Mafanikio katika jambo lolote lile maishani
mwanadamu analolenga kufanya hutokea nje ya uwanja wake wa faraja, kwa kimombo
wanasema, “outside of your comfort zone”,.
Unataka kuwahi kazini, shuleni au kwenye biashara zako kwa lengo la kuzidisha
mafanikio, ufanisi au kipato zaidi, ni lazima ukubaliane na kuachia shuka,
kukatisha usingizi wako mtamu wa alfajiri na kupambana na umande wa
asubuhiasubuhi kwenye nyasi katika uchochoro unaotoka nyumbani kwako kabla
hujafika stendi kupanda basi.
Unataka mwili wako kuwa imara(fiti), ni
lazima kwanza uvuje jasho jingi kwa mazoezi nk. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa
katika biashara au sekta nyingine zozote zile za kimaisha. Mafanikio yanamtaka
mtu kuchukua hatua ambazo mara nyingi haziwezi kumpendeza hata kidogo, na hali
hiyo ya kutokupendezwa ndiyo tunayopigana nayo kila siku ndani ya fikra zetu, na ili tufanikiwe basi ni
lazima tushinde vita hiyo ya kifikra kabla hatujaanza kusaka njia kuu za
mafanikio katika maisha.
Binadamu mara nyingi tumekuwa tukisaka siri
za mafanikio katika mambo yetu mbalimbali tunayoyafanya kama vile, jinsi ya
kufanikiwa kibiashara, jinsi ya kupata pesa, kufanikiwa katika masomo, au
katika maeneo mengine yeyote yale kwenye maisha. Ukweli ni kwamba majibu ya
swali hilo wala siyo magumu hata kidogo kwani siri kuu za mafanikio
hujidhihirisha zenyewe katika mifano ya vitu, watu na hata mambo mbalimbali
yanayotokea kwenye mazingira yetu ya kawaida kabisa. Mifano hiyo katika maisha
ya kawaida ndiyo leo nataka nikutajie katika makala hii, hivyo karibu sana
tujifunze pamoja, hakikisha unaisoma makala hii mpaka mwisho kupata manufaa
yote yaliyokusudiwa na ukiwa na maoni au mchango wowote ule wa mawazo usisite
kuandika mwisho kwenye sehemu ya maoni, nitumie email, jifunzeujasiriamali@gmail.com.
Au ujumbe wa whatsapp kwenye 0765553030
1. SHULENI.
Unafikiri ni kwanini serikali duniani
ziliweka mifumo ya elimu ambayo kila mtu ni lazima kwanza aipitie kabla
hajafanya mtihani wake wa mwisho? Lengo la mtu kwenda shuleni/chuo ni ili aweze
kupata elimu na hatimaye baada ya ule muda uliopangwa na serikali kama ni miaka
saba, minne au miwili kumalizika basi aweze kufanya mtihani na kufaulu.
Serikali inafahamu kabisa kwamba muda uliopangwa mwanafunzi endapo atatia
juhudi zake kwenye masomo ni lazima tu atafaulu. Kwa hiyo imeweka mfumo maalumu
ili kila anayeutumia aweze kufaulu.
Mfumo huo serikali iliyouweka utakuta ndio
kama vile, mitaala mbalimbali(syllabus), ratiba za vipindi madarasani, likizo,
ukaguzi, mitihani ya wilaya, Mkoa na ile ya Kitaifa pamoja na mfumo mzima wa
uongozi katika shule zenyewe na Wizara husika kwa ujumla. Ni vigumu mno kwa
mwanafunzi au mtu yeyote yule kufanya mtihani akaweza kufaulu pasipo kuufuata
mfumo uliowekwa kama inavyotakiwa.
Kama ilivyokuwa vigumu kwa mwanafunzi wa
darasa la kwanza kufanya mtihani wa darasa la saba akafaulu, hali ni hivyohivyo
ilivyo pia katika upande wa maisha ya mtu ya kawaida anapokuwa na malengo
kwenye jambo fulani liwe biashara, kazi au shughuli yeyote ile ya kiuchumi.
Haiwezekani kabisa mtu eti leo umejiwekea malengo katika jambo fulani halafu
kesho tu au keshokutwa unataka malengo hayo yawe yametimia.
Hii ni sababu kubwa sana inayotufanya kila
siku tulalamike kwamba, kujiwekea malengo ni sawa na kupoteza muda, sasa bila
malengo utaendeshaje maisha yako? Hata roboti ili liweze kutimiza wajibu wake
ni lazima lipangiwe malengo na mmiliki wake katika mfumo wa kielektroniki au
kompyuta, yale ni malengo!
Tatizo hapa ni je, UNATUMIA MFUMO GANI KUTIMIZA MALENGO YAKO? Huwezi ukasema utaamka
tu ufanye chochote kitakachotokea mbele yako. Vinginevyo basi serikali
zingetangaza kwamba hakuna haja ya mifumo ya kielimu badala yake siku ya
mtihani mtu yeyote anaweza ‘from no where’ tu akafika shuleni/chuoni na kuja
kujifanyia zake mtihani wa mwisho hata ikiwa wakati wa maandalizi yeye alikuwa
akilea mtoto au akiuza karanga mtaani(kumradhi
sana msomaji sina dhamira mbaya ya kunyanyapaa makundi tajwa).
Malengo yanahitaji kuwekewa mfumo thabiti wa
kuyatekeleza sawasawa tu na serikali zinavyoweka mifumo ya elimu kusudi
wanafunzi waweze kutimiza malengo yao ya kielimu. Umefungua biashara yako, weka
mfumo wa kupata wateja kama kutangaza kwenye social media, magazeti nk., Weka
mfumo wa kuuza kwa kufungua matawi(outlets) sehemu mbalimbai na usikimbillie tu
kumtafuta mchawi anayekuloga au chumaulete usiyeweza kuelezea anakuibiaibiaje
hela zako, inawezekana chumaulete ni wewe mwenyewe, vile tu huna mfumo wa
kubaini kama ni wewe. Mfumo sahihi ungeweza kuwa ni kuweka daftari la mahesabu
kujua kila senti inakokwenda na inakotoka ni wapi.
2. MWANZI
WA KICHINA
(CHINESSE
BAMBOO TREE)
Hii ni stori ya kusisimua mno katika
ulimwengu wa kusaka mafanikio yenye ujumbe na funzo kubwa sana kwa watu wa
makabila yote duniani, siyo kwa wachina tu peke yake. Mti huu, Mwanzi wa
Kichina au Chinesse Bamboo tree kama unavyojulikana kote duniani ni kielelezo
kizuri sana cha jinsi mafanikio ya binadamu yalivyokuwa ni jambo linalohitaji
uvumilivu, subira na msimamo.
Mti huu kama ilivyokuwa miti mingine yote
duniani mara unapopandwa ardhini humea na kuota. Katika mwaka wake wote wa
kwanza huwezi ukaona mabadiliko yeyote yale ya maana kwani huota taratibu sana.
Mwaka wa pili mti huu wa mwanzi napo bado huonekana ukisuasua tu ardhini bila
kuonyesha maendeleo yeyote yale ya kutia moyo na hata mwaka wake wa tatu na wanne
pia bado kamti haka kanaoonekana ni kadogo tu.
Mwishowe sasa mti huu unapofikisha mwaka wake
wa tano (5)- maajabu makubwa hujitokeza. Ghafla mti huanza kuota kwa kasi ya
ajabu! Mwanzi wa Kichina sasa huota futi 80 kwenda juu katika kipindi cha wiki
sita (6) tu
Sasa hebu pata somo hapo, hivi Mwanzi huu wa
Kichina ni kweli huota futi hizo 80 zote katika kipindi hicho cha wiki 6 tu? Au
miaka minne ulikuwa ukijiotea ndani kwa ndani? Bila shaka na hicho ndicho
kilichokuwa kikifanyika. Mwanzi wa Kichina kwa miaka yote 4 hujitengenezea mifumo
imara ambayo ni mizizi, majani, shina, na hata seli na tishu mbalimbali, mifumo
ambayo hatimaye hutengeneza fursa kubwa ya baadae kuja kuota ghafla na
kuishangaza dunia. Mti huu usingelikuwa umetumia muda mrefu wa kutosha
kutengeneza misingi imara(mfumo), tusingeliweza pia kuja kuyaona matunda
unaokuja kuonyesha baada ya miaka 5 kupita.
Kanuni ya mti huu hufanya kazi pia kwetu sisi
binadamu sawasawa tu na inavyofanya kazi kwa mwanzi huu wa Kichina. Yeyote yule
anayeweka uvumilivu mkubwa na subira huku akitekeleza kwa vitendo ndoto na
malengo yake kidogokidogo kila siku na kukabiliana na changamoto bila ya kukata
tamaa kirahisi, anajijengea msingi imara(mfumo) ambao hatimaye kuna siku dunia
huja kushangaa mithili inavyofanya kwa Mwanzi huu wa Kichina.
Hakumna mafanikio rahisi, Siri ya mafanikio
kimaisha ni kwamba, chochote kile tufanyacho huenda taratibu mwanzoni jambo
linaloweza kutuchanganya na kutupa wakati mgumu sana. Lakini yote hayo mwishowe
huja kuzaa matunda. Napoleo Hill katika kitabu chake, THINK & GROW RICH
anasisitiza kwenye Sura ya 9 ya kitabu hicho kwamba, Kwa uvumilivu na msimamo usioyumbishwa kirahisi na kitu chochote kile,
mafanikio ni dhahiri.
Kuwa na malengo na kuendelea kuamini katika
kile unachokifanya hata kama huoni matokeo ya haraka.
3.
WANAMUZIKI KAMA KINA DIAMOND, ALI KIBA NA WENGINEO.
Tunavutiwa sana na mafanikio ya wanamuziki au
wasanii wakubwa kama kina Naseeb Abdul au Diamond, Ali Kiba na wengineo lakini
unaijua siri iliyoko nyuma ya mafanikio yao makubwa? Ni MSIMAMO, Napoleo hili
katika kitabu Think and Grow Rich au Fikiri Utajirike kwa Kiswahili anataja katika sura ya 9 kwamba mfano mzuri kabisa wa
nguvu ya msimamo ni biashara ya burudani, anasema kwa mfano watu kutoka pande
mbalimbali za dunia humiminika Hollywood Marekani kusaka umaarufu, mapenzi,
nguvu na kila aina ya mafanikio lakini kinachomfanya mtu aweze kupenya na
kufanikiwa kuingia pale ni msimamo wake wa kuendelea kupambana bila kuchoka.
Vipi kama Diamond baada ya kukitoa kibao
chake cha Tatizo kwetu Mbagala kama angeliridhika na mafanikio yaleyale halafu akabweteka na kukaa kimya bila
kutoa mfululizo vibao vingine vikali kama vile Nenda kamwambie.., You are My
number one, Wakawaka na nyinginezo? Msimamo wake wa kuendelea kufanya kazi
nzuri hata baada ya kupata mafanikio kidogo ulimfanya kuja kuwa star, nyota
mkubwa kote nchini Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla. Katika kutimiza
malengo yako hakikisha yale matendo mazuri unayoyafanya basi unayarudiarudia
kila mara.
Kufanya tendo moja tu zuri mara moja na kuona
tayari umewini hakutoshi,wala hakuna atakayeguswa na kitendo chako hicho
kimoja. Ukitaka kuvuta hisia za watu wengi ni lazima kwanza uonyeshe msimamo,
urudie mambo mazuri kila siku yaonekane ndipo ushindi utakuja. Umefungua
biashara yako leo na unataka uanze kuona mauzo makubwa siku hiyohiyo,
haiwezekani, ni lazima kwanza uuze elfu 5, elfu 10 na hata elfu 50 kisha itakuja
kufika siku unashangaa unauza laki tano mpaka milioni na kuendelea. Hiyo ndiyo
siri ya utajiri au jinsi ya kupata pesa, siri ya mafanikio katika biashara yeyote ile ni uvumilivu.
4. MICHEZO
YA BAHATI NA SIBU
Makampuni yanayoendesha michezo ya
kubahatisha hutangaza zawadi nono kwa washindi wanaofanikia kupita lakini, je
unafahamu fedha hizo hutolewa na nani? Mchezo wa bahati na sibu wanaoshiriki
huwa wengi na kile kiasi cha fedha wanazotoa ni kidogokidogo lakini kutokana na
wingi wao jumla yake hufika mamilioni ya shilingi na hizi ndizo fedha
zinazotumiwa na makampuni hayo kulipa washindi na wao kupata faida.
Wale wanaocheza huona kama vile hawapotezi
kitu chochote kutokana na sababu kwamba wengi wao hutumia fedha za ziada ambazo
hazipo katikika bajeti zao baada ya kutoa matumizi yao yote ya msingi ingawa
pia kuna baadhi ya watu wachache ambao wamefanya michezo hiyo kimakosa kama
ndio kazi zao. Lakini ni kitu gani kinachotokea baada ya maelfu ya watu
kucheza? Fedha kidogokidogo wanazozichanga huwawezesha washindi wachache
kugeuka mamilionea ghafla huku na makampuni husika pia yakineemeka.
Mfano huu wa michezo ya bahati na sibu funzo
lake ni kwamba mambo makubwa yote maishani hutokana na vitu vidogovidogo sana
kama fedha hizi kidogo wanazocheza watu bahati na sibu. Ili kutimiza lengo
kubwa ni lazima lengo hilo ulivunjevunje katika malengo madogomadogo kwanza na unapokuwa ukiyatimiza hayo malengo madogomadogo
ndiyo unatimiza lile lengo lako kubwa.
…………………………………………………..
Mpendwa msomaji wa blogu hii, na huo ndio
mwisho wa makala hii ya leo. Endelea kufuatilia makala zijazo na ikiwa utapenda
kupata mafunzo ya kina zaidi ya biashara na ujasiriamali, napendekeza kujiunga
na huduma zetu nyinginezo zifuatazo;
1. GROUP LA MICHANGANUO ONLINE
Ada ni sh. Elfu 10 na unapata fursa ya
kujiunga na group pamoja na masomo, vitabu na semina mbalimbali
zilizokwishatayarishwa zifuatazo;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Masomo
11 ya semina kamili ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
3. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
4. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
5. Mfululizo
wa Tafsiri ya kitabu mashuhuri cha THINK & GROW RICH kwa Kiswahili.
6. Kuunganishwa
na blogu ya kulipia ya michanganuo bure.
7. Vielezo(Templates)
za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
8. Masomo
yote yaliyopita katika group la whatsapp la MICHANGANUO NA MZUNGUKO WA FEDHA.
9. Mfumo
mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha
mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo
msaidizi kudokoa hata senti 5
10. Somo
muhimu sana la mzunguko wa fedha.
11. Ukurasa
mmoja wa mchanganuo.
Siyo lazima uwe na WHATSAPP ndipo uweze
kupata masomo haya kwani pia tunatuma kupitia email na blog maalumu ya private.
Namba za malipo ni 0712202244 au 0765553030 jina hutokea Peter Augustino
Tarimo. Unaweza kutuma ujumbe wa simu wa kawaida au wa whatsapp kupitia
0765553030 kutujulisha kama umeshalipa na sisi tutakutumia item zako zote muda
huohuo pamoja na kukuunganisha katika group.
2. VITABU MBALIMBALI VYA
BIASHARA NA UJASIRIAMALI
Unaweza pia kujipatia softcopy au Hardcopy za
vitabu vinavyoonekana majalada yake hapo chini kutoka kwetu; Bei ya vitabu
vyote vitatu SOFTCOPY ni sh. 18,000/= lakini
pia ukihitaji kimojakimoja unaweza
kupata kwa sh. elfu 10 hicho cha kwanza, elfu 5 cha pili na elfu 3 hicho cha
tatu.
1
2
3
HARDCOPY
cha
kwanza ni sh. Elfu 20, cha pili elfu 10 na cha tatu sh. Elfu 5, ukiwa dar
tutakuletea mpaka ulipo ila utaongeza sh elfu 2 za nauli na ukiwa mikoani agiza
mtu anayefika Dar akuchukulie au tunaweza pia kutuma kwa njia ya basi na utaongeza
gharama za usafiri kutegemea na basi au mkoa ulipo.
SANTE SANA
Peter A. Tarimo.
Self help books tz
Pamoja sana mwandishi
ReplyDeleteNice
ReplyDelete