Biashara ya
ardhi na majengo ni moja kati ya vyanzo vya utajiri vya uhakika zaidi duniani
lakini watu wengi wameishiwa kabisa hamu ya kufikiria kuanzisha biashara ya
kuwekeza kwenye ardhi na majengo kutokana na kukosa pesa za kutosha kufanya
hivyo na dhana potofu iliyojengeka kwamba biashara hii walio na uwezo nayo ni
matajiri tu wenye pesa zao. Watu hao hujiuliza hivi;
“Ikiwa
kama mimi sina hata shilingi mia mfukoni ya kuanzisha biashara ya kawaida,
sembuse niweze kuingia kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo unaohitaji
mamilioni ya pesa?”
Ukweli ni kwamba
ni rahisi sana mtu kutengeneza pesa ikiwa tayari unazo pesa na hii
ndiyo sababu kubwa ya matajiri wengi kuendelea kuwa matajiri wakati masikini
wakiendelea kudidimia katika umasikini mkubwa.
SOMO: Unajua
biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara mbili ya mtaji unaowekeza?
Hata hivyo
habari njema kwa watu wa namna hii ni kwamba zipo njia chache ambazo mtu
asiyekuwa na hata mia mfukoni anaweza kuzitumia mwishowe akaweza kutimiza ndoto
yake ya kumiliki biashara ya uwekezaji katika ardhi na majengo kwa muda mfupi sana.
Siri za
kufanikiwa katika kuwekeza kwenye ardhi na majengo (Real Estate Investing) haziegemei tu kwa wale waliokuwa na pesa
nyingi mfano kina Dangote, Donald Trump, Warren Buffet, Mo na Bakhresa hapana,
lakini pia ikumbukwe kuwa uwekezaji kwenye Real estate siyo miradi ya kuleta
utajiri wa haraka ndani ya usiku moja umeamka ukajikuta bilionea, inahitajika
subira na uvumilivu wa kutosha
SOMA: Tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote amekopa, wewe unangoja nini?
Katika kufafanua
jinsi ya kuwekeza kwenye biashara ya ardhi na majengo bila pesa nitazungumzia
njia kubwa 2 watu wengi huzitumia, lakini kabla sijaanza, tambua kuwa uwekezaji
katika ardhi na majengo ni miradi inayohitaji uwekezaji wa kiwango kikubwa cha
fedha kuliko biashara za kawaida na pia haijalishi una umri gani kuwa
mwekezaji, unaweza kuwa na umri wa miaka 15, 45 au hata 70 na kuendelea.
Ardhi na majengo
ni biashara nzuri ya kuwekeza mtu wa rika lolote lile ingawa inaonekana walio
na umri mkubwa ndio zaidi wanaojihusisha nayo pengine ktokana na sbabu kubwa
kwamba tayari wanakuwa wameshajilimbikizia mitaji ya kutosha ujanani. Hata
hivyo vijana na walio na umri mdogo wanaweza wakatumia mbinu na mikakati
itakayoainishwa katika somo hili kuweza kukivuka kihunzi hiki cha kukosa mtaji.
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado
Badilisha pia
msimamo wako ambao pengine umekuwa nao kwa muda mrefu kwamba huwezi kabisa
kuwekeza kwenye biashara ya ardhi na majengo bila ya kuwa hata na mia mfukoni.
Na badala yake jiulize, ni rasilimali zipi nyingine unazoweza ukazitumia
kutimiza ndoto yako hiyo ya kuwa mwekezaji wa ardhi na majengo.
Serikali kupitia
Wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara katika dira ya biashara tayari
imekwishaweka mazingira mazuri kwa kila mtu kwenye sekta binafsi anayefikiria
kuanzisha biashara yeyote ile Tanzania, hivyo ni uamuzi wa mtu mwenyewe kunyoa
au kusuka. Utajiri maana yake ni kumiliki vitegauchumi na biashara na wala siyo
kumiliki pesa kama wengi wanavyodhani kimakosa.
Kitu cha kwanza
kabisa na muhimu kuliko vyote ni kuweka malengo, mwisho ni lazima utambue
kwamba pesa taslimu peke yake ni sawa na chombo tu ambacho mtu anaweza
kukitumia kupata mali anazohitaji haraka, hata hivyo pesa siyo chombo pekee
duniani kinachoweza kufanya kazi ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo, kuna
vyombo vingine mbadala.
Sasa hapo ndipo
ninapotaka ufahamu hivyo vyombo vingine zaidi ya pesa ni vipi katika kujibu
swali letu, “Nitawekezaje kwenye ardhi na
majengo wakati sina hata mia mfukoni?”
Kwani uwekezaji
maana yake ni nini? Kuna uwekezaji wa aina nyini, wapo wanaoamua kufanya
uwekezaji mtandaoni, kuwekeza kwenye hisa, kuwekeza kwenye ardhi na majengo,
kuwekeza kwenye biashara za kawaida za uchuuzi nk. mifano ipo mingi lakini kwa
ujumla uwekezaji ni kitendo cha kuweka pesa zako kwenye miradi ya kiuchumi kwa
lengo la kuja kupata faida hapo baadae. Kuwekeza ndiyo njia bora zaidi ya
kufanikiwa kuwa tajiri iliyokuwa halali na uwekezaji kwenye ardhi na majengo ni
njia salama na ya uhakika zaidio kuwekeza muda na rasilimali zako.
Tambua pia kuwa
hakuna uwekezaji mdogo ikiwa maono yako ni makubwa, mfano kuna walioamua
kuwekeza kwenye kilimo na kupata mikopo ya kilimo kwa urahisi sana lakini kumbe
maono yao makubwa kichwani yalikuwa ni kuja kuwekeza kwenye biashara kubwakubwa
za majengo na ardhi.
Huu ni mfano mdogo
tu nimekumegea, kuna mbinu nyingi watu kote duniani huzitumia ukiwaona
unawadharau lakini mwishowe unakuja kuwakuta ni mabilionea wa kutupa kama
walivyo kina Trump na Warren Buffet, fuatilia somo hili hadi mwisho kuzifahamu
mbinu hizo zote.
Ikiwa basi kama
huna hata mia mfukoni,.....................................
...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................
.....................................................somo litaendelea usiku leo tarehe 18/07/2023 saa 3 kwenye
mastermindgroup la Michanganuo.
Mtu yeyote anaweza akajiunga na group hili
kwa kulipa ada ya mwaka mzima sh. Elfu 10 tu, kupitia namba zetu,
0712202244 au 0765553030 jina ni Peter
Augustino Tarimo, na kisha kutuma ujumbe kwa sms au watsap usemao;
“NIUNGE GROUP LA MASOMO NA OFFA INAYOKARIBIA KUISHA MUDA WAKE”
Muda huohuo nitakutumia vitu vifuatavyo;
1.
OFFA yetu ya vitu 12 inayokaribia
kumalizika
2.
Masomo yote ya fedha
tuliyojifunza kwenye group tangu limeanza (compilation)
3.
Kukuunganisha na Group la masomo
na semia ikiwa unataka (wengine huwa
hawapendi magroup)
OFFA yetu ya vitu 12 inajumuisha vitabu na michanganuo ifuatayo;
1.
COURSE/SEMINA: (compiled
complete course) ya Jinsi ya
kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa
kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili
2.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
5.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili
6.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani na ndio
hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
7.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers - kwa
kiswahili
8.
MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza
9.
MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za
saruji- kwa
kiswahili
10. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili
11. MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
13. Kuunganishwa Group la
masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka
hatukuunganishi)
Imeandaliwa na:
Peter A. Tarimo
0712202244
0765553030
Kujipatia vitabu vyetu au Michanganuo mbalimbali ya biashara tembelea duka letu
la mtandaoni hapa la SMART
BOOKS TZ
Kupata toleo jipya 2023 la kitabu cha MAFANIKIO
YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA bofya hayo maandishi.
Kuona
kwa kifupi baadhi ya kazi tulizowafanyia wadau wetu bovya hapa>>OUR PORTFOLIO
0 Response to "JINSI YA KUANZISHA BIASHARA YA UWEKEZAJI KWENYE ARDHI NA MAJENGO HATA KAMA HUNA MIA MFUKONI"
Post a Comment