‘Kazi’ sasa ni ‘ubia’
Wanaume na wanawake wanaotaka kutangaza
huduma zao kwa faida zaidi kwa siku zijazo ni lazima watambue maabadiliko
makubwa sana yaliyotokea katika mahusiano baina ya mwajiri na mwajiriwa.
Muda utafika ambapo “Sheria ya dhahabu” na
siyo “Utawala wa dhahabu” kitakuwa
kigezo kinachotawala katika kutafuta soko la bidhaa na huduma. Pia uhusiano
baadaye kati ya waajiri na waajiriwa wao utakuwa zaidi katika hali ya ubia
ukijumuisha :
(a)
Muajiri
(b)
Muajiriwa
(c)
Jamii wanayoihudumia
Njia hii mpya ya kutafuta soko la huduma
inaitwa mpya kwasababu nyingi. Kwanza, wote mwajiri na mwajiriwa wa wakati ujao
watachukuliwa kama waajiriwa wenza ambao biashara yao itakuwa ni kuhudumia jamii kwa ufanisi . Zamani
waajiri na waajiriwa walibadilishana wenyewe kwa wenyewe, wakiendesha
makubaliano mazuri kabisa waliyoweza kuafikiana kila mmoja bila ya kujali
kwamba katika tathmini yao ya mwisho ukweli walikuwa wakipatana kwa niaba ya upande wa tatu, jamii waliyoihudumia.
SOMA: Uchumi ukishuka na ajira kuwa adimu, ubunifu wa soko la biashara zetu unahitajika.
SOMA: Uchumi ukishuka na ajira kuwa adimu, ubunifu wa soko la biashara zetu unahitajika.
Wakati ujao, wote waajiri na waajiriwa
watatambua kwamba hamna tena upendeleo wa kuendesha mapatano kwa niaba ya wale
waliowahudumia. Mwajiri wa kweli wa wakati ujao atakuwa ni jamii. Hili
linatakiwa kupewa kipaumbele akilini na kila watu wanaotafuta soko la bidhaa
zao kwa ufanisi.
Heshima na huduma ndiyo kaulimbiu ya biashara
leo. Vinafanya kazi kwa mtu anayetafuta soko la huduma zake hata moja kwa moja
zaidi kuliko kwa mwajiri wanayemfanyia kazi, kwasababu katika tathmini ya
mwisho, wote mwajiri na mwajiriwa wanaajiriwa na jamii wanayoihudumia. Ikiwa watashindwa kuihudumia vizuri, watalipa
kwa kupoteza upendeleo wao wa kutoa huduma.
Kipimo
chako cha “UKI” ni kipi?
Sababu ya kufanikiwa katika kutafuta soko la
huduma kikamilifu na la kudumu
imeelezwa kwa ufasaha. Ikiwa kama sababu hizo hazitasomwa, kuchunguzwa,
kueleweka na kutumiwa, hakuna mtu
atakayeweza kutafuta soko la huduma zake kwa njia kamilifu na ya kudumu. Ni
jukumu lako kuuza huduma zako
mwenyewe. Ubora na Kiasi cha huduma zitolewazo na
Imani huduma inayotolewa ndiyo huamua kwa kiasi kikubwa bei na muda wa
ajira. Katika kutafuta soko la huduma kikamilifu(ambapo maana yake ni soko la
kudumu, katika bei muafaka, chini ya mazingira mazuri) mtu ni lazima akubali na kufuata kanuni ya UKI, ambayo
maana yake ni UBORA jumlisha KIASI jumlisha IMANI sahihi ya ushirikiano sawa na
utafutaji soko kamilifu wa huduma. Kumbuka kanuni ya ‘UKI’ lakini fanya zaidi- itumie kama mazoea!
SOMA: Hatua 6 + kanuni ya kuingiza kiasi chochote cha pesa unazotaka maishani.
SOMA: Hatua 6 + kanuni ya kuingiza kiasi chochote cha pesa unazotaka maishani.
Hebu tuichambue kanuni hiyo kuhakikisha
tunaelewa hasa inamaanisha kitu gani.
1. UBORA
wa huduma unamaanisha utendaji kazi wa kila kitu kwa kina, kuhusiana na nafasi
yako, katika hali ya ufanisi mkubwa inavyowezekana, kwa lengo la ufanisi mkubwa
mara zote akilini.
2. KIASI
cha huduma humaanisha TABIA ya kutoa huduma zote unazoweza kutoa, kwa muda
wote, kwa lengo la kuongeza kiasi cha huduma kwa kadiri unavyoongeza maarifa
kupitia vitendo na uzoefu. Msisitizo tena unawekwa katika neno TABIA
3. IMANI
ya huduma humaanisha TABIA ya ukubalifu(kukubali) kitendo cha utengamano kitakachochochea ushirikiano kutoka kwa
washirika na wafanyakazi wenza.
Wingi
wa UBORA na KIASI cha huduma havitoshi kudumisha soko la kudumu kwa huduma zako.
Mwenendo au IMANI ambayo unatoa huduma ni kigezo kikubwa kinachohusika na vitu
vyote viwili, bei unayopata na kiasi cha muda unachoajiriwa.
Andrew
Carnegie alisisitiza kipengele hiki zaidi kuliko wengine katika maelezo yake ya
sababu za kufanikiwa katika kutafuta soko la huduma . Alisisitiza tena na tena
umuhimu wa tabia ya masikilizano-
Alisisitiza kwamba, asingeweza kumvumilia mtu yeyote ambaye hakufanya kazi kwa
roho ya masikilizano licha ya ukubwa wa kazi au ufanisi wa ubora wa kazi yake.
Bwana Carnegie alisisitiza juu ya kila mtu kukubaliana. Kuthibitisha hilo
aliweka thamani kubwa kwenye sifa hii, aliruhusu watu wengi walioendana na
viwango vyake kuwa matajiri sana. Wale ambao hawakuendana ilibidi wawapishe
nafasi wengine.
SOMA: Nguvu na udhaifu wa akili yako, hutokana na kujiamini binafsi au kukosa kujiamini.
SOMA: Nguvu na udhaifu wa akili yako, hutokana na kujiamini binafsi au kukosa kujiamini.
Umuhimu
wa haiba inayokubalika umesisitizwa kwa sababu unamuwezesha mtu kutoa huduma
katika imani sahihi. Ikiwa mtu ana
haiba inayopendeza na anatoa huduma
katika roho ya masikilizano, rasilimali
hizi mara nyingi huziba pengo kwa mapungufu katika vyote, ubora na wingi wa
huduma anazotoa mtu.
Thamani ya Mtaji wa Huduma zako
Mtu ambaye kipato chake chote hutokana na mauzo ya huduma
zake hana tofauti na mfanyabiashara anayeuza bidhaa. Inaweza kuongezewa vizuri
kwamba mtu kama huyo analengwa na sheria zilezile na taratibu kama ilivyokua
kwa mfanyabiashara anayeuza bidhaa. Hili limesisitizwa kwasababu wengi wetu
wanaoishi kwa kuuza huduma zao, hufanya makosa ya kujichukulia wenyewe kuwa
hawahusiki na sheria za taratibu na wajibu unaoambatana na wale wanaojihusisha
katika kutafuta soko la bidhaa.
Thamani halisi ya mtaji wa ubongo wako inaweza kujulikana
kwa kiasi cha mapato unachoweza kuzalisha (kwa kuuza huduma zako). Makadirio ya
haki ya thamani ya mtaji wa huduma zako
inaweza kupatikana kwa kuzidisha mapato yako ya mwaka kwa 16 na mbili ya
tatu, kama ilivyokuwa sahihi kukadiria kwamba mapato yako ya mwaka yanawakilisha
asilimia sita ya thamani ya mtaji wako. Fedha hukodishwa kwa asilimia sita kwa
mwaka. Fedha haina thamani kushinda ubongo, mara nyingi ina thamani ndogo
zaidi.
‘Ubongo’(akili)shindani ikiwa zitatafutiwa soko
kikamilifu huwakilisha aina ya mtaji unaofaa zaidi kushinda ule unaohitajika
kuendesha biashara inayohusika na bidhaa. Hii ni kwasababu ‘ubongo’(akili) ni aina ya mtaji ambao
hauwezi ukashushwa thamani moja kwa moja
kwenye mdororo wa uchumi, wala aina hii ya mtaji hauwezi ikaibiwa wala kupotea.
Zaidi ya hapo, pesa zinazohitajika kuendsha biashara thamani yake ni ndogo kama
mchanga mpaka pale zitakapochanganywa na
akili yenye ufanisi.
Sababu
Kuu 30 za Kuanguka.
Ni
ngapi kati ya hizi zinazokurudisha nyuma?
Maisha ni janga kubwa linalojumuisha wanaume na wanawake
ambao kwa kweli hujaribu na kufeli! Janga hilo lipo katika idadi kubwa
kupindukia ya watu wanaofeli, ukilinganisha na watu wachache wanaofanikiwa.
SOMA: Utajiri huanza na wazo, ukomo wa utajiri hupangwa na mtu mwenyewe akilini.
SOMA: Utajiri huanza na wazo, ukomo wa utajiri hupangwa na mtu mwenyewe akilini.
Nilikuwa na bahati ya kuchunguza maelfi kadhaa ya Wanaume
na Wanawake, kati yao asilimia 98 walikuwa wamewekwa katika kundi la
“waliofeli”. Kuna kitu fulani kisichokuwa sahihi kabisa kuhusu ustaarabu na
mfumo wa elimu unaohusu watu wengi kiasi hicho kupitia maisha kama
walioshindwa. Lakini sikuandika kitabu hiki kwa lengo la kupima mema na mabaya
ya dunia, hilo lingeweza kuhitaji kitabu
chenye ukubwa mara 100 zaidi ya hiki.
Kazi yangu ya kutathmini ilithibitisha kwamba kuna sababu
kuu 30 za kuanguka. Kama utakavyoipitia orodha hiyo, iangalie mwenyewe kipengele
kwa kipengele kugundua ni sababu ngapi kati ya hizi za kuanguka zinazosimama
katikati yako na mafanikio.
1.
KURITHI MAZINGIRA YASIYOFA.
Kama kuna kitu
chochote kinachoweza kufanyika ni kidogo sana kwa watu wanaozaliwa na upungufu
katika nguvu ya ubongo. Filosofia hii hutoa njia moja tu ya kurekebisha
upungufu huu kupitia msaada wa nguvu ya ushirika ‘Master mind’(angalia uk. wa
193). Chunguza kwa faida, hata hivyo kwamba hii ndiyo sababu pekee kati ya
sababu 30 za kufeli ambayo haiwezi kuirekebishwa kirahisi na mtu yeyote.
2.
KUKOSA LENGO LILILOKUWA WAZI MAISHANI.
Hakuna matumaini ya
mafanikio kwa mtu asiyekuwa na kusudi kuu, au lengo dhahiri la kulenga. Watu
tisini na nane kati ya kila mia ya wale niliowachunguza hawakuwa na lengo la
namna hiyo. Pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu
kubwa ya maanguko yao.
SOMA: Nguvu inayohitajika kuweka malengo ya kupata mali na utajiri ni sawa na ile inayohitajika kuleta mateso na umasikini.
SOMA: Nguvu inayohitajika kuweka malengo ya kupata mali na utajiri ni sawa na ile inayohitajika kuleta mateso na umasikini.
3.
KUKOSA NIA THABITI YA KUWA NA MALENGO MAKUBWA.
Hatutoi matumaini kwa
watu wasiojali kabisa kutaka kupiga hatua maishani na asiyekuwa tayari kulipa
gharama.
4.
ELIMU DUNI
Hiki ni kilema
kinachoweza kuondolewa kwa urahisi zaidi. Uzoefu umethibitisha kwamba watu
walioelimika vizuri mara nyingi ni wale wanaojulikana kama ‘waliojijenga
wenyewe’ au waliojielimisha wenyewe. Huchukua zaidi ya shahada ya chuo kikuu
kumfanya mtu kuwa mtu wa elimu. Mtu yeyote aliyeelimika anajifunza kupata
chochote kile atakacho maishani bila ya kuingilia haki za wengine. Elimu haina
maarifa mengi sana, bali maarifa yanayotumiwa kikamilifu na kwa uendelevu. Watu
hulipwa siyo tu kwa kile wajuacho, bali zaidi hasa kwa kile wakifanyacho na kile wakijuacho.
5.
UKOSEFU WA NIDHAMU BINAFSI
Nidhamu huja kupitia
kujizuia binafsi. Hii ina maana kuwa ni lazima udhibiti sifa zote hasi. Kabla
haujadhibiti hali ni lazima kwanza ujidhibiti mwenyewe. Kujidhibiti binafsi
ndiyo kazi ngumu zaidi utakayopambana nayo. Ikiwa hautaishinda nafsi,
utashindwa na nafsi. Unaweza ukaona katika nafsi moja na kwa wakati mmoja watu
wote wawili yaani rafiki yako mkubwa na adui yako mkubwa , kwa kusogea mbele ya
kioo.
6.
AFYA MBAYA.
Hakuna mtu anayeweza
kufurahia mafanikio yanayoonekana pasipokuwa na afya njema . Nyingi ya sababu
zinazoleta afya mbaya hutegemea ustadi na udhibiti. Nazo kwa kiasi kikubwa ni;
· Ulaji
wa vyakula visivyofaa kwa afya.
· Mazoea
mabaya ya kufikiri, kuonyesha hisia hasi.
· Matumizi
mabaya na kuendekeza ngono kupita kiasi.
· Ukosefu
wa mazoezi ya viungo yanayofaa.
· Ukosefu
wa hewa safi, unaotokana na upumuaji usiofaa.
7.
ATHARI ZA MAZINGIRA YASIYOFAA WAKATI WA UTOTO
Kwa kadiri tawi
linavyokunjwa, ndivyo mti nao utakavyoota, watu wengi walio na tabia za
kihalifu, walizipata kutokana na mazingira mabaya na makundi yasiyofaa wakati
wa utoto
SOMA: Uwezo wa akili ya binadamu ni wa ajabu na usiokadirika.
SOMA: Uwezo wa akili ya binadamu ni wa ajabu na usiokadirika.
8.
KUSITASITA.
Hii ni moja ya sababu
kubwa ya kushindwa. ‘Kikongwe kusitasita’ husimama miongoni mwa vivuli vya watu
wote akisubiri nafasi ya kuharibu fursa zao za mafanikio. Wengi wetu huishi
maisha kama waliofeli kwasababu tunasubiri muda wa ‘kuwa sahihi’ kuanza kufanya
kitu fulani chenye manufaa. Usisubiri. Muda hautakaa ‘uwe sahihi’. Anzia pale
uliposimama, fanya kazi na zana yeyote unayoweza kuwa nayo, na zana bora
zitapatikana kadiri utakavyokuwa ukisonga mbele.
9.
KUKOSA UVUMILIVU.
Wegi wetu ni
waanzilishi wazuri lakini ni wamaliziaji wabaya wa kila jambo tunaloanzisha. Na
zaidi, watu ni wepesi wa kukata tamaa katika dalili za mwanzo za kushindwa.
Hakuna mbadala wa uvumilivu. Mtu
mvumilivu hugundua kwamba ‘Kikongwe anguko’ mwishowe huchoka na kutoweka .
Anguko haliwezi kustahimili uvumilivu.
10.
HULKA MBAYA.
Hakuna matumaini ya
mafanikio kwa mtu anayewafukuza watu kupitia tabia hasi.Mafanikio huja kupitia
matumizi ya nguvu na nguvu hupatikana
kupitia ushirikiano wa watu wengine. Hulka hasi hazitavuta ushirikiano.
11.
KUSHINDWA KUZUIA TAMAA YA NGONO
Nguvu ya ngono ndiyo
kichocheo chenye nguvu zaidi kuliko vingine vyote vinavyomsukuma mtu kutenda.
Kwa kuwa ndiyo mhemko ulio na nguvu zaidi, ni lazima udhibitiwe kupitia mageuzi
na kubadilishwa kwenda kwenye mikondo mingine.
12.
HAMU ISIYOTULIZIKA YA KUPATA KITU BILA YA KUTOA CHOCHOTE.
Tabia ya kucheza
kamari huwafanya watu wengi kuanguka .
13.
KUKOSA UWEZO ULIOKUWA DHAHIRI WA MAAMUZI.
Watu wanaofanikiwa
hufikia maamuzi mara moja na kuyabadilisha taratibu ikiwa ni lazima kufanya
hivyo. Watu wanaoanguka hufikia maamuzi mara kwa mara na kwa haraka.
Kutokufanya maamuzi na kuahirisha ni vitu mapacha, kinapokuwepo kimoja, kingine
mara nyingi huwepo pia. Waue marafiki hawa wawili kabla hawajakufunga katika
kinu cha maanguko moja kwa moja.
14.
MOJA AU ZAIDI YA HOFU SITA.
Hofu hizi
zimetathminiwa kwako katika sura ya 15. Ni lazima zifahamike vyema kabla
haujaweza kutafuta soko la huduma zako kikamilifu.
SOMA: Imani mapenzi na ngono ndiyo vitu vyenye nguvu kuliko mihemko mingine yote mikubwa.
SOMA: Imani mapenzi na ngono ndiyo vitu vyenye nguvu kuliko mihemko mingine yote mikubwa.
15.
UCHAGUZI MBAYA WA MWENZA KATIKA NDOA.
0 Response to "SABABU KUU 30 ZA KUSHINDWA KUFANIKIWA, ZIPI ZINAKUVUTA NYUMA USIFANIKIWE?"
Post a Comment