Wajasiriamali Wengi na wale wote wanaotamani siku moja
kuja kuwa wawekezaji wakubwa wangependa sana kupata njia ambayo wangeweza
kuifuata hatua kwa hatua mpaka kuwafikisha kwenye mafanikio wanayoyatamani iwe
ni maisha mazuri, utajiri au hata uhuru kamili wa kifedha.
Lakini pamoja na njia kujulikana wazi kabisa na kuwepo
mifano ya matajiri au watu waliofanikiwa kupitia njia hizo, bado imekuwa vigumu
wengi wetu kuweza kukamilisha mchakato huo. Wajasiriamali wengi hukatishwa tamaa na kujikuta katika hali ambayo unaweza
ukaifananisha na mtu aliye kwenye handaki(njia ndefu ipitayo chinichini kwenye
ardhi mfano wa daraja refu). Shimo lenye giza nene na nuru hafifu sana huku
kukiwa hakuna hatua zozote za maana zinazopigwa kusonga mbele na wakati
mwingine bila ya kupiga hatua kabisa.
Kama wewe mjasiriamali ndio upo ndani ya handaki hili
lenye giza nene na mishumaa michache sana inayokuwezesha kuona angalao kidogo kwa kupapasa, utachukua hatua gani?
Mpenzi msomaji, somo hili lililo na funzo kubwa kwa
mjasiriamali yeyote yule anaye ‘struggle’ hangaika litafundishwa leo hii katika
Group la Whatsapp na Email la MICHANGANUO ONLINE. Tutaweza kufahamu kwa kina ni
kwanini njia za kufanikiwa zinajulikana wazi lakini bado wengi wetu tunashindwa
kufikia mafanikio ya kweli kimaisha. Sambamba na somo hili la leo pia kutakuwa
na mfululizo wa tafsiri ya kitabu cha THINK & GROW RICH kwa Kiswahili na
leo tunaanza rasmi Sura ya 10 baada ya jana kumalizia sura ya 9.
Masomo sasa ni kila siku kuhusu PESA, MICHANGANUO YA
BIASHARA pamoja na TAFSIRI ya THINK & GROW RICH. Mtu anapojiunga pia tunamtumia
papo hapo offa ya vitu(items) nyingine 10 yakiwemo masomo na mijadala yote
iliyopita kwenye Group. Ikiwa hutumii Whatsapp masomo utapata kama kawaida
kupitia Email au blogu ya private ya wanachama.
Ili kujiunga na masomo haya unaweza kulipia moja kwa moja kupitia namba zeti za simu, 0712202244 au 0765553030 jina hutokea Peter Augustino Tarimo, kisha tutumie ujumbe. Unaweza pia kuwasiliana na sisi kwa maelezo zaidi kupitia namba hizo au WHATSAPP 0765553030
0 Response to "KANUNI YA KUPATA FEDHA INAJULIKANA, UGUMU UPO WAPI?"
Post a Comment