Binafsi napenda kuzungumzia vitu kutokana na uzoefu wangu mwenyewe na hasa katika mambo ninayoandika katika blogu hii ya jifunzeujasiriamali. Katika kampeni tunazoanzisha hapa, tangu mwaka jana nimekuwa nikitoa taarifa zake kwa wale wanaofuatilia hatua kwa hatua kwa kadiri mimi mwenyewe ninavyotekeleza kampeni hizo kwa upande wangu huku nikiwasihi pia wasomaji nao kupima mwenendo wa uteelezaji kwa upande wao.
Siyo lazima kila mmoja alingane na mwenzake katika
kiwango cha utimizaji wa malengo lakini angalao kila mtu anapaswa kujitathmini
ikiwa anapiga hatua ama la. Siku chache kabla sijatoa makala ya mwisho katika
blogu hii niliandika makala ya kuwakumbusha wadau wote wa blogu hii kwamba, Ni
robo ya mwaka sasa, je malengo yao waliyojiwekea Januari yalikuwa katika mstari
sahihi kama walivyokusudia au walikuwa tayari wameshayaacha na kushika mambo
mengine tofauti?
SOMA: Salamu zangu 2018 kukutakia heri na mafanikio ya kweli.
SOMA: Salamu zangu 2018 kukutakia heri na mafanikio ya kweli.
Nakiri kweli kwamba baada ya hapo, ghafla sikuonekana
tena katika blogu wala mitandao mingine ya kijamii niliyokuwa nimezoea
kuonekana kila mara kinyume kabisa na malengo yangu niliyokuwa nimejiwekea
Januari. Kwa waliokuwa wamesoma ujumbe wangu huo wa mwisho bila shaka
walistaajabu kuona “Mhubiri anashindwa kuyaishi yale
anayohubiri”, “Kama anayoandika ni ya kweli mbona sasa yeye hayatimizi, ona sasa
tulimwambia mipango siyo matumizi, anakataa, ”
Dhamira yangu kuu mimi na blogu hii kwa ujumla mwaka huu
ilikuwa ni kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya Mzunguko chanya wa fedha ndiyonjia bora zaidi ya kutimiza malengo yako mwaka 2018, na moja kati ya
malengo madogomadogo tuliyojiwekea ni kuhakikisha kila mwezi tunajadili
mchanganuo mmoja bunifu ndani ya group la wasap la MICHANGANUO ONLINE pamoja na mada mbalimbali kuhusiana na mzunguko
wa fedha katika biashara zetu na mifukoni pia kila siku.
Ukiniuliza vipi malengo hayo kama ninayatimiza nitakujibu
ndiyo, japo siwezi kukuambia kama nayatimiza kwa asilimia mia moja. Na hii iko
hivyo kila mahali duniani, kila taasisi na kila mtu, hata serikali zenyewe
haziwezi zikatimiza malengo au mipango zinayojiwekea “exactly” kama zilivyoipanga. Kwa mfano mimi mwenyewe binafsi
majuzi katika kampeni yetu hii niliugua kiasi sikuweza kutimiza ipasavyo
majukumu yangu yote ya kila siku na hio likasababisha na shughuli zangu kwenye
mitandao ya kijamii kusita kwa muda pia.
SOMA: Punde kabla hujakata tamaa ya maisha hebu soma hapa kwanza.
SOMA: Punde kabla hujakata tamaa ya maisha hebu soma hapa kwanza.
Huwezi kuandika wala kufikiria vizuri ili hali unaumwa na
kama ujuavyo shughuli zinazohusiana na maudhui kukasimu kwa mtu ghafla ni
vigumu kama hukuwa umefanya maandalizi ya kutosha, hata hivyo nashukuru kwenye
group letu la MICHANGANUO ONLINE bado kuna wadau ambao tayari walikuwa
wameshaanza kutoa michango yao kuhusiana na mada mbalimbali hasa ya ufugaji wa
kuku kwa kweli nawashukuru walikuwa wanafanya kazi kubwa kuendelea kuchangamsha
group lisisinzie.
Hili linanikumbusha siyo mimi tu na hata wewe pia kama ulikuwa hujafahamu umuhimu wa kufanya kazi kama timu, basi ujue umuhimu huo upo na ni mkubwa hasa ikiwa utataka kutengeneza mfumo ambao haukutegemei wewe kama wewe kuwepo pale eneo la tukio moja kwa moja ndipo mambo yaweze kwenda.
SOMA: Jifunze nguvu ya ushirika(mastermind group)
Hili linanikumbusha siyo mimi tu na hata wewe pia kama ulikuwa hujafahamu umuhimu wa kufanya kazi kama timu, basi ujue umuhimu huo upo na ni mkubwa hasa ikiwa utataka kutengeneza mfumo ambao haukutegemei wewe kama wewe kuwepo pale eneo la tukio moja kwa moja ndipo mambo yaweze kwenda.
SOMA: Jifunze nguvu ya ushirika(mastermind group)
Binadamu tunaweka mipango, tunapanga malengo na hivyo
ndivyo tumekuwa tukifanya karibu katika kila jambo tulifanyalo, jana nimemsikia
mdhibiti mkuuu wa hesabu za serikali Profesa Musa Assad akizungumzia bungeni
jinsi ambavyo wanafanya kazi kubwa kuhakikisha mipango inayopangwa na Bunge la
Jamhuri ya Muungano inatimizwa na
serikali, alitaja baadhi ya maeneo ambayo wahusika hawakuweza hata kutimiza
mipango iliyowekwa kwa asilimia 50%.
Ni kweli inawezekana kunakuwa na uzembe mahala pengine
lakini kwingine ni sababu tu ambazo zisingeliweza kuzuilika. Nimemsikia pia
Raisi msaafu wa awamu ya nne Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho kikwete wakati akiwa
na mwenzake Rais wa sasa Mh. Dokta John Pombe Magufuli wakati wa ufunguzi wa
Taasisi yake ya Jakaya Kikwete Foundation.
Kikwete katika malengo ya taasisi yake nadhani ni manne
aliyoyataja kuwa ni Afya hasa mama na mtoto, Kilimo vijana na kina mama, Mabadiliko
ya hali ya nchi na Utawala bora alitamka bayana kwamba haiwezekani kutimiza
kila lengo kwa wakati mmoja, na watakachokifanya ni kutimiza kidogokidogo
wakianza kwanza na lengo la Afya ya mama na mtoto. Hapa Kikwete anaonyesha ni
kwa jinsi gani kutekeleza mipango kunahitaji subira na malengo.
Ninachotaka kusema hapa tu ni kwamba, juu ya yote ingawa
mipango tunayojiwekea maishani tunaweza tusiweze kuitekeleza kama tulivyojipangia
lakini mipango kamwe haiwezi kuepukika katika shughuli zetu za kila siku hapa
duniani. Ninaposema mipango namaanisha malengo, ni kitu kile kile hata ikiwa
kuna tofauti kidogo.
Angalia ni sababu zipi zinazokwamisha usiweze kutekeleza
mipango yako, je unaweza ukazirekebisha mara moja na kuendelea kusonga mbele?
Vipi kama ni ugonjwa, umepona? Kama ni uzembe tu, umerekebisha haraka?. Baada
ya kurekebisha kile kilichokukwamisha kwa muda kutekeleza mipango yako sasa ni
wakati wa kuendeleza mapambano mpaka umefikia mwisho.
Kampeni yetu ya Mzunguko
chanya wa fedha ndiyo njia bora ya kutimiza malengo mwaka 2018 ipo palepale
na wala haijatetereka licha ya misukosuko ya hapa na pale, Leo tunaendelea na
somo letu la “NAANDIKA HATUA KWA HATUA MCHANGANUO WA BIASHARA YA UFUGAJI WA
KUKU WA NYAMA sehemu ya 4” ambayo tutaangalia hesabu au mpango wa fedha kwa
undani kabisa.
SOMA: Naanza hatua kwa hatua kuandika mchanganuo wangu wa biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama(BROILERS)
SOMA: Naanza hatua kwa hatua kuandika mchanganuo wangu wa biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama(BROILERS)
Michanganuo hii tunayoijadili katika hili group la
watsapp ni ya kipekee, pamoja na kwamba unaweza ukaona ni ya kawaida tu kwa
kuitaja lakini ndani yake ina ubunifu mkubwa wenye lengo la kumfanya anayeisoma
kujijengea mawazo ya kijasiriamali yatakayomwezesha kuendesha biashara yake kwa
ufanisi mkubwa zaidi na hivyo kusababisha mzunguko wake wa fedha kuwa chanya
muda wote.
Ikiwa hutumii watsapp siyo tatizo kwani masomo haya yote
pia huwa tunayatuma yote kwa njia ya email pamoja na kuyaweka katika blogu
maalumu inayoweza kufikiwa na mtu aliyejiunga na GROUP hilo tu.
KARIBU SANA KWENYE GROUP LA MICHANGANUO ONLINE
WHATSAPP: 0765553030
SIMU: 0712202244
0 Response to "INGAWA MIPANGO SI MATUMIZI LAKINI HAIEPUKIKI KWENYE MAISHA NA BIASHARA"
Post a Comment