapokuwa
nyingi zaidi ya zile zinazotoka kwenye biashara maana yake mzunguko wako wa
fedha ni chanya(+), na fedha zinazotoka zinapokuwa nyingi kuliko zile zinazoingia maana yake ni kwamba, mzunguko
wako wa fedha ni hasi(-)
Ili biashara iweze kunawiri vizuri zaidi au
iendelee inahitaji mzunguko wake wa fedha uwe chanya(+), yaani fedha
zinazoingia zizidi zile zinazotoka. Ikitokea mzunguko wa biashara ukawa
hasi(-), ina maana kwamba biashara ipo katika hali mbaya kipesa na inahitaji
kuongezewa pesa kutoka mahali pengine ili iendelee kuwepo na kinyume chake
itakufa. Ni sawa na mgonjwa aliye na upungufu wa damu na anahitaji kuongezewa damu 'fasta' vinginevyo anaweza akapoteza maisha katika muda mfupi.
..............................................................................
Baada ya kugundua katika kampeni yetu ya mwaka jana tuliyoiita JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA kwamba kikwazo kikubwa miongoni mwa vikwazo vingine katika kufanikisha malengo mbalimbali ya kibiashara na maisha ni mzunguko mdogo wa fedha katika shughuli zetu, mwaka huu mpya wa 2018 tumeamua kulivalia njuga suala hili na hatua tulizochukua ni pamoja na kuanzisha masomo ya semina ndani ya blogu yetu ya private au Darasa la michanganuo(HAICHACHI SEMINA) yanayolenga kuamsha uelewa juu ya tatizo hili na namna ya kukabiliana nalo kwa vitendo.
Tutakuwa na masomo ndani ya blogu hiyo sambamba na njia ya Whatsapp kupitia namba 0765553030 kila wiki ambapo tunajadili na kuchanganua miradi iliyokuwa na FURSA kubwa za kutengeneza fedha taslimu kila siku, kumbuka mfanyabiashara mdogo au mwenye mtaji wa chini anahitaji mzunguko wa pesa wa harakaharaka na uliokuwa chanya ili kukabiliana na mahitaji makubwa ya ukuaji wa biashara yake huku akiweza kumudu gharama mbalimbali za maisha yake na familia bila kukwama.
SOMA: Kufa au kuanguka kwa biashara yako, fanya vitu hivi 9 kujiepusha.
SOMA: Kufa au kuanguka kwa biashara yako, fanya vitu hivi 9 kujiepusha.
Kila mradi au biashara itakayochanganuliwa ni lazima kuwe na kitu kikubwa cha ubunifu ambacho ndicho kiini cha kuifanya iwe na mzunguko wa fedha usiokuwa wa mashaka, tumeshafanyia utafiti miradi zaidi ya 12 ambayo ndiyo tutakayoiwasilisha kwenye semina hizo. Ni miradi isiyokuwa na hatari kubwa ya kukata mtaji, isiyohitaji gharama kubwa za uwekezaji wa awali, iliyo na faida kubwa, inayolipa ndani ya muda mfupi na isiyoumiza kichwa kwenye usimamizi.
Semina ya kwanza kwa mwaka 2018 itafanyika siku ya tarehe 3 na itahusu aina mpya kabisa ya ufugaji wa kuku wa kienyeji ambayo haijawahi kuzungumzwa mahali pengine popote pale, sikuambii kwa sasa ikiwa ni kuku wa kienyeji wa nyama au wa mayai, kwa ajili ya vifaranga au kwa ajili ya manyoya, bali ninachokusihi tu ni kwamba shiriki semina hiyo ili ukafahamu mwenyewe kila kitu.
Kupata tiketi ya kushiriki masomo haya ada yake ni shilingi elfu 10 tu na unapata fursa ya kusoma masomo ya semina zote zilizokwisha wahi kufanyika pamoja na masomo mengine yote yajayo kwani huhifadhiwa ndani ya blogu hiyo ya HAICHACHI na katika group la whatsapp maalumu tuliloanzisha kwa ajili hiyo. Kama tayari ulishajiunga na blogu hiyo kwa kulipa kiingilio chako utaendelea kupata masomo ya semina bila gharama za ziada ila tuma namba yako kwa ajili ya kuunganishwa na group la Whatsapp.
Ukihitaji kujiunga na mpango huu lipa kiingilio chako sh. 10,000/= kupitia namba za simu 0712202244 au 0765553030 jina litokee Peter Augustino Tarimo, kisha tuma anuani yako ya GMAIL kwa njia ya meseji, pia ili kuunganishwa katika group la watssap tuma ujumbe wa 'Niunganishe na semina' kwenye namba 0765553030.
Vitabu pia vipo na kuelekea mwaka mpya tumetoa offa kwa yule anayenunua vitabu vyote vitatu katika mfumo wa softcopy kupitia email, badala ya kulipa shilingi elfu 18 vyote 3, atalipa sh. elfu 15 tu! kwa softcopy za vitabu vyote vitatu.
0 Response to "JE UNAIJUA HESABU MUHIMU ZAIDI KWENYE BIASHARA? HUHITAJI DIGRII KUIJUA"
Post a Comment