Jinsi ya kuanzisha kampuni ya ulinzi hakuna
tofauti na namna biashara nyingine zote zinavyoanzisha isipokuwa tu ni lazima
upitie wizara ya Mambo ya ndani au makao makuu ya jeshi la Polisi ili
kuwathibitishia uwezo wako uliokuwa nao kimtaji, umiliki wa silaha, na rekodi
zako kiusalama kwani wanapendekeza zaidi kuwa na rekodi nzuri kama kutokuwa na
rekodi za kutenda uhalifu nk. Pia watendaji wa kampuni inafaa zaidi wawe
wamepitia mafunzo ya kijeshi au wastaafu kutoka majeshi mbalimbali na walio na
rekodi safi.
Jeshi la Polisi watakapohakikisha una sifa za
kupewa kibali cha kuanzisha biashara ya ulinzi binafsi ndipo sasa unaweza
kuanza kufanya mambo mengine kama vile kuandaa mpango wa biashara yako
utakavyokuwa pamoja na kutafuta walinzi watakaolinda malindo mbalimbali ya
wateja. Ni lazima pia uhakikishe umekata leseni, kuwa na namba ya mlipa kodi
TIN namba, eneo la ofisi la kudumu kampuni yako ya ulinzi itakapokuwa
ikiendeshea shughuli zake pamoja na timu yako ya usimamizi na wafanyakazi.
Katika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI, kuna mpango wa biashara ifuatayo ya Ulinzi binafsi iitwayo NYUKI
SECURITY SERVICES. Hapa chini ni muhtasari wake ukiangazia yale mambo muhimu
tu, mchanganuo wake kamili unapatikana katika kitabu hicho.
KAMPUNI YA ULINZI.
Nyuki Security Services.
Muhtasari.
Nyuki
Security Services ni kampuni itakayowahakikisha
wateja wake na mali zao ulinzi wa uhakika. Inatarajjia kuanza rasmi mwaka 2013
chini ya wamiliki wake, bwana Silas John na William Wambura; wote wawili ni wastaafu kutoka Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania TPDF
na Polisi katika vyeo vya Meja Jenerali na Sajenti.
Kampuni
itajihusisha na utoaji wa huduma za ulinzi katika ofisi mbalimbali za
mashirika ya umma na binafsi, maduka ya
watu, majumbani na katika shughuli mbalimbali
za mikusanyiko.
Mtaji
wa kuanzia utapatikana kutoka kwa
wamilliki wenyewe kwa kutoa jumla ya shilingi milioni 11 pamoja na mkopo wa
muda mrefu benki, kiasi cha shilingi milioni 10. Kwa kuanza watahudumia
jiji la Dar es salaam na baadaye katika mikoa mingine Tanzania.
Biashara
hii inafunguliwa kipindi muafaka kwani
ongezeko la shughuli za kiuchumi hasa kupanuka kwa sekta binafsi na serikali
kujiondoa katika biashara ndio kunazidi
kushika kasi. Nyuki watalenga kundi la
ofisi na magodown ya makampuni binafsi
katika juhudi zake za kukamata sehemu kubwa ya soko la ulinzi katika jiji la Dar es salaam.
Wafanyakazi
watakaoajiriwa na Nyuki
watachukuliwa kutegemeana na mahitaji yaliyopo tu, hakuna wafanyakazi
watakaoajiriwa bila kupewa lindo isipokuwa wale wa akiba ambao ni watatu tu.
Kampuni
inatarajia kupata mauzo mazuri na faida
mwaka wake wa kwanza na mauzo hayo
yataongezeka mara dufu ifikapo
mwaka wa tatu. Itakapofika mwaka wa tatu
kampuni imepanga kukaribisha wabia ikiwa ni juhudi za kuongeza mtaji wake ili
iweze kulifikia soko la nje ya mkoa wa Dar es salaam.
1.1 Dhamira kuu.
Nyuki Security
imedhamiria kuwahakikishia wateja
wake ulinzi wa uhakika pamoja na mali zao kwa kuajiri wafanyakazi walioiva kimafunzo
na wenye rekodi nzuri.
1.2 Malengo ya
kampuni.
Mafanikio
ya kampuni yatategemea kutimizwa kwa malengo yafuatayo;
(i)
Kufikisha mauzo yapatayo shilingi millioni
244 mwaka wa tatu.
(ii)
Kupata wateja wakudumu wapatao 12 ifikapo
mwaka 2015.
(iii)
Kuajiri
walinzi wa kudumu wapatao 23
ifikapo mwaka 2015
(iv)
Kupata faida ipatayo shilingi milioni 60 ifikapo mwaka 2015.
(v)
Kufikisha huduma zetu mikoani tukianza na Morogoro na Pwani
kuanzia mwaka 2015
1.3
Siri za mafanikio.
Nyuki
pia watahakikisha yafutayo yanatekelezwa katika kuhakikisha mafanikio yanapatikana.
· Kuajiri
wafanyakazi wenye uzoefu na mafunzo ya kutosha.
· Kuwalipa
wafanyakazi mishahara mizuri na kwa wakati.
· Kuwatembelea
wafanyakazi wawapo lindoni(patrol) mara kwa mara kujua matatizo au udhuru, hivyo
kubadilishana na wafanyakazi wa akiba.
· Sare(Yunifomu)
kwa kila mlinzi yenye nembo ya kampuni na wakati wote kuhakikisha wanakuwa
nadhifu na wakakamavu.
…………………………………………..
Kwa
mahitaji ya vitabu kutoka Self Help Books Tanzania tembelea; SMART BOOKSTANZANIA
Semina
za michanganuo pia zinaendelea katika group la whatsapp la MICHANGANUO ONLINE,
email na blogu ya private karibu tujifunze kwa kina jinsi ya kuchanganua
biashara pamoja na mzunguko wa fedha kwenye biashara zetu kila siku saa 3 usiku
mpaka saa 4.
SIMU:
0712202244
WHATSAPP:
0765553030
Je kama haujawahi kupitia jeshi lolote hauruhusiwi kumiliki kampuni ya ulinzi?
ReplyDeleteUnaruhusiwa ila ni lazima katika timu yako wale key person kuwe na watu waliopita katika majeshi
DeleteNaomba link ya group
ReplyDeleteKaribu kiongozi tuwasiliane 0712202244
Delete