Hatimaye jana ijumaa tarehe 19/1/2017 ndiyo
ilianza rasmi ile semina au mafunzo ya Michanganuo ya biashara 12 zilizo na
fursa kubwa ya kuleta faida na kusababisha mtiririko wa fedha kuwa chanya
katika mwaka wote wa 2018.
Mafunzo haya yametokana na utafiti
tulioufanya mwaka jana 2017 katika kampeni yetu iliyoitwa “Make your self great again” au “Jirudishie ukuu wako tena” ambapo tulibaini kwamba watu wengi huwa
tunashindwa kutimiza malengo yetu tunayojiwekea kila mwaka kutokana na sababu
mbali mbali lakini kubwa ikiwa ni mzunguko mdogo wa fedha katika biashara zetu.
Kwa hiyo tukaona itapendeza zaidi ikiwa tutajaribu kutafuta biashara bunifu 12
tutakazochanganua pamoja na washiriki watakaoamua kujiunga na mafuzo hayo
katika mwaka mzima wa 2018.
UFUNGUZI
JANA ULIVYOKUWA
Kwanza Admin alianza kama saa 11 jioni hivi
kuunganisha katika kundi majina ya washiriki ambao tayari walishatuma namba zao
za wasap pamoja na kulipia kiingilio cha shilingi elfu 10, Kuna makundi mawili,
la MAPOKEZI na kisha lile lenyewe la MICHANGANUO ONLINE ambalo sasa wanaingia
tu wale waliokamilisha malipo yao na kuanza kujifunza.
Washiriki wengi walikuwa na shauku ya kuanza
kujadili mada lakini kutokana na admin kuwa na shughuli nyingi muda huo za
kuadd majina ya washiriki, ilibidi achelewe kidogo mpaka ilipofika kama saa 1
na nusu hivi jioni ndipo sasa mjadala ukaanza rasmi. Tuliweka kwanza baadhi ya
sera za group na tukakubaliana kuwa muda wa kuanza uwe ni saa 3 mpaka saa 4
usiku kwani watu unakuta pilikapilika nyingi zimepungua.
Darasa litaendelea tena leo, ila samahani
kama wewe unayesoma hapa siyo mshiriki, utanisamehe kwani siwezi kutaja
chochote kuhusiana na mada, mchanganuo wa mwezi tuliowasilisha au hata yaliyomo
kwenye masomo hayo kwa undani, maswala hayo yote ukipenda kuyapata bila chenga
njia rahisi ni kujiunga na darasa.
Kama umechelewa kuanza huna sababu ya kuwa na
wasiwasi kwani, vitu vyote muhimu utavikuta katika blogu yetu ya ‘private’,
utakuta downloads zote hapo na nyingine unatumiwa moja kwa moja katika email au
wassap.
Unapojiunga unapata vitu vingi kwa gharama
kidogo ukilinganisha na mafunzo yeyote ya ujasiriamali yanayotolewa hapa
Tanzania kupitia hii mitandao ya kijamii. Kwa shilingi elfu 10 tu unapata vitu
vifuatavyo;
1. Masomo ya semina, jinsi ya kuandaa
michanganuo, michaganuo bunifu yenye uwezo mkubwa wa kuboresha mzunguko wa
fedha pamoja na chochote kile kuhusiana na ujasiriamali/biashara mshiriki
atakachowasilisha.
2. Michanganuo bunifu 12 ya kila mwezi katika mwaka wote wa 2018
3. Kitabu cha jinsi ya kuandika mpango wa
biashara cha Kiswahili(softcopy)
4. Kitabu mashuhuri zaidi cha jinsi ya
kuandaa mpango wa biashara cha kiingereza kinachoaminiwa katika vyuo vingi
duniani(softcopy)
5. Templates(vielezo) unavyoweza kutumia
katika uandaaji mpango wako kwa urahisi na haraka zaidi, unajaza tu maneno yako.
6. Michanganuo(Samples) ya Kiswahili na
kiingereza unayoweza kuitumia kama mifano wakati ukijifunza kuandika wakwako.
7. Masomo au semina zopte zilizopita kwenye
blogu yetu ya private pamoja na material mbalimbali unazoweza kudownload hapo
free.
8. Fursa ya kushiriki mafunzo mengine yote
kwa mwaka wote huu wa 2018 bila kulipa gharama yeyote ile ya ziada.
Zana hizi 8 unakabidhiwa pindi tu umalizapo kutimiza
taratibu za kujiunga, Ikiwa wewe ulishawahi kujiunga na semina zetu siku
zilizopita, tafadhali tujulishe tukuunganishe kwani wewe tayari una sifa zote
za kuingia katika mafunzo haya na hautalipa tena kiingilio kingine.
Mwisho nikukaribishe sana leo, njoo tujifunze pamoja saa
3 usiku pale ‘MICHANGANUONI ONLINE’, WHATSAPP: 0765553030
SIMU: 0712202244
Peter Augustino Tarimo.
0 Response to "UZINDUZI WA SEMINA YA MIPANGO YA BIASHARA BUNIFU 2017 ULIVYOFANA MTANDAONI"
Post a Comment