Ni tangu enzi za dahari, kitu hiki kinachoitwa pesa au
fedha hakijawahi kuwa rahisi kupatikana, kila enzi utasikia kuna misemo na
lugha mbalimbali kuhusiana na ugumu wa upatikanaji wa fedha kwa mfano enzi za
Mwalimu Julius Nyerere tulisikia misemo kama vile,uhujumu uchumi wakati wa
Azimio la Arushaa, uhuru na kazi kipindi cha Uhuru, Siasa ya ujamaa na
kujitegemea na hata kufunga mikanda baada ya vita ya Idd Amin Dada kule Uganda.
Zikaja enzi za Mheshimiwa Ali Hassana Mwinyi Rais wa
awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukazuka msemo mashuhuri sana
ulioitwa RUKSA. Alipoanza kutawala Mzee Benjamin William Mkapa tukasikia,
maneno kama vile, Ukapa, uchumi wa sayansi na teknolojia na mengine yaliyofanana
na hayo. Rais Jakaya Kikwete yeye aliingia na maisha bora kwa kila mtanzania
akimaanisha kila mtu awajibike kuyapata maisha bora. Na Mheshimiwa Rais Joseph
Pombe Magufuli misemo karibu inayofanana na ile ya enzi za Mkapa imeibuka
ukiwemo huu wa vyuma vimekaza, hapa kazi tu nk.
Maneno
na misemo yoote hii inamaanisha kitu gani?
Misemo yote hii katika awamu zote 5 za uongozi ukiitazama
kwa umakini haimaanishi chochote zaidi ya Mzunguko wa fedha, nikimaanisha fedha
kuingia na fedha kutoka hazina kuu ya serikali na mifukoni mwa wananchi. Kila
sera au kaulimbiu ina malengo ya kutaka kuelezea hisia za wananchi au serikali
juu ya hali ya kiuchumi iliyokuwepo katika kipindi husika na maneno hayo
yanaakisi hali ya kiuchumi iliyopo. Hali kuwa ngumu katika mzunguko wa fedha
iwe ni serikalini, katika biashara au mfukoni mwa mtu binafsi maana yake ni
kwamba fedha zinazoingia ni chache kuliko zile zinazotoka.
Kiuchumi kuimarisha mzunguko wa fedha au kwa maneno mengine
kudumisha mzunguko wa fedha uwe chanya ni lazima serikali, biashara au mtu
binafsi achukue hatua za kubana matumizi au kuwa na kitu kinachoitwa nidhamu ya
pesa ya hali ya juu. Na zoezi hili ndilo linalofanywa na serikali za awamu
mbalimbali katika nyakati tofauti ndipo sasa tunashuhudia misemo kama hiyo
kuibuka.
Kwa mfano Serikali inapolegeza sana ukusanyaji wa fedha
maana yake inakuwa dhaifu lakini wananchi wananeemeka na hiki ndicho kilichotokea
enzi za Mzee Ruksa na Mzee kikwete, serikali inapoamua kubana matumizi, kukusanya
fedha kikamilifu na kudumihsa nidhamu ya hali ya juu ya matumizi, serikali
huimarika kifedha japo wananchi hupata shida kidogo kwa kuona fedha hamna
mifukoni mwao.
Hali kama hiyo ndiyo inayotokea hata katika biashara
zetu, biashara kama serikali ilivyo, inapaswa kuingiza pesa nyingi na kwa
nidhamu ya hali ya juu ikiwa itataka kuimarika. Kinyume chake ni kuanguka au
kufa kabisa.
Somo hili la fedha ni muhimu sana kwa kila mtu, kampuni, taasisi
na hata serikali yenyewe. Ni lazima kuelewa kwamba fedha hata siku moja
haijawahi kuwa rahisi kupatikana, ukiona imekuwa rahisi basi na ujue kuna
matokeo au athari nyuma yake. Fedha inayopatikana kiurahisi nyuma yake ni
lazima kuna habari ya utovu mkubwa wa uwajibikaji, wizi, magendo, ujanja
ujanja, au uhujumu uchumi wa namna moja ama nyingine.
Kwa mfano, ukiona mfanyakazi katika biashara yako “anatanua
sana” nikiwa na maana kwamba anatumia fedha ovyo, basi ujue anaihujumu biashara
yako, atapata wapi fedha kirahisi namna hiyo? Na hali ni hivyohivyo katika
taasisi zingine na serikalini pia. Wema usizidi uwezo, mweleze msaidizi wako wa
kazi ukweli kwamba fedha haijawahi kuwa rahisi hivyo kupatikana, na ikiwezekana
mtimue mapema kabla hali kwako haijawa tete zaidi. Michezo michezo yake mwishowe
wote, wewe na yeye mtajikuta mkiomba mia ya kula.
Tunashuhudia viongozi kadhaa wa serikali na taasisi za
umma waliokosea katika matumizi ya fedha au kushindwa kusimamia vizuri matumizi
ya fedha za serikali miaka mingi iliyopita wakiwajibishwa sasa mahakamani, kosa
la kushindwa kusimamia fedha halijawahi kumwacha mtu yeyote yule salama,
usipowajibika sasa, utawajibika hata baada ya kifo chako, wanao, wajukuu au
hata vitukuu watakuja kuwajibika kwa makosa yako hayo kwa kisingizio bandia cha
laana
ya mabibi na mababu.
Ni wangapi wanaowajibika kwa makosa ya kipesa waliyotenda
wazazi wao huko nyuma? Inawezekana leo unaishi katika lindi la umasikini wa
kutisha kwa sababu tu mzazi hakuwa na nidhamu ya pesa. Kinachotakiwa sasa ni
wewe kutorudia makosa hayo vizazi vyako navyo vikaendelea kuipata ‘laana hiyo’.
Enzi zitapita, zitakuja nyingine lakini hakuna enzi hata
moja utakuja kusikia eti fedha imekuwa rahisi kupatikana bila ya kufanya kazi
kwa nidhamu na maarifa. Ili uweze kudumisha mzunguko mzuri(chanya) wa fedha
katika vyanzo vyako inatakiwa kuchukua hatua mbalimbali za kinidhamu na ubanaji
matumizi, hakuna njia ya mkato hata kidogo na hii ni kila mahali popote pale
duniani, usije ukaona nchi zilizoendelea ukafikiri walitapanya ovyo mapato yao,
wasingefika pale walipo.
Kabla hujanunua itu chochote kile hebu jiulize kwanza, “Hivi kitu hiki ninachonunua au kulipia,
kina manufaa gani kwangu na hasa katika kuongeza mzunguko wangu wa fedha
badalaa ya kuupunguza?”
………………………………………….
Ndugu msomaji wangu, nashukuru kwa kuchukua muda wako wa
dhamani kusoma hapa, hayo ni machache lakini mengi zaidi tumeyaweka katika
vitabu vyetu hivi hapa chini pamoja na machapisho mengineyo mbalimbali katika
private blogu yetu ya Michanganuo na kundi la whatsapp la michanganuo online.
Vitabu hivi unaweza kuvipata kimojakimoja au vyote kwa
pamoja ukiwa popote pale kwa njia mbili zifuatazo.
1. SOFTCOPY(PDF) kupitia
email yako unavidownload na kusoma katika simu au kompyuta yako
2.
HARDCOPY(VYA KARATASI). Unaletewa kitabu/vitabu popote pale
ulipo Dar es salaa kwa gharama ya ziada ya sh. 2000/=. Kama upo mikoani unaweza
ukaagizia kwa mtu anayefika Dar au ukatuma fedha na sisi tukatuma vitabu kwenye
basi.
SIMU: 0712202244
WASAP: 0765553030
JINA: Peter
Augustino Tarimo
TUPO
MBEZI KWA MSUGURI KARIBU NA STENDI YA DALADALA
Softcopy sh. 10,000/=
Harcopy sh. 20,000/=
Softcopy sh. 5,000/=
Harcopy sh. 10,000/=
Softcopy sh. 3,000/=
Harcopy sh. 5,000/=
0 Response to "KAMA FEDHA HAIJWAHI KUWA RAHISI KUPATIKANA KWANINI UCHEZEE PESA?"
Post a Comment