Mada niliyokuletea leo hii itaegemea katika
maudhui yaliyopo kwenye kitabu cha THINK & GROW RICH (FIKIRI UTAJIRIKE)
Kitabu hiki tunatoa tafsiri yake kila siku katika Group la Whatsapp na email la
MICHANGANUO ONLINE na baadhi ya sura za kitabu hicho pia zipo kwenye blogu hii
ya jifunzeujasiriamali.
Katika sura ya 10 ambayo tumeanza kupost
sehemu ya kwanza jana katika group, Napoleon Hill mwandishi wa kitabu hicho
maarufu duniani anazungumzia kitu kiitwacho, “MASTER MIND” au “MASTER MIND
GROUP”. Maneno haya yanamaanisha ushirika wa watu 2 au zaidi waliounganisha
nguvu, kwa maneno mengine unaweza ukaita ni “KUNDI LA KUSHAURIANA” au “KUNDI LA
MASHAURIANO”
Kama kuna silaha kubwa na yenye nguvu zaidi
iliyowahi kutumiwa na watu wengi waliofanikiwa duniani, wawe ni matajiri, wenye
viwanda, wasanii mashuhuri, wanasiasa na wasomi, basi ni silaha hii ya ya Kundi
la mashauriano(Master Mind Group)
Katika kundi la kushauriana, mtu anaweza
kupata nguvu kubwa itokanayo na wenzake katika kundi na pia nguvu kutoka juu
kwa NGUVU iliyo kuu zaidi ya zote au MUNGU, vyovyote vile utakavyoiita nguvu
hii, katika kitabu hiki imetajwa kuwa ni NGUVU KUU(INFINITE INTELLIGENCE)
ambayo kimsingi kama wewe unaamini, ni Mungu muumba wa nguvu nyingine zote
Ulimwenguni.
UTAUNDAJE KUNDI LAKO LA KUSHAURIANA MASTER
MIND GROUP?
1. Chagua
watu ambao tayari wana maono yanayofanana na ya kwako bila kujali kama
wamekupita sana kiuwezo lakini hakikisha angalao mpo katika levo moja
kiuwezo(mnafanana) au wanakuzidi iwe ni kiuchumi, kielimu nk.
2. Ukweli
ni kwamba watu hupenda kuwa katika ushirikiano lakini wanashindwa kupata watu
sahihi wanaoendana nao kimaono. Lakini siku hizi Intaneti ikiwa imerahisisha
sana mambo tofauti na enzi za nyuma kuunda group la kushauriana imekuwa jambo
jepesi sana.
3. Unaweza
ukatumia mitandao ya kijamii kuunda kundi lako la mashauriano mfano facebook,
whatsapp na mengineyo.
4. Idadi
ya watu katika kundi la kushauriana huanzia watu wawili na kuendelea.
5. Makundi
haya siyo sawa na vyama ambapo kunakuwa na uongozi na wanachama wengine
kuwajibika kwa viongozi hapana, ndani ya kundi mnaishi kwa
masikilizano(harmony), kusaidiana, kuiunuana kimawazo na kiushauri na hata
wakati mwingine kwa hali na mali.
Sura hii ya 10 ina umuhimu mkubwa kwa yeyote
anayesoma au aliywahi kusoma kitabu hiki. Ushirikiano unaotajwa hapa ni moja ya
kigezo kikubwa mno katika kufanikiwa mtu yeyote yule. Hakuna mtu leo duniani
anayeweza akasimama na kudai aliweza kufanikiwa katika nyanja yeyote ile
mwenyewe pasipo kuwepo na msaada wa kundi lake la mashauriano(master mind
group). Upana wa somo hili sina namna ninayoweza kukueleza hapa ukaupata wote
zaidi ya wewe mwenyewe kuisoma sura hiyo kwa kituo.
Napoleo Hill anawataja baadhi ya watu
mashuhuri na waliokuwa matajiri wakubwa wa Dunia nyakati hizo kama kina Henry
Ford, Thomas Edison na Andrew Carnegie kuwa walikuwa na makundi yao ya
kushauriana. Mfano Bwana Ford akiwa na elimu yake ya miezi 3 tu shuleni,
aliweza kulitumia vyema kundi lake la kushauriana na kujikuta ndani ya miaka 10 akiwa ni zaidi ya
Profesa wa chuo kikuu kwa maarifa mengi aliyochota kutoka kwa wanachama wa
kundi lake. Alikuwa mjanja kuchagua watu sahihi.
Mimi binafsi nimelifanya kundi la whatsapp la
MICHANGANUO ONLINE kuwa kundi la kushauriana(Master mind group). Namna
tunavyoendesha mambo yetu kwenye kundi hili ni sawa sawa kma nilivyoeleza hapo
juu. Wote tuna maono yanayofanana ya kutaka kufanikiwa zaidi kimaisha.
Ngugu msomaji ikiwa bado hujajiunga katika
kundi hili, nakukaribisha sana njoo ujiunge, kuna faida nyingi utakazozipata
mbali na masomo na vitabu. Sasa hivi tupo zaidi ya watu 50, wote ni watu makini
na kila mmoja wetu yupo kwenye tasnia yake lakini kile kinachotuunganisha
pamoja ni ujasiriamali.
Haijalishi ikiwa upo katika tasnia ya habari,
ufugaji, kilimo, uhandisi, sheria au nyingine yeyote, lakini spirit yetu kubwawote
ni kufanikiwa, kuwa na maisha bora zaidi kiuchumi, kiafya, kiroho na kiakili
pia. Binadamu lazima vitu vyote hivi vibalansi ndipo mtu useme umefanikiwa.
Haitosi tu kuwa na hela nyingi wakati ukitetereka kiafya au kimahusiano na wale
uwapendao.
Jana katika group letu tulikuwa na somo la
fedha lililosema ‘KANUNI YA KUPATA FEDHA INAJULIKANA, UGUMU UPO WAPI?’ pia
tulianza sehemu ya kwanza ya Sura ya 10 ya tafsiri ya kitabu cha Think &
Grow Rich.
Leo hii tutakuwa na somo la michanganuo na
litahusu; “MAUZO YANAYORUDISHA GHARAMA”(BREAK EVEN SALES). Hii inatokana na
maombi ya baadhi ya wanakikundi waliotaka ufafanuzi zaidi wa kipengele hiki
kwenye mpango wa biashara hasa kwa upande wa biashara ya bidhaa zisizoweza
kuhesabika moja moja kwa urahisi. Leo
somo hili tutalitazama kwa namna ya kipekee kabisa.
Ada ya kujiunga na Group hili ni shilingi
elfu 10 ambayo ni kwaajili ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli hizi,
mimi naamini kabisa faida nitakazozipata nikiwa kama mwanachama wa group hili
ni nyingi kushinda hata kama ningelichaji kiingilio cha shilingi laki moja.
Ikiwa na wewe ndugu msomaji utapenda kujiunga
na Group hili, unaweza kutuma ada kupitia namba hizi hapa, 0712202244 au
0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe kwa meseji
au ukitumia whatsapp 0765553030
Ikiwa hutumii Whatsapp bado unaweza kujiunga
na group na ukapata masomo kupitia email au blogu ya private ya masomo.
Baadhi ya masomo yaliyopita na vitu
mbalimbali tunavyotuma kwa mtu anayejiunga mbali na masomo ya kila siku ni hivi
hapa chini;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Masomo
11 ya semina kamili ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
3. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
4. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
5. Mfululizo
wa Tafsiri ya kitabu mashuhuri cha THINK & GROW RICH kwa Kiswahili.
6. Kuunganishwa
na blogu ya kulipia ya michanganuo bure.
7. Vielezo(Templates)
za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
8. Masomo
yote yaliyopita katika group la whatsapp la MICHANGANUO NA MZUNGUKO WA FEDHA.
9. Mfumo
mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha
mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo
msaidizi kudokoa hata senti 5
10. Somo
muhimu sana la mzunguko wa fedha.
11. Ukurasa
mmoja wa mchanganuo.
……………………………………………………..............................
Kwa vitabu mbalimbali vya biashara na
ujasiriamali katika lugha ya Kiswahili unaweza kutembelea ukurasa huu hapa,
SMART BOOK TANZANIA
0 Response to "KWANINI KUNDI LA KUSHAURIANA(MASTER MIND GROUP) NI MUHIMU KWA KILA ANAYETAFUTA MAFANIKIO?"
Post a Comment