Ndugu msomaji wa blog hii, Karibu tena na leo
napenda kukushirikisha jambo moja ambalo ndilo litakalokwenda kuwa ufunguo
katika kampeni zetu mwaka wote huu wa 2018 tunaokwenda kuuanza masaa machache
yajayo.
Mzunguko chanya wa fedha katika shughuli zetu
za kiuchumi ndio kila kitu, ukiweza kuudumisha hautahangaika tena, utapata
utulivu wa nafsi na kila kitu kitakwenda barabara.
Ili kudumisha mzunguko chanya wa pesa katika
biashara yeyote unayofanya kuna hatua zinazopaswa kuchukuliwa. Nyingi ya hatua
hizo tutazijadili katika kampeni zetu lakini lakini, hatua kubwa zaidi ya zote
ni lazima kwanza mtu umiliki biashara iliyokuwa na uwezo wa kuzunguka haraka,
biashara yenye uhitaji mkubwa kwa jamii, kwa maneno mengine uwe na biashara
ambayo soko lake halina mashakamashaka.
Mwaka huu mpya wa 2018 tumeandaa michanganuo
maalumu ya miradi bunifu yenye fursa za kipekee. Miradi hiyo imefanyiwa utafiti
mkubwa na kuthibitika kuwa na kiwango cha chini kabisa cha hatari(lower risk)
pamoja na uwezekano mkubwa sana wa kuzalisha faida na hivyo kuufanya mzunguko
wako wa fedha kuwa chanya muda wote.
Katika mwaka huu wa 2018 mwezi wa kwanza
tutaanza na mradi mmoja ambao ni mradi wa ufugaji wa kuku. Ijapokuwa ni ufugaji
wa kuku wa kienyeji, siyo ufugaji wa kawaida na uliozoeleka hapana, staili yake
ni mpya na wala haijapata kusimuliwa mahali pengine popote pale, ni kazi ya
ubunifu mkubwa wa kijasiriamali kama ujasiriamali wenyewe unavyotaka kwa mujibu
wa kitabu cha “MICHANGANUO YA BIASHARANA UJASIRIAMALI.”.
Habari nyingi kuuhusu mradi huu zitafichuliwa
kwa wale watakaoshiriki mafunzo haya ambayo yatafanyika rasmi siku ya Jumatano
ya tarehe 3 mwezi Januari 2018 kupitia Blog maalumu ya SEMINA ZA MICHANGANUO pamoja na kundi ‘group’ la Whatsapp kwa namba
0765553030.
Mjadala utaendelea kwa mwezi mzima kabla
hatujahamia kwenye mradi mwingine. Kumbuka tumeandaa miradi/biashara 12
zisizokuwa na mashaka yeyote kuhusiana na ulipaji wake.
Ikiwa utapenda kujiunga na mpango huu,
kiingilio ni shilingi elfu 10 na utapata fursa ya kushiriki semina zote
zitakazofuata pamoja na kusoma masomo ya semina nyingine zilizokwisha pita siku
za nyuma. Ikiwa ulishalipia semina zilizopita hautalipa tena, utakachofanya ni
kunitumia tu namba yako kwa ajili ya kukuunganisha Whatsapp ikiwa utataka kwani
asilimia kubwa ya masomo ya kwenye blogu
ndiyo hayohayo yatakayotumwa whatsapp.
Ili kujiunga, lipa shilingi elfu 10 kupitia
namba 0712202244 au
0765553030, jina, Peter Augustino Tarimo, tuma na anuani yako ya GMAIL, isiwe yahoo wala aina nyinginezo.
Na kama unatumia Whatsapp, nitumie ujumbe huu kupitia whatsapp “NIUNGANISHE
KUNDI LA SEMIA ZA MICHANGANUO” kwa namba 0765553030.
Mwaka mpya huu wa 2018 pia tumetoa OFFA,
punguzo la bei kwa wateja wanaonunua vitabu vyetu 3 katika mfumo wa softcopy
kwa njia ya email. Badala ya kulipa sh. Elfu 18 kwa softcopy za vitabu vyote 3,
utalipa sh. Elfu 15 tu! na kutumiwa vitabu 3 utakavyodownload kwenye simu au
kompyuta yako. Offa itamalizika rasmi tarehe 10 January 2018.
Karibu sana kwenye semina, na nakuhakikishia
hautojutia kamwe kiingilio chako.
Peter Augustino Tarimo
Self help books Tanzania
Simu:
0712202244
Whatsapp:
0765553030
0 Response to "SEMINA: NJIA ZA UHAKIKA ZA KUBORESHA MZUNGUKO WAKO WA FEDHA 2018"
Post a Comment