Ni hali inayojitokea popote pale palipo na mapambano ya aina yeyote. Wapigania uhuru wote duniani walikutana na hali kama hiyo, na hata mimi na wewe leo tunaopambana na hali mbalimbali za kimaisha ni lazima tukubali ukweli huu kwamba mapambano yeyote huanza na mtu mmojammoja lakini hakuna ushindi mpaka pale watu hao mmojammoja watakapoamua kukaa na kuunda umoja (Master Mind Group).
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.
Vita ya kutafuta uhuru hawakuanza Mwalimu
Nyerere, Jomo Kenyetta, Obote, Mugabe, Lumumba na wengineo, hapana, kabla yao
yalikuwepo mapambano kama hayo mengi mfano wa akina Kinjekitile na Majimaji,
Maumau, nk. Lakini kwanini hawakuweza kuwashinda Wakoloni? Sababu kubwa ilikuwa
ni kukosa Umoja! Hawakuwa na kundi la kushauriana(mastermind group) la uhakika.
Umeona katika Sura ya 8 ya ya kitabu cha
Think & Grow Rich(Fikiri Utajirike) umuhimu wa kuwa na umoja(kundi) pamoja
na kufanya maamuzi thabiti. Mapambano ya Uhuru wa Marekani yalianza muda mrefu
watu wakipambana mmojammoja lakini nguvu
ya maana ilikuja kujitokeza baada ya “Mababa wa Taifa hilo kuja kugundua kuwa,
kumbe bila ya umoja, ushirikiano, hakuna Ushindi wowote ule wa kweli.
SOMA: Muda biashara itakaorudisha faida.
SOMA: Muda biashara itakaorudisha faida.
John Hancock, Samuel Adams na Richard Henry
Lee walianzisha wazo la mawasiliano ya pamoja kati ya makoloni yote 13 ambalo
hatimaye lilikuja kuzaa uhuru tunaoushuhudia leo hii Marekani. Kabla ya hapo
hakukuwa na watu walioweka mioyo yao, akili, roho na mwili pamoja katika uamuzi
mmoja kusuluhisha matatizo yao.
Leo nimeandika haya kwa lengo la kuonyesha
umuhimu wa kufanya kazi kama kundi. Wakati mwezi huu ukianza tulitangaza
kuanzisha semina maalumu za michanganuo ya biashara zenye ubunifu wa kipekee
kwa njia ya Whatsapp, pamoja na zoezi hili kuchelewa kidogo hata hivyo leo
tarehe 19 tumeianza rasmi na tayari kundi la whatsapp limeshaundwa. Katika
kundi hilo tutajadili mada mbalimbali zinazohusiana na;
· Michanganuo
ya biashara 12 zenye fursa za kipekee.
· Jinsi
ya kuongeza mzunguko wa fedha katika biashara zetu.
· Jinsi
ya kuandaa mipango ya biashara kwa kina.
· Mada
yeyote ile inayohusiana na Ujasiriamali, biashara na maendeleo binafsi itakayoibuliwa
na mwanachama.
Unapojiunga na kundi hili unapata vitu
vifuatavyo bila malipo ya ziada.;
· Kitabu
cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali katika lugha ya Kiswahili(softcopy)
· Kitabu
mashuhuri zaidi cha jinsi ya kuandika mpango wa biashara katika lugha ya
kiingereza.
· Templates(Vielezo)
za mpango wa biashara za Kiswahili na za kiingereza zitakazokuwezesha kuandika
mpango wa biashara yako kwa muda mfupi.
· Kuunganishwa
na Blogu maalumu ya michanganuo ya private bure.
SOMA: Jinsi ya kujiunga na Darasa la michanganuo online.
Kundi la Whatsapp ni njia rahisi na nzuri zaidi ya kuwasiliana kwa haraka na ambayo kila mwanachama anapata fursa ya kutoa mchango wake kwa wanakundi wenzake wote tofauti na njia
Kundi la Whatsapp ni njia rahisi na nzuri zaidi ya kuwasiliana kwa haraka na ambayo kila mwanachama anapata fursa ya kutoa mchango wake kwa wanakundi wenzake wote tofauti na njia
zingine kama email ambazo ni ‘admin’ peke yake mwenye fursa hiyo.
Ili kujiunga na kundi la MICHANGANUO ONLINE,
tuma ujumbe kwenye Whatsapp kupitia namba 0765553030 unaosema; “NIUNGANISHE NA
GROUP LA MICHANGANUO”. Nitakuunganisha kwanza na kundi la MAPOKEZI, kisha baada
ya malipo ya kiingilio ambacho ni sh. Elfu 10, unaunganishwa moja kwa moja na
kundi la Michanganuo online pamoja na kupata vitu vingine vyote
vilivyoorodheshwa hapo juu.
SOMA: Utambulisho rasmi wa semina ya Michanganuo ya biashara.
SOMA: Utambulisho rasmi wa semina ya Michanganuo ya biashara.
Karibu njoo tushirikiane kwa karibu zaidi,
haijalishi uelewa wako wa michanganuo ya biashara ni kiasi gani,
tunawakaribisha kila mtu, uwe hujui kabisa maana ya mpango wa biashara na hata
ikiwa ni mtaalamu uliyebobea ndio tunakuhitaji haswa, kwani lengo letu ni kila
mmoja ajifunze kutoka kwa mwenzake na hii ndiyo sababu kubwa ya kuanzisha kundi
la Wassap ili kila mmoja aweze kutoa mchango wake.
0 Response to "NGUVU YA USHIRIKA, UMOJA NI NGUVU"
Post a Comment