Sri ya mafanikio ya kila biashara hutegemea sana usimamizi,
uendeshaji na soko lako. Kila biashara ni lazima iwe na idara mbalimbali
zinazofanya kazi pamoja kusudi biashara iweze kutimiza malengo yake kama
mmiliki wake alivyokusudia ni sawa na ilivyo kwa mwili wa binadamu kila kiungo
na umuhimu wake.
Idara hizi kwenye biashara zipo nyingi zaidi ya soko, uendeshaji
na usimamizi na unaweza ukazitaja zote au kuzijua kwa urahisi kwenye vipengele
mbalimbali katika mpango wa biashara lakini idara zinazotajwa mara kwa mara
zaidi ni hizi, USIMAMIZI, SOKO na UENDESHAJI.
Naziita idara lakini unaweza ukaziita jina lolote kulingana na
mazingira ya biashara yako kwani kwa mfano ukitaka kuanzisha biashara ya mtu
mmoja unaweza usiseme idara ukasema tu ni shughuli za usimamizi, masoko na
uendeshaji.
Kwa kweli kama ilivyo kwa viungo vya mwili wa mwanadamu vitu vyote
3 pamoja na hivyo vingine nilivyosema kwenye biashara ni muhimu lakini hapa
tunatakiwa tulenge zaidi kile kinachohusika moja kwa moja na kazi ya
kusababisha fedha ziingie kwenye biashara kwa kuwa lengo letu ni kutafuta hasa
mbinu za kuongeza mzunguko wa fedha kwenye biashara zetu
SOMA: Njia
ya mafanikio ni nyeupe kwa mjasiriamali mdogo anayeweza kuvikwepa vidakizi
hivi.
Hebu fanya zoezi lifuatalo, chukua vitu vyote hivi vitatu, viweke
mahali kisha kila kimoja kipe mazingira yote sawa na mwenzake, kama ni bajeti
kila moja ipe bajeti sawa na mwenzake, kama ni muda hivyohivyo. Kisha baada ya
hapo biashara yako izalishe bidhaa au huduma nyingi lakini wateja wawe wachache
sana kiasi cha kutisha.
Hebu niambie ukiwa kama meneja au mmiliki wa biashara ni hatua gani za kwanza utakazoanza kuzichukua
kabla ya nyingine?
Bila shaka yeyote utanijibu kwamba utaanza kutafuta soko la bidhaa
au huduma hizo kwa udi na uvumba kusudi zisizidi kukudodea. Sidhani kama
utaniambia eti utaongeza uzalishaji wa bidhaa huku zikiendelea kuoza, wala
kuajiri wasimamizi zaidi wakati bidhaa zimejaa stoo hazina wanunuzi.
Tunapojiuliza
swali, ni ipi siri ya mafanikio ya biashara kati ya usimamizi, soko na
uendeshaji, Soko au kwa maneno mengine wateja ndiyo
kiini cha mafanikio ya biashara yeyote ile. Sisemi idara nyingine hazina
umuhimu hapana, ila soko ndiyo kitu muhimu zaidi katika kuhakikisha biashara
inafanya vizuri na kuleta mafanikio yaliyokusudiwa na mwanzilishi wake au
waanzilishi.
SOMA: Je,
wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya 4 madogomadogo?
Biashara zetu huwa zinashindwa kutengeneza mzunguko chanya wa
fedha au kwa maneno mengi kutengeneza utajiri haraka kutokana na sababu hii
kuliko sababu nyingine zozote zile na hii hutokana na sababu kwamba tunashindwa
kuelewa ni nini hasa maana ya utafutaji wa masoko ya biashara zetu tukidhani
kuwa utafutaji wa soko ni kile kitendo cha kutangaza biashara tu peke yake kama
vile kutangaza redioni, mtandaoni au kwenye magazeti na vipeperushi kumbe siyo,
ni zaidi ya hivyo.
Ukichunguza kwa umakini tabia za watu waliofanikiwa maishani ni
pamoja na hulka yao ya kujitangaza sokoni, kujijengea majina makubwa yanayodumu
akilini mwa wateja ambao hatimaye wanafanya kazi ya kuwatangaza kwa watu
wengine bure bila ya wao kuingia gharama zozote zile za ziada.
Dhana ya kutafuta soko ni pana kidogo, utafutaji wa soko ni
mchakato unaoanzia pale unapopata wazo la biashara unayotaka kuifanya,
unapoanza kutengeneza bidha zako au huduma mpaka dakika ya mwisho unapokuwa
ukimkabidhi mteja na yeye kukupa fedha yake. Ukikosea hata hatua moja kwenye
mchakato huo mzima na ujue umeharibu au kupunguza ufanisi wa shughuli za
kimasoko za biashara yako na hivyo kuidumaza isikuletee faida haraka.
SOMA: Umuhimu
wa kuligawa soko la biashara yako katika makundi/vipande tofauti
Mchakato huo wa kimasoko ninaouzungumzia maarufu kwa kimombo kama
4ps, unajumuisha; BIDHAA, BEI, MATANGAZO na ENEO (MAHALI), Product, Price, Promotion and Place. Hii inamaanisha, kutoa huduma
au bidhaa sahihi, katika eneo sahihi, kwa bei sahihi na kwa wakati sahihi.
Ikiwa kimoja kati ya hivi kitakosekana basi biashara au kampuni
italazimika kuingia hasara kubwa na wakati mwingine kufa kabisa. Biashara
nyingi hukosa mzunguko mzuri wa fedha kwa sababu tu ya kukosa mpangilio mzuri
wa shughuli hizi 4 za kimasoko. Ukitaka kuanza biashara au unaendesha biashara
ya zamani siri kubwa ya kufanikiwa ni kuhakikisha unatengeneza mpango wako wa
masoko mapema hata kabla hujaanza biashara yenyewe.
Kumbuka mteja ndiyo kiini cha soko na thamani ya bidhaa au huduma
hutegemea mtazamo wa mteja na lengo lake ni kumfanya huyu mteja aridhike na
kuendelea kumfanya kuwa mteja mtiifu kwako au biashara yako.
SOMA: Utafiti
wa soko la biashara yako/Upembuzi yakinifu-1
Hebu tuone mchakato mzima wa kimasoko ulivyo na jinsi unavyoweza kuutumia
katika biashara yako kuifanya yenye kutiririsha fedha zaidi ndani kuliko
kuzitoa nje.
1. Tafuta kiini cha bidhaa/huduma zako,
kiini hiki ni ile faida atakayoipata mteja, jiulize ikiwa kama
faida hiyo itawashawishi wateja kununua. Dalili ya utajiri huanzia pale
unapoona umebuni bidhaa ama huduma inayohitajika mno na wateja, wateja hawawezi
kuishi bila huduma/bidhaa hiyo.
Na hata kama ikiwa ni anasa mtu wa kawaida anayoweza kukwepa
kuinunua basi matajiri au wanaomudu kuinunua hiyo bidhaa/huduma hakikisha
hawapati kabisa sababu ya kuacha kuinunua. Usiishie tu kuhangaika kutangaza
kila mahali bidhaa au huduma utapoteza
fedha na muda wako bure ikiwa kama huna sababu nzito ya wateja kununua toka
kwako.
2. Wajue wateja wako.
Ni nani atakayenunua bidhaa yako, anahitaji nini, thamani ya
bidhaa/huduma yako kwake ni kitu gani. Ukivifahamu vitu hivyo bayana utakuwa na
uhakika kwamba bidhaa/huduma zako ni sahihi kwake na malengo yako pia ni sahihi
3. Tambua washindani wako.
Fahamu bei zao, huduma na bidhaa zao na ulinganishe na zile
zakwako ili uweze kupanga bei muafaka.
4. Fanya Tathmini ya Eneo utakalouzia bidhaa/huduma zako.
Ukizingatia ikiwa kama wateja wako watakuwa tayari kufika eneo
hilo bila vikwazo vyovyote, zingatia pia gharama zake na ukubwa wa biashara. Je
lina faida zipi zinazolandana na biashara yako?
5. Tengeneza Mkakati wa Mawasiliano/Matangazo
Njia yeyote ile ya matangazo utakayotumia unatakiwa uhakikishe
unawafikia wateja wako watarajiwa na kuhakikisha kwamba faida za bidhaa au
huduma ulizoainisha zinaeleweka vyema na kupewa kipaumbele cha kwanza.
6. Hakikisha vipengele vyote vinne, BIDHAA, BEI, MATANGAZO na
ENEO vinahusiana na kutegemeana na havipingani mahali popote pale.
Kuwekeza pesa zako kwenye biashara bila ya kulizingatia hili hauna tofauti na
mtu anayeendesha gari angali amefumba macho.
Unapoanzisha biashara yako au bidhaa mpya sokono ni lazima
uhakikishe unazingatia vipengele vyote vinne kwa usawa ijapokuwa unaweza ukafika
mahali ukaamua uzingatie kimoja au viwili zaidi ya vingine kulingana na
utakavyoona umuhimu wake katika kufanikisha zaidi biashara yako.
SOMA: Kukuza
biashara yake haraka, mjasiriamali mdogo anapaswa ajue vitu hivi 10
Nahitimisha somo hili la leo kwa kusema kwamba, SOKO au utafutaji
wa soko la biashara yako ni kitu cha kuangalia kwa umakini wa hali ya juu hata
kama ikiwa biashara ni ndogo kiasi gani, tenga muda wa kutosha na fedha kwa
shughuli zako za masoko angalao hata asilimia 10% ya mauzo yako yote iende
kwenye masoko kwani soko ndilo linalohusika na uletaji wa fedha katika biashara
moja kwa moja kuliko shughuli nyinginezo zozote katika biashara yako. Ndiyo
siri kubwa zaidi ya kufanikiwa biashara yako kuzidi hata usimamizi, uendeshaji,
fedha, mauzo na idara nyingine zote katika biashara yako
......................................................
TAARIFA MUHIMU!
1. Nikukumbushe kuhusiana na ile OFFA ya vitu 12 bado ipo ingawa
inakaribia kufika mwisho wake. Offa hii unalipa ada ya mwaka kujiunga na group
la masomo sh. Elfu 10 kisha nakutumia vitabu na michanganuo ya biashara kamili,
jumla vitu 12 papo hapo kama uonavyo katika orodha pale chini mwisho.
2. Nakutumia pia masomo mbalimbali yenye maudhui ya fedha tuliyokwishajifunza
tangu group linaanza mpaka sasa hivi.
3. Nakuunganisha na group la masomo ya fedha & semina za
Michanganuo ya biashara ikiwa unapenda kama hupendi nakutumia tu offa zako.
Semina za jinsi ya kuandika hatua kwa hatua
Michanganuo ya biashara bunifu zenye fursa kubwa ni kila wiki na zinaaza wiki
hii. Tutachanganua biashara zinazolipa haraka kwa mtaji kidogo. Ni fursa nzuri
ya kujifunza kuandika mpango wowote ule wa biashara kwa gharama nafuu kabisa.
Siyo lazima ziwe ni biashara za mtaji kidogo
ama zinazolipa haraka lakini tutajitahidi kuonyesha ubunifu wa hali ya juu
mjasiriamali anaoweza kuutumia katika kuigeuza biashara hata isiyokuwa na fursa
kubwa ikawa biashara inayolipa sana.
Ikiwa unahangaika kutafuta wazo bora la
biashara inayolipa unakaribishwa kwani katika mawazo mengi tutakayochanganua
huwezi ukakosa wazo hata moja utakalofanyia kazi likakupa matokeo makubwa. Au
hata ukapata mbinu mbalimbali za kiubunifu utakazoweza ‘kuapply’ kwenye
biashara yako unayoifanya sasa hivi.
Kulipa ada tumia namba zangu hizi, 0712202244 au
0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo na baada ya malipo tuma ujumbe kwa
meseji au watsap usemao, “NATAKA OFFA
INAYOKARIBIA MWISHO”
ORODHA
YA VITU 12 VYA OFFA INAYOKARIBIA MWISHO WAKE NI HII HAPA CHINI;
1.
COURSE/SEMINA: (compiled
complete course) ya Jinsi ya
kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa
kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili
2.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
5.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili
6.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani na ndio
hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
7.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers - kwa
kiswahili
8.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
9.
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za
saruji- kwa
kiswahili
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. Kuunganishwa Group la
masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka
hatukuunganishi)
Imeandaliwa
na:
Peter Augustino Tarimo
0712202244
0765553030
0 Response to "IPI SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA KATI YA USIMAMIZI, SOKO NA UENDESHAJI?"
Post a Comment