Alianza biashara yake kama ilivyokuwa ada kwa
wajasiriamali wengine wote wadogo wadogo wanapoanza, kwa kukodisha kioski
kidogo cha mabati ya kontena, kidogo usije ukafikiri labda ni saizi ya kontena
zima la futi 40 hapa. Mfano wake kama umewahi kuona vibanda hivi vya kuuzia
vocha au kutoa na kuweka pesa kwenye simu vinavyowekwa kwa muda(temporally)
katika maeneo yasiyoruhusiwa rasmi na serikali kwa urahisi wa kuvihamisha pindi
lolote linapotokea. Hata kusimama wima ilikuwa ni shughuli.
Na mimi ndiyo maeneo ninakopita kuelekea
stendi ya basi kwa hiyo huwa namuona pale kila mara nipitapo akihangaika na
kompyuta yake ndogo, pembeni ameweka kiprinta kidogodogo pamoja na vifaa
vingine vya steshenari. Ilikuwa ni biashara ya stationary lakini kwa haraka
haraka kama hukutazama vizuri unaweza ukasema ni kibanda cha kuingiza nyimbo
kwenye simu. Dada wa watu akapiga kazi kama mwaka na kitu hivi, mara siku
napita pale nikakuta kesha hama, kahamia upande wa pili mahali palipokuwa na
fremu ya duka ilyohamwa siyo siku nyingi, sasa palikuwa pa kutosha hata hewa
alikuwa akivuta kwa kujinafasi.
Niliendelea kufuatilia maendeleo ya huyu dada
kila nilipokuwa nikipita pale kwani niliona alikuwa na mwenendo fulani hivi
usiokuwa wa kawaida ambao nitaeleza baadaye kidogo katika makala hii hii. Miezi
mitatu tangu ahamie pale kabla haijamalizika nikagundua tena mabadiliko mengine
ofisini kwa huyu dada wakati nikipita jambo lililonishawishi nitafute sababu ya
kwenda pale nijifanye nahitaji kitu ili nimsome vizuri na mambo yake haya
yasiyotabirika. Dada sambamba na vile vifaa vya steshenari alikuwa ameweka
kabati dizaini fulani hivi kama la chipsi lakini lina ngazi mpaka chini za
kupanga vinywaji mbalimbali, juu aliweka chipsi na vyakula vingine kama nyama
za mishikaki, vitafunwa na ndizi za kukaanga. Kwa kweli vilikuwa vinavutia.
Ilikuwa ni biashara ya chakula na vinywaji ndani ya biashara ya stationary.
Sijui aliwaza nini dada huyu, nadhani watu wengi walikuwa wakimshangaa sana
wengine wakibeza na wngine kusifia ila yeye hakujali, aliendelea kupiga kazi.
TABIA YAKE YA AJABU!
Nilikuahidi nitakueleza tabia yake ya ajabu.
Hufanya maamuzi yake haraka sana akihisi ni maamuzi sahihi na kuchelewa
kuyabadilisha, tabia iliyokuwa muhimu sana kwa mjasiriamali makini ambaye
kufanikiwa kwake ni lazima kutokee hata kama siyo leo wala kesho. Akiona uamuzi
alioufanya siyo sahihi au unampeleka kwenye hasara badala ya faida hachelei
kuubadilisha mara moja na mwingine uliokuwa na tija.
Halafu isitoshe hafanyi hivyo kichwakichwa,
hupima kwanza, na mfano ni pale unapoona anaamua kuchanganya biashara ya
chakula na steshenari akijua kabisa hawezi kukurupuka kuifunga mara moja
stationary yake angali hajui kama biashara ya vyakula na vinywaji itamletea
mapato ya kutosha au la.
Bado naendelea kumfuatilia dada huyu nyendo
zake mpaka nijue hatima yake ni nini, nakuahidi nitaendelea kukupa matokeo ya
ufuatiliaji wangu huu kwa kadiri mapya yatakavyokuwa yakiendelea kujifunua
kwani naamini kabisa dada huyu anayo stori nzuri ya kusimulia. Kumbuka ni wiki
hii hii tu nilipopita pale na kumkuta akipanga panga vinywaji kwenye friji lake
nilipojifanya nakwenda kutoa fotokopi pale.
Mwenendo wa huyu dada kilichonifanya uniguse
kiasi hiki ni jinsi nilivyouhusianisha na yaliyowahi kunikuta mimi binafsi
katika safari yangu ya ujasiriamali, kweli kuna wakati inabidi tujifunze
kutokana na makosa tufanyayo ijapokuwa njia hiyo ni chungu na ndefu. Mimi
nyakati fulani niliwahi kufanya kosa kubwa sana la kuachana na biashara niliyokuwa
nikiifanya kwa matumaini kuwa biashara mpya iliyokuwa mbele yangu ingeweza
kunipa mapato makubwa kushinda ile ya zamani wakati nilikuwa na nafasi nzuri tu
ya kufanya kama huyu dada wa shoka alivyofanya. Matokeo yake nayajua mwenyewe,
ipo siku nitakusimulia lakini kwa kweli hayakuwa mazuri kama nilivyokuwa
nimedhania.
Uzoefu huu unafanya kazi vilevile hata na
kwenye ajira, muulize mtu aliyeachana na ajira yake ghafla kwa matumaini ya
kufanya biashara ya ndoto yake atakusimulia, ingawa inawezekana alikuja
kujinasua lakini hebu muulize ilikuja kumchukua muda gani mpaka kurudisha tena
hali yake ya zamani, kama alikuwa akila nyama kila mwisho wa wiki muulize baada
ya kuachana na ajira yake kimhemko, je nyama aliiona tena? Hivyo yafaa tuwe
makini sana tunapofanya (mabadiliko)transitions katika shughuli zetu na hususan
biashara tunazozifanya bila kujali kama biashara hiyo ya awali inatupa fedha
kiasi gani.
…………………………………………
Mpenzi msomaji wangu , naendelea kukuletea
makala za kina katika blog yako hii, makala ambazo kwa kweli kama utakuwa
ukizifuatilia mara kwa mara hutabakia kama ulivyo, ni kazi ninayoifanya kwa passion(kutoka
moyoni kabisa) na wala si kama nasaka pesa kama vile mtu mwingine anavyoweza
kufikiria. Ndiyo ni kweli tumeweka kiingilio kwa semina au malipo kwa baadhi ya
vitabu vyetu kwa yule anayehitaji huduma hizi kwa kina kabisa lakini ni
kutokana tu na kuzifanya huduma hizi ziweze kuwa endelevu kama vile ambavyo
ungependa kibatari chako kiendelee kuwaka kwa kutia ndani yake mafuta ya taa
kidogo.
Ili uweze kuwa karibu kabisa na mimi, Peter
Augustino Tarimo pamoja na timu au kundi langu la kushauriana MASTERMIND GROUP
la MICHANGANUO ONLINE, na wewe kuwa miongoni mwa kundi hilo, toa kiingilio
kidogo cha shilingi elfu 10 tu, mjasiriamali ni lazima unapotoa fedha yako hata
kama ni kidogo lakini uhakikishe unapata thamani halisi inayozidi pesa uliyotoa,
hiyo ni sheria(principle) namba 1 katika kutengeneza nidhamu ya hali ya juu ya
fedha, somo tunalosoma kila siku kundini.
Kundini tunajifunza pia mambo mengi ikiwamo
namna ya kuchanganua biashara mbalimbali pamoja na michanganuo yenyewe halisi
ya biashara bunifu za kipekee zilizokuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza mzunguko
chanya wa fedha. Kundi lina wataalamu na wazoefu waliobobea katika fani
mbalimbali za ujasiriamali kama vile ufugaji wa kuku aina zote, tunao watu kama
kina FRANK MAPUNDA ambao hakuna kitu kinachowashinda katika ufugaji wa kuku
aina zote.
Njia ya pili ya kuwa karibu zaidi na Peter na
kundi lake ni kwa kusoma vitabu vyetu vya self help books Tanzania, bonyeza
maandishi hayo kuviona vitabu vyote, unaweza kununua kimoja kimoja au vyote kwa
pamoja na vingine ni free, hulipi chochote. Vile vya kununua ukitaka vyote 3 ni
sh. Elfu 18 tu, unatumiwa kwenye email yako na kuvisoma jinsi unavyosoma hapa
baada ya kutuma pesa kwa njia ya simu. Ukitaka vya karatasi tuwasiliane
nitakupa utaratibu wa kuvipata.
Siku ya leo Jumapili ya tarehe 4 Feb. 2018,
Kundini tunajifunza somo la jinsi ya kuufanya mtiririko wa fedha katika biahsra
zetu kuwa chanya, kwa mada isemayo hivi;
0 Response to "NIMEIPENDA STAILI ALIVYOJIONGEZA DADA HUYU NA BIASHARA YAKE YA CHAKULA"
Post a Comment