Mwanasayansi mkubwa duniani Stephen Hawking wa Uingereza
aliyefariki jana, kifo chake kimetokea miaka 55 baada ya madaktari kumwambia
kwamba alikuwa na miaka 2 na nusu tu ya kuishi kutokana na kugundulika kuwa na
ugojwa wa mishipa ya fahamu kupungua uwezo wa kusapoti misuli. Ugonjwa huu unawapata
watu kwa nadra sana na unajulikana kitaalamu kama, amyotrophic lateral sclerosis (ALS)
Akiwa na umri wa miaka 21 tu, huku ukiwa
ni mwaka wake wa kwanza akisomea PHD katika chuo kikuu cha Cambridge ndipo
alipolazwa hospitalini kwa uchunguzi wa ugojwa huo, kwa hakika zilikuwa ni
habari za kushitua sana kwake na kwa familia yake. Hata hivyo kuna vitu kadhaa
vilivyomfanya asikate tamaa moja kwa moja licha ya habari hiyo ya kuogofya.
Kitu cha kwanza kabisa kilichomfanya awe
na matumaini ni pale pale akiwa amelazwa hospitalini, kulikuwa na kijana
mwingine aliyekuwa amelazwa naye chumba kimoja kwa tatizo tofauti la ugojwa wa leukemia.
Akilinganisha ukubwa wa tatizo la kijana yule mwezie alilokuwa akikabiliana
nalo na la kwake, Stephen Hawking baadae aliliona tatizo lake kuwa na nafuu
zaidi na linaloweza kuvumilika zaidi ya hilo la mwenzake la leukemia. Leukemia
ni ugojwa wa kansa ya damu ambao mgojwa hawezi kudumu nao kwa muda mrefu.
Muda mfupi baada ya Stephen kuruhusiwa
kutoka hospitali, aliwaza kichwani na kujifananisha na mtu aliyekuwa akisubiri
hukumu ya kifo, lakini mawazo yake hayo yalimfanya kutambua kwamba bado
kulikuwa nafasi japo kidogo katika maisha yake yaliyosalia ya kufanya mambo ya
maana hata ikiwa I machache kiasi gani. Huku akitambua wazi kwamba amesaliwa tu
na miaka michache ya kuishi pengine masikini hata kutokutosha mpaka asheherekee
PHD yake, aliamua kusoma kufa na kupona angalao atomize ndoto yake aliyoota
akiwa pale hospitalini ya kufanya vyema mambo machache yaliyobakia katika muda
mfupi wa kuishi hapa duniani.
Ugonjwa ulimbadililisha kuwa
mwanasayansi mkubwa kama yeye mwenyewe alivyowahi kusimulia hivi,
“Kabla sijagundulika na ugonjwa huu, sikuwa kabisa na malengo
na masomo, nilikuwa nimechoshwa sana na maisha, sikuwa naona chcochcote kile
cha maana cha kufanya, lakini pindi tu baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa na
nisingeliweza kuishi hadi nimalize chuo nikaanza kuzingatia masomo”-Stephen Hawking
Sababu hii ndiyo iliyokuja kumfanya
Hawking kuwa mwanasayanzi mashuhuri kiasi hiki. Alijitupa katika tafiti na kazi
mbalimbali mbali za kisayansi hususani kuhusiana na anga za mbali na kwa kadiri
mafanikioa yake katika tasnia hiyo yalivyozidi kuwa makubwa ndivyo na afya yake
ya kimwili nayo ilivyozidi kuzorota. Lakini jambo la ajabu katika ugonjwa huu
ni kwamba akili hubakia kama ilivyo, huwa haiathiriwi kabisa na ugonjwa huu wa (ALS).
Ilifikia kipindi akawa kila kitu kimwili
ni lazima asaidiwe huku akitumia kiti cha magurudumu mawili. Sauti nayo
ikakatika kabisa lakini kwa msaada wa wataalamu wa kompyuta kutoka Marekani
wakaweza kumtengenezea program(speech
synthesizer) inayoweza kutafsiri hisia za mtu na
kutamka maneno anayotaka kusema ambayo ilikuja kumsaidia hata alipokuwa akitoa
mihadhara mbalimbali katika vyuo vikuu duniani mpaka anakufa.
Akitumia programu hiyo na msaidizi aliweza
kuandika ripoti mbalimbali za kisayansi na zisizokuwa za kisayansi, vitabu na
hata amewahi pia kujihusisha katika filamu na vipindi vya televisheni hadi
mauti inamfika jana.
Mtu huyu ni ushahidi wa wazi kwetu sisi wajasiriamali
kwamba akili ya binadamu inao uwezo wa ajabu wa kutenda mambo bila hata ya
kutegemea mwili wake(Think & Grow Rich). Aliweza
kufanya mambo makubwa yanayolingana na mambo waliyowahi kufanya kina Albert
Einstain, Sir Izak Newton, Galileo Galilei na wengineo huku mwili na viungo
vyake vikiwa havifanyi kazi yeyote isipokuwa akili yake pekee. Hayo ndiyo
maajabu ya UBONGO wa binadamu.
Akifungua mashindano ya paralympic mwaka 2012 huko London
baada ya kukaribishwa na watu kumshangilia mno kwa makofi alitamka maneno
yafuatayo;
“Sisi sote tuko tofauti, hakuna kitu kama
binadamu wanaofanana au wa aina moja, lakini tunachangia wote kuwa na roho.
Kitu muhimu ni kwamba tuna uwezo wa kubuni. Ubunifu huu unaweza kuchukua sura
nyingi, kuanzia mafanikio yanayoshikika mpaka fizikia ya nadharia. Hata maisha
yawe magumu kiasi gani, mara zote kuna kitu mtu unachoweza kufanikisha.” ”-Stephen
Hawking
0 Response to "UMEKATA TAMAA YA MAISHA? HEBU SOMA MAAJABU YA MWANASAYANSI HUYU MKUBWA DUNIANI."
Post a Comment