WAKATI MADENI KWAKO NI NUKSI, MATAJIRI NA WALIOFANIKIWA MAISHA HUYACHUKULIAJE? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WAKATI MADENI KWAKO NI NUKSI, MATAJIRI NA WALIOFANIKIWA MAISHA HUYACHUKULIAJE?

Kikundi cha mikopo midogomidogo (vicoba)
Karibu kila mtu wa kawaida utakayekutana naye, mkizungumzia kuhusiana na madeni utamsikia akilalamika juu ya ubaya wa madeni au mikopo inayokuwa mara nyingi ikihusishwa na kufilisiwa, umasikini na hata mikosi. Lakini kuna ukweli wowote kwamba deni ni adui mkubwa kiasi hicho?

SOMA: Jinsi 2020 unavyoweza kugeuza wazo lako la muda mrefu kuwa biashara halisi yenye mafanikio.


Ubaya au uzuri wa madeni unatokana na jinsi mtu anavyoyachukulia na dunia nzima kumekuwa na tabaka mbili za watu wanaoyachukulia madeni kwa namna mbili tofauti kabisa. Tabaka hizo mbili za watu ni;

1.   Watu waliofanikiwa kiuchumi/matajiri
2.   Watu wa kawaida/masikini.

Vile vile ubaya au uzuri wa madeni hutegemea ni aina gani ya deni, kuna aina mbili za madeni;

1.   Madeni mabaya na
2.   Madeni mazuri

Madeni mabaya ni yale madeni ambayo mkopaji huyatumia katika matumizi yake ya kawaida yasiyokuwa ya kibiashara. Unapokopa fedha na kwenda kuzitumia katika shughuli zisizozalisha faida, hayo ni madeni mabaya. Kwa upande mwingine madeni mazuri ni yale ambayo mkopaji huutumia mkopo kuzalisha faida na katu hawezi kukiuka kiholela matumizi ya mkopo anaochukua.

SOMA: Je, kukopa ili ukalipe deni la zamani kunawezaje kuboresha mzunguko wa fedha kwenye biashara yako? 


Watu wa kawaida, bila kujali tofauti hii iliyokuwepo katika aina hizi mbili za madeni, wao huyachukulia madeni yote yawe mabaya au mazuri kuwa ni kitu cha hatari sana kisichostahili kabisa mtu kuwa nacho. Wanapojikuta wameingia katika madeni kitu ambacho ni cha kawaida kabisa kwa mtu yeyote anayehangaika kujikwamua kiuchumi, hujawa na hofu kubwa na kuona kama hamna kabisa njia rahisi ya kujinasua. Watu wa namna hii aghalabu husikia hata wamejinyonga shauri ya madeni.............somo hili linaendelea... 


....................................................
Ungana na mimi leo Mei Mosi 2020 katika darasa letu la masomo ya fedha na semina za Michanganuo ya biashara,  nitafundisha somo hili kupitia njia ya Whatsapp, Channel yetu ya Telegram na Email. 

Masomo ni kila siku saa 3 mpaka saa 4 usiku. Unapewa offa ya vitabu, kifurushi cha michanganuo maarufu mitatu ya kuku, masomo yote ya zamani yaliyokwishapita, templates na vingine vingi. Ada ni  shilingi elfu 10 tu.


Namba za kulipia ni, 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo.


Kwa vitabu na Michanganuo mbalimbalia ya biashara tembelea Duka letu la mtandaoni la; SMART BOOKS TANZANIA

0 Response to "WAKATI MADENI KWAKO NI NUKSI, MATAJIRI NA WALIOFANIKIWA MAISHA HUYACHUKULIAJE?"

Post a Comment