Sekta ya mawasiliano hususani katika kipengele cha simu
za mkononi nchini Tanzania imekuwa ikikua kwa kasi kubwa tangu kuanza kwake
miaka ya 90 mwishoni wakati tuliposhuhudia ujio wa simu kubwa za mkononi aina
ya Motorola ambazo baadae kidogo watu waliziita kwa jina la utani kama “miche
ya sabuni” lakini jina hilo mche wa sabuni lilikuja baada ya kuingia aina
nyingine za simu mpya zilizokuwa na umbile dogodogo mfano, siemen, Ericson na
Nokia.
Nyakati hizo ndiyo tulishuhudia maneno kama, siemen ya
dole gumba, twangapepeta, Nokia ya kitochi, ‘jeneza’ na simu yeyote ile ya
mkononi kuitwa mobitel hata kama ilikuwa inatumia mtandao wa kampuni tofauti na
mobitel kama vile tritel, Vodacom na Celtel
Mabadiliko hayo yalikuwa yakitokea kwa haraka kiasi
kwamba ukinunua tu simu kabla hata haijachakaa, tayari inakuwa imekwishapitwa
na wakati, unatamani kununua toleo jingine tena . Hamna tofauti na iivyo sasa
unapoona makampuni kama TECNO, Samsung, na Apple wanavyotoa matoleo tofautitofauti
kila kukicha na kila toleo likiwa bora zaidi kushinda lile lililopita.
Tukiachana na historia hiyo sasa tuangalie jinsi kuibuka
kwa kasi kwa sekta hii kulivyoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa
ujumla hasa kwa wafanyabiashara wadogowadogo. Miji yote kuanzia Dar es salaam
na hata mikoani kila kona viliibuka vibanda vidogo vidogo maarufu kama vibanda
vya kupigisha simu ambavyo wingi wake ulitokana na idadi ndogo ya watu
waliokuwa wakimiliki simu za mkononi kwa wakati huo, wachache waliokuwa na simu
walikuwa na watu wengi waliotaka kuwasiliana nao, lakini kwa kuwa hawakuwa na
simu zao binafsi iliwabidi waingie katika vibanda hivyo ili kuweza kuwapigia na
kuwasiliana nao. Taratibu vibanda hivi vilianza kutoweka kadiri idadi ya watu
wanaomiliki simu za mkononi nayo ilivyozidi kuongezeka.
Badala yake viliibuka vibanda vingine kwa ajili ya
kuchajia simu na betri za simu kwa kutumia kobe sambamba na huduma zingine
mbalimbali kama vile, kuuza vocha za simu jumla na rejareja, kuingiza nyimbo
katika simu, kuuza kava za simu, kuuza vifaa mbalimbali vya simu za mkononi
kama earphones, vioo, betri, housing, protector, covers charger za simu, power
banks, touch, memory cards, flash nk. Vilevile katika vibanda hivyo utakuta
wengine wakitoa huduma za kusajili line za mitandao ya simu mbalimbali kama
vile mitandao ya Vodacom, Tigo, Airtel, Zantel, Halotel, Smart, TTCL na
mingineyo pamoja na huduma za kurudisha namba za simu zilizopotea(kuswap)
Kuna huduma nyingine kama vile, kudownload nyimbo mpya na
kuziburn katika CD au DVD au kuweka katika flash na memory cards japo kisheria
hii haikubaliki kabisa lakini kuna wakati watu walikuwa wakidownload sana. Wateja
wengi hupendelea kudownload nyimbo za dini, kudownload nyimbo mpya za kibongo,
kudownload nyimbo za bongo flava, nyimbo za Injili, Qaswida nk.
Huduma zoote hizo pamoja na vifaa mbalimbali kwa ajili ya
mawasiliano ya simu za mkononi zimebadilisha maisha ya vijana wengi wa
Kitanzania na watu wote walioamua kujiingiza katika biashara hizi, zimetoa
ajira za muda na za kudumu pamoja na kuongeza mapato ya serikali kutokana na
kodi na tozo mbalimbali.
Ubunifu
utakaokufanya uongeze mapato yako(faida) kama unafanya biashara ya kuuza na
kutoa huduma ndogondogo za simu za mkononi na smartphones.
Lengo kuu katika makala hii ilikuwa ni kukudokezea mbinu
kadha ambazo nimegundua zinaweza zikamfanya mtu anayejishughulisha na biashara
ndogondogo za kutoa huduma kwa watumiaji wa simu za mkononi akazidisha faida
anayopata mara nyingi zaidi ya ile aliyozowea kuipata kila siku katika kibanda
chake au kama ni duka, kioski na katika miavuli kwenye baraza za nyumba maeneo
mbalimbali, stendi na maeneo mengine ya wazi.
Simu za kisasa za mkononi maarufu kama Smartphones kwa
sasa hivi ndiyo habari ya mjini kila mahali. Kwa lugha nyingine unaweza ukasema
simu hizo sasa ndiyo ‘zinatrend’ hapa Tanzania na duniani kwa ujumla. Hii inafanya
mahitaji ya huduma mbalimbali zinazohusiana na simu hizo kuwa spesho na
zilizokuwa na uhitaji wa kiwango cha juu sana. Kuna watu wengi mpaka sasa hivi
ambao bado hawana simu hizi lakini wana mpango wa kuzimiliki hapo baadae. Kwa
ujumla kila mtu anatamani kununua simu hizo hata kama siyo leo wala kesho
lakini ni lazima ipo siku.
Kuna watu pia wanaomiliki simu hizo lakini bado hawajaweza
kufahamu kutumia kila kipengele kilichopo katika simu hizo, watu hao wanahitaji
sana mtu wa kuwaelekeza chapchap, wengine si kama ni mambumbumbu hapana, hawana
tu muda mwingi wa kuanza kukaa na kubonyabonya wakijifunza, wanataka njia ya
haraka ya kujifunza ambayo ni kwa kupata maelekezo kutoka kwa mtu aliyekwisha ‘master’
kuelewa vyema jinsi ya kutumia smartphones. Unaweza kushangaa hata mwingine
hajui awashie tochi wapi au aongeze mwanga wa kioo wapi.
Nilijaribu kufanya utafiti kidogo kwa kutembea vibanda
kadhaa nikijidai kama nahitaji huduma za kujiunga intanet, kufungua e-mail, kujiunga na facebook, kujiunga instagram, kujiunga
na whatsapp, kubadilisha kioo, kukata line, kubadilisha line, nk. Karibu kila
kibanda nilichopita wanakuambia, “sisi tunachaji simu tu” au “hapa tunaweka
miziki kwenye simu tu”. Ni vibanda vichache sana nilivyokuta wameweka vibao
vilivyoandikwa; “Tunaunganisha intaneti, e-mail, instagram, facebook, whatsapp,
badoo, twitter, youtube na telegram
Kama wewe unatoa huduma za simu, jifunze jinsi ya
kuunganisha huduma hizi zote nilizozitaja hapa na nyinginezo ambazo sikuzitaja
hapa lakini zinahusiana na smartphones au Intaneti kwa ujumla. Siyo kazi ngumu
kujifunza vitu hivi, waweza hata kumlipa mtu fedha kidogo akakuelekeza siku mbili,
tatu, ukishafahamu vizuri nenda katika kibanda au kioski chako na uweke bango
linalosomeka vizuri maandishi yanayotaja huduma zote hizo. Utashangaa kuona
wateja wakiongezeka siku hadi siku kuhitaji huduma hizo, usisahau pia kuweka na
charger kwa ajili ya smartphones kwani nyingi huwa hazikai na chaji muda mrefu.
…………………………………………………………
Ndugu
msomaji wa makala hii kwanza nikushukuru kwa muda wako halafu nikuombe tena
kushea makala hii kwa wale unaowathamini. Kama unapenda kujifunza biashara na
ujasiriamali kwa kina zaidi unaweza kupata moja ya vitabu vifuatavyo hapa chini
pichani kwa gharama kidogo. Unaweza pia kujipatia vitabu vyetu vingine bure
bila malipo na kwa maelezo yake zaidi unaweza ukayapata katika ukurasa huu
hapa; SMART BOOKS TANZANIA
Mawasiliano kwa ajili ya kupata vitabu hivi ni haya hapa;
simu: 0712202244
whatsapp: 0765553030
jina: Peter Augustino Tarimo
Mawasiliano kwa ajili ya kupata vitabu hivi ni haya hapa;
simu: 0712202244
whatsapp: 0765553030
jina: Peter Augustino Tarimo
1
2
3
0 Response to "JINSI YA KUONGEZA FAIDA BIASHARA YA KUINGIZA NYIMBO NA KUCHAJI SIMU ZA SMARTPHONE"
Post a Comment