Kabla mitandao ya kijamii haijashika kasi, miaka ya nyuma
kidogo, mtu ilikuwa kujifunza ujuzi mbalimbali kama vile jinsi ya kupika
vyakula vya aina mbalimbali vikiwemo vitafunio vya chai, ice cream, koni,
lambalamba, na hata pilau na biriani ni lazima kwanza utafute chuo kilichotoa
mafunzo ya upishi au wakati mwingine umtafute mtaalamu aliyekwishapitia mafunzo
hayo akufundishe. Kulikuwa na vitabu pia, japo upatikanaji wake ulikuwa mgumu
kidogo.
Mambo yamebadilika sana siku hizi, binafsi siku moja
katika pitapita yangu mitandaoni nikakutana na tangazo la kozi za utengenezaji
vyakula mbalimbali kwa njia ya whatsapp, nikawa najiuliza watu hawa
wanafundishaje mtu akaelewa? au labda wanatumia njia ya video? Japo sikuwa na
interest ya kujifunza mimi binafsi lakini nikasema kama ni mafunzo ya kweli
basi nitampa ‘wife’ ayafuatilie.
Mapishi ya chapati kwa mfano ni kitu cha kawaida sana
katika kaya nyingi Tanzania lakini chagamoto kama vile chapati kuwa kavu na
ngumu ni moja ya suluhisho wakufunzi hawa wa kwenye whatsapp intaneti hutoa
kirahisi mno! Sikuwa nalijua hilo kabla nikidhani ni wajanja wajanja tu
wanaotaka kula hela za watu kumbe wanamaanisha kile wanachokisema. Siyo kila
watoa mafunzo mtandaoni ni matapeli.
Baada ya kujiunga wasap na kuingizwa katika group la
masomo, wakufunzi wake walianza kunitumia maelezo mbalimbali na picha na namna
ya kupika vitu mbalimbali kuanzia, bagia za dengu, mkate mwupe, mkate wa brown,
sambusa, maandazi, mkate wa kumimina, chapati za maziwa, half cake, kababu za
nyama na mayai, maandazi ya kuoka, donuts, visheti, vitumbua, kachori,
kalimati, skonzi, chapati, nk. Wana
masomo mengine pia ya vyakula na vitu vinavyouzwa katika biashara nyingi
ndogondogo kama vile pipi, biskuti, koni, lambalamba, zulia, sabuni, barafu,
kashata, na mapishi ya vyakula mbalimbali vikiwemo pilau, biriani nk.
Maelekezo yale yalikuwa mafupi na yanayoeleweka vizuri
kiasi kwamba shakashaka niliyokuwa nayo juu ya mafunzo haya ziliisha kabisa.
Wanakupa mahitaji yote, Maelezo na mwisho jinsi ya kuandaa. Nilimfuata wife na
kumjulisha juu ya mafunzo yale akafurahi sana. Hakuamini macho yake kwani vitu
vingi ambavyo alikuwa akiviona tu vikiuzwa mabarabarani sasa aliweza kuvipika
mwenyewe bila wasiwasi wowote. Na ukiwa na dukuduku lolote au labda kitu fulani
tuseme hamira huelewi utatumia ya aina gani, ya chenga au ya unga, basi
unauliza na mkufunzi anakupa maelekezo ya kutosha.
Mafunzo kama haya ni fursa kubwa sana kwa mjasiriamali
mdogomdogo anayehangaika kupata mtaji. Kwa kuwa anao mtaji kidogo sana, hawezi
akaanzisha biashara kubwa itakayohitaji vitu vingi vya kuanzia lakini pia hata
ikiwa anataka kuanzisha biashara ndogondogo ya chakula inayohusisha aina hizo
za vyakula au vitafunwa, masomo haya ya gharama nafuu na yasiyohitaji muda
maalumu bali hitaji lake tu ni mtu kuwa na simu yenye intaneti hasa smartphone,
yanaweza kuwa msaada mkubwa sana kumtoa pale alipo na kumfikisha mahali pengine
juu zaidi.
Kitu cha msingi nilichoona mtu anaweza akafanya ikiwa
anataka kuyatumia mafunzo hayo kuanzisha biashara ndogo ni kujifunza kitu
ambacho anajua ataweza kupata soko lake kwa urahisi. Kila mtu hukaa mazingira
tofauti na mwenzake, inawezekana eneo unaloishi wewe ukiuza mandazi yanatoka
sana lakini skonzi haziwezi kutoka kabisa, halikadhalika na mwingine yawezekana
eneo analokaa vitu kama sambusa na chapatti vina soko la uhakika ushinda vitu
vingine kwa hiyo hapo ni suala la kufanya utafiti wa soko kwanza hata kabla ya
kuanza mafunzo yenyewe kusudi uwe na uhakika unakwenda kujifunza nini kukepa
gharama ya muda na pesa ya kujifunza kila kitu hata kile ambacho huendi ‘kudili’
nacho.
Siyo vibaya pia ukafanya mchanganuo wa biashara yako
ndogo kwa kuainisha mahitaji yote na bei zake, kisha ukaorodhesha mbinu
utakazotumia kufanikisha uuzaji wa chakula au vitafunwa vyako kama vile, “nitatembeza
kwa chombo safi mtaani huku nikitangaza, vitafunwa, vitafunwa”, “Nitaweka chombo
safi barazani wateja wafuate wenyewe watakapoviona” au “Nitatembeza katika
maduka ya rejareja kuomba wanipe oda ya kuwapelekea kwa jumla” Usisahau pia
kukisia hesabu zako ikiwa utapata faid kiasi gani kwa siku, wiki na mwezi,
ukiona hautaweza kupata faida kulingana na mahitaji yote utakayotakiwa kuwa
nayo basi ni bora ukafikiria tena upya ikiwa utabadilisha aina ya chakula au
vitafunwa hivyo au kutafuta biashara nyingine kabisa.
Utengenezaji wa vitu hivi sijaona mahali ambapo wanasema
ni lazima utumie mashine au vyombo vya gharama kubwa tofauti na maneno ya watu
wengi mitaani kwamba kuoka kitu kama mkate au skonzi ni lazima uwe na ma oven makubwa
makubwa, wanapendekeza mashine na vifaa mbadala kabisa kuanzisha kiwanda chako
kidogo cha utengenezaji wa vyakula.
Nimetaja kiwanda makusudi kwani huwa Napata maswali mengi
sana toka kwa wajasiriamali wadogo wanaotaka kuanzisha viwanda vidogovidogo
lakini wanakuulizia habari za ni wapi watapata mashine kubwakubwa ambazo
najiuliza, watamudu vipi kuzinunua hata ikiwa watajua ziliko? Siyo vibaya kujua
zinapatikana wapi, lakini ninachomaanisha hapa ni kuwa mfanya biashara mdogo
fikiria makubwa lakini “just start small”,
anza kwa kiwango kidogo kwanza ili usijeukakata tamaa njiani mambo yakionekana
kuwa magumu kidogo kwani safari ya ujasiriamali ina kupanda na kushuka kabla
hujafika kileleni.
……………………………………………………
Ndugu msomaji wa makala hii, unaweza kupata mafunzo yetu
kwa kina kupitia vitabu mbalimbali vifuatavyo. Softcopy kwa njia ya email ni sh. elfu 10 hicho cha kwanza, elfu 5 cha pili na elfu 3 cha tatu.
Hardcopy ni sh. elfu 20, elfu 10 na elfu 5. Ulkiletewa ulipo Dar utaongeza sh. elfu 2. Mikoani agiza mtu anayefika Dar au tunaweza kukutumia kwa basi.
SIMU: 0712202244
WASAP: 0765553030
SIMU: 0712202244
WASAP: 0765553030
1.
2
3
Kwa maelezo na vitabu zaidi tembelea ukurasa huu ufuatao,
0 Response to "UZURI WA MAFUNZO YA MAPISHI YA VITAFUNWA, CHAKULA LAMBALAMBA, WHATSAP MTANDAONI"
Post a Comment