Ndugu msomaji wangu karibu tena katika makala ya Ushauri ambapo tunaweka hapa katika blogu ushauri kwa msomaji aliyetutumia swali au changamoto anayokumbana nayo kuhusiana na ujasiriamali au biashara kwa ujumla. Leo hii kuna msomaji mmoja yeye kauliza kama ifuatavyo
“Nataraji kuanza utumishi mwezi wa kwanza, na kabla ya hapo
niliwahi kumsaidia kaka yangu kazi ya kuuza duka la vifaa, hata hivyo nikiwa
mtumishi ningependa kuwa huru kifedha kwa kuanzisha mradi wangu mwenyewe wakati
nikiendelea na utumishi sasa swali ni je, itawezekana au lazima nijiingize
kwenye mkopo?”
SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma, nipeni ushauri nina wakati mgumu.
SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma, nipeni ushauri nina wakati mgumu.
MAJIBU.
Asante sana na hongera ndugu yangu kwa ajira na
malengo uliyokuwa nayo. Upo sahihi kabisa kwani utumishi tofauti na baadhi ya
watu wengine wanavyouchukulia, siyo kitu kibaya bali ni chanzo kizuri sana na
cha uhakika cha mtaji kwa ajili ya kuwekeza katika shughuli nyinginezo za
kiuchumi na biashara.
Bila shaka umepata uzoefu kiasi fulani kutoka katika hilo duka
la ndugu yako, na hiyo ni faida pia. Ninachokushauri hasa ni kwamba, chukua
muda wa kutosha kufanya maandalizi ya biashara au uwekezaji wowote ule
utakaoufanya wakati ungali ukifanya utumishi wako. Kumbuka utakuwa na muda ‘limited’
sana nikimaanisha muda kidogo. Hivyo shughuli utakayoianzisha ni lazima uiwekee
mfumo(system) madhubuti ambayo haitaingiliana na utumishi wako hata
kidogo.
SOMA: Kutumia nyumba, kiwanja au ardhi kama rehani kuomba mkopo ni sahihi? naomba ushauri.
SOMA: Kutumia nyumba, kiwanja au ardhi kama rehani kuomba mkopo ni sahihi? naomba ushauri.
Zingatia sana hili: usikubali hata kidogo ‘kuisacrifice’ kuitoa
sadaka ajira yako kwa ajili ya shughuli ya kujiajiri mwenyewe kabla
haujahakikisha shughuli ama biashara hiyo inao uwezo wa kukutiririshia pesa
zinazozidi pesa unazotumia(mtiririko wako wa fedha kuwa chanya),
matokeo yake utakwama vibaya sana na maisha yako kiuchumi yanaweza kwenda
kuvurugika.
Suala la kukopa sikushauri uliwekee kipaumbele cha kwanza japo
baadaye haliwezi kuepukika. Katika hatua za awali mradi wowote ule wa
kibiashara ni vizuri zaidi kufadhiliwa na vyanzo vya pesa ambavyo siyo mikopo
hasa hii ya riba kwani iwapo itatokea mradi kutofaulu madhara yake huwa makubwa
na magumu kuhimili. Mkopo ni mzuri pale biashara inapoanza kujitegemea yenyewe
na kuzalisha mapato ya uhakika. Labda mkopo wenyewe uwe ni kiasi kidogo sana
ambacho hata mtaji ukikatika hautasumbuka kuurejesha.
Asante, nakutakia kila la kheri katika majukumu yako.
Peter Tarimo
Self help books Tanzania.
…………………………………………………….
Ndugu
msomaji nakualika katika SEMINA kwenye blogu ya private ya kulipia itakayoanza
tarehe 3 siku ya Alhamisi mwezi wa kwanza. Somo kuu ni JINSI YA KUUFANYA MZUNGUKO WAKO WA FEDHA KUWA CHANYA MWAKA HUU WA 2018
na tutakuwa tukijifunza mawazo na biashara zenye fursa kubwa ya kutengeneza
pesa kwa uhakika. Mawazo ya biashara hizo ni ya kipekee na yaliyofanyiwa
utafiti wa kutosha uliothibitika kuzalisha faida haraka na kwa urahisi huku
ukitumia mtaji kidogo unaoweza kuumudu. Tutakuwa pia na mpango mkakati mzima wa
biashara hizo.
KIINGILIO
ni shilingi elfu 10 tu, na unapata fursa ya kusoma na semina nyingine zote
zilizopita pamoja na fursa ya kuingia semina nyingine zote zitakazofuata bila
kulipa tena kiingilio. Unapewa na kitabu cha michanganuo ya biashara na
ujasiriamali bure. Offa ya kitabu itadumu kwa muda maalumu tu.
Malipo
ni kupitia namba 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo. Tuma
na anuani yako ya GMAIL(isiwe yahoo wala aina nyinginezo) kwa ajili ya
kukuunganisha na blogu ya masomo.
Vitabu navyo vipo kwa anayehitaji tuwasiliane kwa namba hizo hapo juu, kwa SOFTCOPY tuma pesa na anuani yako ya email tutakutumia udownload popote pale ulipo. Kwa HARDCOPY ukiwa Dar tunakuletea mpaka ulipo kwa gharama ya ziada ya sh. 2,000/= na mikoani tunatuma kwa basi au muagize mtu anayefika Dar akuchukulie kutoka kwetu.
Vitabu navyo vipo kwa anayehitaji tuwasiliane kwa namba hizo hapo juu, kwa SOFTCOPY tuma pesa na anuani yako ya email tutakutumia udownload popote pale ulipo. Kwa HARDCOPY ukiwa Dar tunakuletea mpaka ulipo kwa gharama ya ziada ya sh. 2,000/= na mikoani tunatuma kwa basi au muagize mtu anayefika Dar akuchukulie kutoka kwetu.
HARDCOPY TSH. 20,000
SOFTCOPY TSH. 10,000
HARDCOPY TSH. 10,000
SOFTCOPY TSH. 5,000
HARDCOPY TSH. 5,000
SOFTCOPY TSH. 3,000
Kwa maelezo vitabu zaidi tembelea SMARTBOOKSTZ
0 Response to "NAANZA UTUMISHI JANUARI, NIFANYEJE KUWA HURU KIFEDHA AU NIKAKOPE?"
Post a Comment