Kabla sijaanza mada hii ya leo ya kwanini
ufugaji wa kuku wa nyama maarufu kama Broilers wana faida kidogo sana, hebu
kwanza nizungumzie kwa kifupi kuhusiana na soko la mazao mbalimbali ya kilimo
na mazao ya mifugo. Miongoni mwa maswali mengi ninayokutana nayo kutoka kwa
wasomaji wa blogu hii ni haya hapa chini.
NITAPATA WAPI… Soko la kuku wa nyama, soko
la nyanya, soko la sungura, soko la matikiti maji, soko la mahindi, soko la kuku
na mayai ya kienyeji, soko la mananasi, soko la choroko, soko la kuku wa mayai,
soko la pilipili hoho nk. orodha ni ndefu lakini kwa bahati mbaya sana
waulizaji wengi wa maswali haya huuliza wiki chache, moja au 2 tu kabla ya
mazao yao kuvunwa au kuingizwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa.
Kwa kweli utaona kwa mtindo kama huo, ni
dhahiri kabisa kuwa kilimo na ufugaji ambavyo ndiyo injini ya viwanda tunavyoimba kila siku zitaendelea
kuonekana ni biashara kichaa kila siku wakati shughuli za kilimo na ufugaji ni
miongoni mwa biashara zenye fursa kubwa na nzuri ambazo bado kabisa hazijaguswa,
fursa endelevu ya kutengeneza pesa au hata ya mtu kuweza kupata utajiri wa haraka kuliko kwenda kupoteza senti zako chache kwa kucheza kamari.
Kanuni kuu ya biashara ni hii hapa; LIJUE
VIZURI SOKO LA BIDHAA/HUDUMA ZAKO KABLA HATA HAUJAANZA KUIFANYA BIASHARA
ULIYOKUSUDIA KUIFAYA. Fanya kwanza utafiti(feasibility study). Kufanya utafiti
wa soko la biashara yako kumeelezwa vizuri sana katika kitabu cha MICHANGANUO
YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, nashauri ikiwa hujui namna ya kufanya utafiti na
una wazo la kuanzisha biashara au kiwanda kidogo basi kitafute kitabu hicho bei
yake ni shilingi elfu 10 tu, unapata softcopy yake utakayoisoma kama unavyosoma
sasa hivi hapa.
KWANINI
UFUGE KUKU WA NYAMA, NA NI KWELI HAWANA FAIDA AU WATU WANATIA CHUMVI TU
KUKUKATISHA TAMAA HUKU WAO WAKITENGENEZA HELA?
Biashara ya ufugaji wa kuku wa kisasa kwa
ujumla ni biashara yenye sifa zifuatazo, Ni biashara kwanza inayohitaji mtaji
wa uhakika(capital intensive) hapa nitafafanua kidogo, simaanishi kila
anayeanza basi anatakiwa kuwa na mtaji mkubwa sana hapana, bali namaanisha kuwa
unapoianzisha basi uwe na uhakika idadi unayoanza nayo una kiasi cha mtaji
unaotosha kuwahudumia mwanzo mpaka mwisho bila ubabaishaji wowote ule sijui
leo umewapa pumba, kesho magimbi ya kuchemsha, keshokutwa kiporo cha ugali, hapana. Bajeti yake ya chakula na vifaa
vyote uwe nayo kabisa mkononi si ya kuungaunga.
Sifa nyingine ya biashara hii ni ‘very risky’
au kwa maneno engine ina hatari kubwa, kosa kidogo tu unaweza ukala hasara ya
mwaka ukalaani kabisa ufugaji wa kuku wa kisasa. Hapa elimu na maarifa
mbalimbali yanahitajika kukabiliana na hilo. Na sifa ya tatu kuku wa kisasa
nikiwa na maana ya kuku wa mayai na kuku wa nyama wana faida kubwa sana, ni
miongoni mwa miradi duniani inayolipa ajabu!. Mbali na sifa hizo nyingine mbili
hapo juu ufugaji wa kuku wa kisasa unaweza ukakufanya kuwa milionea katika muda
ambao watu wanaweza wakahisi umeshukiwa na muujiza.
KWANINI
UFUGE KUKU WA NYAMA?
· Bei
ya vifaranga wa kuku wa nyama sokoni siyo kubwa sana ukilinganisha na aina
nyinginezo za ufugaji wa kuku kama vile kuku wa mayai(layers) na kuku chotara.
· Mabanda
ya kuku wa nyama huchukua nafasi ndogo, kuku mpaka 10 katika square metre 1 ya
mraba, hata maeneo yaliyobanana sana mijini kama dar e s salaa mtu anaweza
akafuga bila wasiwasi.
· Chakula
cha kuku wa nyama ni rahisi hata mtu kutengeneza mweyewe ikiwa unajua
kanuni(formula) ya uchanganyaji wa chakula cha kuku wa nyama. Isitoshe kuku wa
nyama hawali chakula mifuko mingi sana kipindi chote cha ukuaji wao kutokana na
kipindi hicho kuwa ni kifupi, wiki 4 mpaka 6 tu. Kwa ujumla ulishaji wa kuku wa nyama
ni rahisi.
· Biashara
ya kuku wa nyama sokoni haisumbui sana ikiwa utawakuza kuku wako katika uzito
unaokubalika sokoni. Hutapata washindani wengi kwani kuku ni bidhaa inayopendwa
sana duniani na huliwa na kila mtu.
· Faida
na mapato ya kuku wa nyama ijapokuwa ni kidogo lakini kutokana na muda mfupi
faida hiyo inayochukua mpaka kupatikana kwake bado ni biashara inayolipa na ni
nzuri.
NI
KWELI UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA UNAKATISHA TAMAA?
Binafsi mimi hilo nalipinga kuku wa nyama si
kweli kwamba faida yake inakatisha tamaa, kwanza kitu watu wengi wasichofahamu
ni kwamba katika biashara yeyote ile kuna gharama kuu za aina mbili, zile za
kuanzishia biashara ambazo unanunulia vifaa na miundombinu yote kwa ujumla,
halafu kuna zile gharama za uendeshaji za kila siku ambazo ndizo hubainisha
faida ya mradi kila siku.
Sasa watu wengi hutegemea baada ya msimu
mmoja tu wa ufugaji wa kuku wa nyama waweze kurudisha gharama zote hizi mbili
jambo ambalo ni gumu na lisilowezekana, labda iwe ni katika mazingira fulani fulani
tu ambayo nimeyazungumzia vyema katika moja ya mchanganuo kwenye kifurushi cha
michanganuo 3 niliyoandaa spesho kwa mfugaji yeyote yule makini wa kuku wa aina
zote.(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS). Kifurushi hiki nilichokizindua wiki hii kina
mipango ya biashara ya kuku mitatu, kuku wa kisasa wa mayai, kuku wa kienyeji wa
mayai na kuku wa kisasa wa nyama.
Umewahi kufanya biashara ya kuuza vocha zasimu za mkononi? Vipi faida yake, ndogo au kubwa? Ili upate faida nyingi
unapaswa kufanya nini? Uuze kiasi kikubwa siyo. Na kuku wa kisasa ni hivyo
hivyo, wanalika sana kwa hiyo isingelikuwa rahisi faida yake iwe kubwa sana vinginevyo kila mtu
angekimbilia kufuga na isingekuwa biashara tena. Katika ulimwengu wa viwanda
kuna kitu wanaita, economies of scale,Wachina kwa mfano ujanja huu huutumia sana, Mchina akigundua bidhaa ina soko kubwa na la uhakika atadili nayo kwa udi na uvumba kuizalisha
kwa wingi kiasi ambacho ile faida ndogondgo inayoingia hatimaye hulundikana upesi na kugeuka utajiri
mkubwa.
Nimefanya makusudi kuandaa mpango wa kuku 100
wa nyama na wala siyo 500 au 1000. Katika mchanganuo huo wa kuku 100 tu unaonyesha ipo faida lakini kwa mtu
anayetaka mafanikio ya usiku mmoja ni lazima atajiunga katika lile kundi la wanaobeza
ufugaji wa kuku wa kisasa wa nyama akidai ni biashara kichaa isiyokuwa na
faida. Ukifanikiwa kuuona jaribu kuucheki mchanganuo huo vizuri kwani
umechambuliwa kwa umakini wa hali ya juu baada ya ubishani mkali na wanaopinga
biashara hii.
Biashara ni mahesabu bwana asikuongopee mtu,
na usipoyapiga vizuri utaishia kusema haina faida, mahesabu hapa simaanishi calculus hapana, simple maths, hesabu za
kichwa ambazo hata darasa la nne anamudu kuzifanya.
Katika kifurushi hiki cha (MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) kila
mchanganuo uliokuwemo ndani una upekee wake, kimezima kabisa kiu ya maswali
yote yanayohusiana na biashara ya ufugaji wa kuku wa aina mbalimbali kama vile;
· Gharama
za kuanzisha miradi ya kuku
· Faida,
hasara na mapato ya ufugaji wa kuku kwa ujumla
· Nitaanza
na kuku wangapi wa mayai?
· Nataka
kufuga kuku wa kienyeji mtaji nianze na shilingi ngapi?
· Kuku
wa mayai wa kienyeji kwa mwaka hutaga mayai mangapi?
· Kuku
wa mayai na kuku wa nyama ni yupi aliye na faida zaidi.
· Kuku
wa mayai tangu kifaranga mpaka kuuzwa gharama yake ni shilingi ngapi?
· Nikiwa
na laki tatu mchanganuo wa kuku wa kienyeji upoje?
· Gharama
za ufugaji wa kuku chotara aina ya kuroila ni kiasi gani?
· Nifuge
kuku wa kienyeji au wa kisasa?
Michanganuo yote 3 ipo katika mfumo wa
softcopy(PDF). PDF ya mchanganuo wa ufugaji wa kuku wa mayai, PDF ya kuku wa
kienyeji na mchanganuo wa tatu ni ufugaji wa kuku wa kisasa wa nyamaPDF. Kila
mchanganuo bei yake ni shilingi elfu 10 lakini kwa idadi yangu ya watu wa
mwanzo nitawapa kifurushi hiki kizima kwa bei ya ofa ya shilingi elfu 10 tu.
Idadi yangu ikitimia kila mchanganuo utauzwa peke yake kwa bei ya kawaida ya sh,
elfu 10.
Offa nyingine kubwa nitakayotoa kwa idadi
yangu maalumu ya wateja wa mwanzo watakaonunua kifurushi cha MKOMBOZI CHICKS
PLAN 3PACKS ni offa ya kuunganishwa bure kwenye kundi langu la kushauriana la
WHATSAPP(MASTER MIND GROUP) ambalo kila
siku tunashauriana na kujadiliana maswala mbalimbali kuhusu miradi yenye fursa kubwa,
michanganuo ya biashara bunifu, na njia za kuongeza mizunguko ya fedha katika
biashara zetu.
Ndani ya group pia unapata masomo yote (complete course on business planning) kwa kiswahili rahisi, pamoja na masomo mengine ya ziada yanayotolewa kila siku usiku kupitia wasap, Vitabu mbalimbali pamoja na templates/vielezo vya mpango wa biashara unavyoweza kujaza maneno yako tu ukakamilisha kuandika mpango wa biashara yako kwa njia rahisi na ya haraka.
Kumbuka ada ya kawaida ya kujiunga na group
hili bila ofa ni sh. 10,000/=. Mle utakutana na magwiji katika tasnia ya ufugaji kuku, ‘uombe ushauri gani usishauriwe?’ Ma
experts kama kina Frank Mapunda watakaokufundisha ABC zote za biashara ya uuzaji na ufugaji wa
kuku wa aina zote kitaalamu. Ofa hiyo nayo haitadumu muda mrefu ni ya kuwahi mapema.
.................................................................
Ukihitaji vitabu vyetu mbalimbali tembelea; SMARTBOOKSTZ
SIMU: 0712202244
Wasap: 0765553030
0 Response to "KUKU WA NYAMA BROILERS: KWANINI FAIDA NA GHARAMA ZA UFUGAJI ZINAVUNJA MOYO?"
Post a Comment