Sina shaka unawafahamu ama umeshawahi kusikia kuhusu wale waongoza watalii wanaopanda milima mfano wa mlima Kilimanjaro, kwa kimomgo huwa wanaitwa guides. Kupanda kileleni mwa mlima kama Kilimanjaro, mlima Everest au Mlima Kenye isingelikuwa ni kazi rahisi kwa mtu ambaye hata siku moja hajawahi kufanya hivyo. Ingelimchukua muda mrefu kubahatisha huku akipotea na wakati mwingine hata kuporomokea katika mapango ya kale kitendo ambacho kingeliweza hata kuhatarisha maisha yake.
Maguide hawa au waongozaji wapanda milima, wana uzoefu wa
muda mrefu na kazi hiyo, walitumia muda wao mwingi kujifunza mazingira yote ya
mlimani, njia zote, vichochoro na hata kujua ni wapi palipokuwa na hatari za
aina mbalimbali. Huwezi kuwadanganya kitu chochote kuhusiana na upandaji mlima.
Siri ya mafanikio ya upandaji mlima hadi kufikia juu kabisa kileleni wanaijua
wao.
SOMA: Siri 10 alizotumia Aliko Dangote kufika pale alipo.
SOMA: Siri 10 alizotumia Aliko Dangote kufika pale alipo.
Mfano huu wa wanaoongoza wapanda milima unafanya kazi
karibu katika kila nyanja nyingine zote za maisha na biashara ikiwemo.
Waliofanikiwa kimaisha kila sekta wanacho kitu cha kufundisha kwa wale ambao
bado hawajafanikiwa kufikia levo zao. Waliofanikiwa kwenye kilimo mathalani
wanajua mbinu na maarifa mengi yahusuyo kilimo na bila shaka yeyote ikiwa ndio
unaanza shughuli ya kilimo huna budi kuwatafuta ili wakupe ujuzi huo.
Halikadhalika na kwa waliofanikiwa kielimu, waliofanikiwa kibiashara nk.
Ni dhahiri kabisa kuwa sisi binadamu hatuna kabisa muda
wa kutosha hapa Duniani kujifunza kila kitu kutokana na makosa tutakayofanya
katika mchakato wa kusaka mafanikio. Wakati mwingine inabidi kutafuta njia za
mkato(shortcut) na njia hiyo si nyingine bali ni ile ya kujifunza kutoka kwa wengine ambao
walishawahi kupitia hali na mazingira yanayofanana na yale unayojiandaa
kukutana nayo au ambayo tayari unakutana nayo.
Hapa kuna mjadala wa wale wanaodai kuwa mtu unapaswa
kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa tu na wengine hudai mtu unaweza
kujifunza kutoka kwa wote, wale waliofanikiwa na hata kutoka kwa wale
walioshindwa kwa mantiki kubwa kwamba
hata waliofeli nao wanacho cha kufunza kwani utajifunza kukwepa yale
yaliyowafanya washindwe kufanikiwa kusudi usirudie makosa yao tena.
SOMA: Kwanini kufanikiwa kifedha si dhambi na ni kwanini kila mtu anatakiwa afanikiwe.
SOMA: Kwanini kufanikiwa kifedha si dhambi na ni kwanini kila mtu anatakiwa afanikiwe.
Makosa mengi yanaepukika kirahisi kwa kujifunza njia
wengine walizotumia kuyatatua. Unapojifunza, jifunze kutoka kwa watu wenye
mtazamo chanya na uzoefu ndipo utajijengea mazingira yaliyokuwa imara kabla
haujaanzisha kile unachokusudia kuanzisha.
JINSI YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WALIOFANIKIWA
Kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa au walio na uzoefu wa
kutosha siyo jambo gunu. Dhana hii hubeba maana tofauti kulingana na mtazamo wa
kila mtu. Kwa mfano wapo wanaowaita wale wanaoigwa au waaliofanikiwa kama
‘mamentor’, makocha, ‘role models’ nk. na hata unaweza usiwaite jina lolote
lakini ikabakia tu kuwa wewe unafuata mfano wa mtu fulani aliyewahi kupitia
njia unazotamani na wewe uzipitie kusudi uweze kutimiza ndoto yako ya maisha
kutegemeana na ni kwa namna gani unavyojibu swali la mafanikio ni nini.
Mafanikio pia yanaweza yakawa na maana tofauti kutegemea mtu na mtu.
Wajasiriamali waliofanikiwa kwa mfano pamoja na wasanii
mashuhuri duniani ndio wanaoongoza kuwa na wafuasi wengi wanaoiga mifano
yao(role models). Kufuata mfano wa mtu siyo lazima uonane naye ana kwa ana
mzungumze hapana, zipo njia nyingi ikiwemo hata kusoma na kutazama taarifa zake
kutoka vyombo mbalimbali vya habari na vitabu.
SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka.
SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka.
Hasahasa vitabu imekuwa ni njia nzuri sana ya watu kuiga mifano ya watu maarufu na
waliofanikiwa. Watu kama kina Bill Gates, Warren Buffet, George Weah, Ronaldo,
Messi, Barack Obama, Alli Kiba, Ophra Winfrey, Wema Sepetu, Said Salim
Bakhressa, Diamond, Reginald Mngi, Mohamed Dewji na wengineo wengi.Wote hawa
wasingeliweza kumfikia kila mtu mmojmmoja anayehitaji kufuata mifano yao
isipokuwa kwa njia ya vyombo vya habari, vitabu na magazeti.
Chagua mtu wako wa kujifunza kutoka kwake na siyo lazima
awe ni mtu maarufu, kuna hata watu wanaochagua kujifunza kutoka kwa wazazi wao
au ndugu zao wa karibu waliokwishapitia uzoefu fulani au mafanikio.
………………………………………………….
Ndugu
msomaji wa makala hii, hata wewe na mimi pia tunavyo vitu, uzoefu au maarifa
watu wengine wayoweza kuiga kutoka kwetu. Mimi binafsi kwa mfano, nina uzoefu
wa miaka zaidi ya 12 katika biashara ya rejareja hususani DUKA LA REJAREJA.
Yeyote
sasa anayefikiria kuanzisha au tayari anayo biashara ya DUKA au biashara yeyote
ile ya rejareja, hana haja tena ya kutumia zaidi ya miaka yote hiyo 12
akijifunza ni kipi kinachofanya kazi na ni kipi kisichofanya kazi. Tayari
nimeweka uzoefu wangu wote katika kitabu unachokiona hapo chini baada ya
maelezo haya.
Njia
ya haraka sana ninayoweza kutuma kitabu hiki kwako ni kwa kupitia email kama
softcopy(PDF). Bei ni sh. Elfu 5 tu na zinatumwa kupitia namba za simu 0712202244 au
0765553030 jina Peter Augustino Tarimo
Ikiwa
pia utataka kitabu cha karatasi, hardcopy unaletewa mpaka ulipo kwa sh. Elfu 12
ukiwa Dar es salaa. Mikoani agiza mtu
anayekuja dar akuchukulie.
SIMU: 0712202244
WASSAP:
0765553030
TUPO: Mbezi kwa Msuguri karibu na stendi.
0 Response to "JINSI YA KUPATA MAFANIKIO MAISHANI: USIPANDE MLIMA BILA KIONGOZI"
Post a Comment