UTAJIRI HUENDA KWA WALIOTAYARI KUTAJIRIKA KAMA MAJI YAENDAVYO BAHARINI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UTAJIRI HUENDA KWA WALIOTAYARI KUTAJIRIKA KAMA MAJI YAENDAVYO BAHARINI


FIKIRI UTAJIRIKE SURA YA 9 SEHEMU YA I
SURA YA 9
MSIMAMO
Nguvu Endelevu inayohitajika kushawishi Imani.
(Hatua ya 8 kuelekea utajiri)

Msimamo ni kigezo muhimu katika njia ya kugeuza shauku kuwa katika kipimo chake cha fedha. Msingi wa msimamo ni nguvu ya utashi. Utashi na shauku zinapochanganyika pamoja vizuri hutengeneza pea isiyokatalika. Watu wanaokusanya utajiri mkubwa kwa ujumla huitwa wenye damu baridi na wakati mwingine wasiokuwa na huruma. Mara nyingi wanashindwa kueleweka. Kile walichokuwa nacho ni nguvu ya utashi ambayo huichanganya na uvumilivu na kuitumia kama msingi wa shauku yao ya kuhakikisha ukamilishaji wa malengo yao.

Henry Ford kwa ujumla amekuwa akichukuliwa sivyo kama mtu asiyejali na mwenye damu baridi. Mkanganyiko huu ulitokana na tabia ya Ford ya kufuatilia mipango yake yote kwa msimamo. Wengi wa watu wapo tayari kutupilia mbali nia na malengo yao na kukata tamaa katika dalili za mwanzo za upinzani au mkosi. Wachache huendelea licha ya upinzani wote mpaka wanafikia lengo lao. Wachache ndio kina Ford, kina Carnegie, kina Rockfellers na kina Edson.

Panaweza pasiwe na kiashiria cha sifa kwa neno “ Msimamo” lakini sifa hii inafananishwa na Carbon kwa chuma cha pua.

Kutengeneza utajiri kwa ujumla huhusisha matumizi yote ya vigezo 13 ya filosofia hii. Kanuni hizi ni lazima zieleweke - wote wale wanaokusanya pesa ni lazima wazitumie pamoja na msimamo.

Ikiwa unasoma kitabu hiki kwa lengo la kutumia maarifa kinachotoa, jaribio la kwanza la msimamo wako litakuja wakati utakapoanza kufuata hatua sita zilizoelezwa katika sura ya pili. Ikiwa kama wewe siyo mmoja wa wawili kati ya kila watu mia ambao tayari wana “lengo kamili” ambalo unalenga na mpango kamili kwa ajili ya kulifikia, unaweza kusoma maelekezo na kisha kuendelea na ratiba yako ya kila siku, kamwe usifuate maelekezo hayo.

Mwandishi anakuangalia katika hatua hii kwasababu ukosefu wa msimamo ni moja ya sababu kubwa ya kuanguka. Zaidi uzoefu na maelfu ya watu umethibitisha kwamba ukosefu wa msimamo ni udhaifu uliozoeleka kwa watu wengi. Ni udhaifu unaoweza kurekebishwa kwa jitihada. Urahisi ambao ukosefu wa msimamo unaweza kuondolewa utategemea kwa kiasi kikubwa nguvu ya shauku ya mtu.

Mwanzo wa mafanikio yote ni shauku. Kumbuka hili daima akilini. Shauku dhaifu huleta matokeo dhaifu, kama ilivyokuwa tu kiasi kidogo cha moto kutengeneza kiasi kidogo cha joto. Ikiwa utajikuta mwenyewe ukiwa huna msimamo, udhaifu huu unaweza ukarekebishwa kwa kutengeneza moto mkubwa chini ya shauku zako.

Endelea kusoma mpaka mwisho, kisha rudi nyuma kwenye sura ya 2 na uanze mara moja kutekeleza maelezo yaliyotolewa katika hatua sita. Shauku ambayo umekuwa ukifuata haya maelekezo itaonyesha wazi ni kwa kiasi gani una shauku kweli ya kupata pesa. Ikiwa utakuta kwamba shauku yako ni kidogo, unaweza ukawa na uhakika kwamba, bado haujajijengea “ufahamu wa pesa” ambao ni lazima uwe nao kabla haujaweza kuwa na uhakika wa kujilimbikizia utajiri.

Utajiri huelekea kwa watu ambao akili zao zimejitayarisha ‘kuuvuta’, kweli kama vile maji yanavyoelekea baharini. Katika hiki kitabu kunaweza kupatikana vichocheo vyote muhimu vya kupatanisha akili yeyote ya kawaida na mitetemo ambayo itavuta shauku ya kitu mtu anachotamani. Ikiwa utajikuta dhaifu katika msimamo,weka umakini wako katika maelezo yaliyopo katika ukurasa wa 10 kuhusiana na Jitihada.

Jihusishe mwenyewe na Kundi la Kushauriana, na jenga msimamo kupitia juhudi za ushirikiano wa wanachama wa kundi hili. Utapata maelekezo ya ziada ya kujenga msimamo katika sura ya 4 juu ya Kujishauri  na sura ya 12 juu ya Akili ya ndani. Fuata maelekezo yaliyotolewa katika hizi Sura mpaka tabia yako ya asili ikabidhi kwa akili yako ya ndani picha halisi ya kitu unachotamani. Kutoka hatua hiyo na kuendelea, hautalemazwa tena na ukosefu wa msimamo.

Akili yako ya ndani hufanya kazi muda wote, wakati ukiwa macho na wakati ukiwa umelala . Juhudi za ghafla au za mara chache kuzitumia hizi kanuni  hazitakuwa na maana kwako. Ili kupata matokeo ni lazima uzitumie kanuni zote mpaka matumizi yake yanakuwa tabia iliyozoeleka kwako. Hakuna njia nyingine unayoweza kujenga ‘uelewa wa pesa’ unaohitajika.

Umasikini unavutwa kwa mtu ambaye akili yake inaendana nao, kama vile pesa inavyovutwa kwa mtu ambaye akili yake imekuwa ikijiandaa kwa makusudi kuivuta, na kwa kupitia kanuni hiyohiyo. UFAHAMU WA UMASIKINI KWA HIYARI UTAKAMATA AKILI AMBAYO HAIJAJAZWA NA UFAHAMU WA PESA.


 FUNGUA SEHEMU NA SURA ZOTE HAPA ZILIZOKWISHA WEKWA
     

0 Response to "UTAJIRI HUENDA KWA WALIOTAYARI KUTAJIRIKA KAMA MAJI YAENDAVYO BAHARINI"

Post a Comment