Kama mtu atakuuliza ni kitu gani ambacho ungependa
ukibadilishe katika maisha yako halafu pesa zisiwe tena tatizo kwako ungetaja
kitu gani? Bila shaka ungeweza kumtajia kitu chochote kile hata kama ingelikuwa
ni kula mmlo mmoja tu kila siku kwa miezi kadhaa.
Binadamu sisi sote ndoto zetu, tungependa kuishi maisha
mazuri, kumiliki vitu vizuri, kama nyunba, magari ya kisasa, simu ya bei kubwa
nk. lakini bado wengi wetu tunaishi maisha yenye mzunguko hafifu wa fedha na
vikwazo lukuki katika masuala yote yahusuyo fedha, na tunaathiriwa kwa kiasi
kikubwa hata na zile gharama za msingi kabisa za maisha kama vile, kodi za
nyumba, chakula na ada za watoto za shule.
Ingekuwaje kama kuna tabia moja katika maisha yetu ambayo
tukiibadilisha mambo yanaweza kunyooka? Na
je, ungekubali kubadilisha tabia hiyo? Wala jambo hilo halipaswi kuwa kubwa au
gumu sana kulitekeleza. Mara nyingi huwa tunajiwekea malengo ambayo hatimaye
tunashindwa kuyatekeleza kama tulivyodhamiria. Lakini vipi kama tunaweza
kubadilika sasa na kuamua kuwa tofauti?
Katika mambo 11 yaliyotajwa, hebu amua leo
kubadilisha moja tu, siyo yote ingawa huzuiwi kuyazingatia yote ikiwa utaweza. Huo
unaweza ukawa ndio mwanzo wa kubadilisha kabisa uhusiano wako na fedha, kuwa
mzuri zaidi kama ulikuwa mbaya.
........................................................................
Ndugu msomaji somo hili tunakwenda kujifunza leo jumapili usiku katika Group la Whatsap na email la MICHANGANUO ONLINE, Tutakuwa pia na sehemu ya pili ya sura ya 9 ya tafsiri ya kile kitabu cha THINK & GROW RICH(FIKIRI UTAJIRIKE)
Kujiunga na Group hili kiingilio ni shilingi elfu 10 na unakuwa mwanachama wa kudumu siku zote. Tunatoa pia masomo mbalimbali yote yaliyokwishapita kwenye group pamoja na vitabu na makala mbalimbali zenye mafunzo. Namba za kulipia ni 0712202244 au 0765553030 ukishalipa tuma ujumbe wa simu au whatsapp 0765553030
Mbona hua humalizii Hizi makala au
ReplyDeleteHellow Unknown, Kuna baadhi ya makala huwa simalizii kwa sababu zinakuwa ni maalumu kwa ajili ya group la wale wanaohitaji kujifunza zaidi. Sababu ya kuziweka hapa nusu ni kwamba msomaji yule anayependa kujifunza zaidi aweze tu kupata utangulizi wa makala na kisha makala kamili anajiunga na kundi hilo kwa kiingilio kidogo sana cha shilini elfu 10 tu kwa mwaka mzima anapata na vitabu na michanganuo ya zawadi(offa)
DeleteAidha kuna makala nyingine nyingi ndani ya blogu ambazo huwa zinabakia kuwa kamili bila ya kuzipunguza kitu chochote, na mtu yeyote anaweza akazisoma free of charge kabisa pasipo kulipia chochote zaidi ya muda wake mwenyewe.
Asante sana
peter Tarimo