UJENZI WA MABANDA YA KUKU ISIWE KIKWAZO CHA WEWE KUANZISHA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UJENZI WA MABANDA YA KUKU ISIWE KIKWAZO CHA WEWE KUANZISHA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU

BANDA LA KISASA LA KUFUGIA KUKU

Mabanda ya kuku au nyumba kwa ajili ya kufugia kuku ukiacha chakula ndiyo kitu kinachogharimu uwekezaji mkubwa tena katika biashara ya ufugaji wa kuku aina yeyote ile iwe ni kuku wa mayai, kuku wa nyama, kuku wa kienyeji au hata kuku chotara, kabla hata mfugaji hajaamua kwenda kununua vifaranga ni lazima kwanza afahamu akishawaleta vifaranga wake ama kuku hao atawaweka wapi.  Lakini wala haipaswi gharama hizo kuwa kubwa kiasi cha kutisha.


Gharama za ujenzi wa mabanda ya kuku zitategemea wewe mwenyewe mfugaji uwezo wako kifedha, aina ya mabanda unayotaka, uimara wa vifaa na hata ukubwa wa mabanda yenyewe. Banda linaweza kuwa ni la gharama ya juu sana au ya chini lakini kitu cha msingi cha kuzingatia ni mahitaji ya kuku. Ni lazima ufikirie kwanza ni kwanini kuku wanahitaji banda?


Mabanda yako ya kuku yakiweza kutimiza masharti au mahitaji hayo huna sababu ya kuumiza kichwa eti ni wapi utapata fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya kisasa ya kuku. Mafanikio ya ufugaji wa kuku hayategemei kuwa na banda la gharama kubwa bali banda litakalokidhi vigezo na mahitaji ya msingi ya kuku wako. Banda la kuku linatakiwa litimize vigezo vikuu vifuatavyo;

1.  Banda la kuku linatakiwa kuwa na paa lisilovuja wakati wa mvua.
2.  Kuwakinga kuku wakati wa jua, upepo na baridi kali.
3.  Banda liwe rahisi kufanya usafi
4.  Banda liwe imara kuzuia wezi, wanyama na wadudu wabaya kama vicheche, nyoka, mwewe, mbwa, paka na fisi.
5.  Sakafu ya banda iwe tambarare na isiyoruhusu maji kutoka nje kuingia ndani.
6.  Banda likae sehemu iliyoinuka kidogo kuzuia mafuriko wakati wa mvua.

Ujenzi wa banda unaweza ukawa kikwazo kikubwa cha mtu kuanza ufugaji wa kuku kutokana na gharama lakini mjasiriamali makini anaweza akapunguza gharama za ujenzi wa mabanda kwa kiasi kikubwa kwa kuamua kujenga mabanda kwa kutumia vifaa mbalimbali vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira aliyopo huku akizingatia vigezo vilivyotajwa pale juu. Ikiwa udongo ndiyo material pekee inayopatikana kirahisi zaidi pale ulipo, basi fyatua matofali yako ya udongo mwenyewe kupunguza gharama au kama miti ya mitete ndiyo inayopatikana kwa urahisi itumie achana na nyavu za bei mbaya dukani.


Unaweza hata ukatumia vipande vya mabati ya zamani vilivyotupwa au utakavyonunua kwa bei rahisi kutoka kwa watu wanaouza vitu vilivyokwisha tumika. Ukishaanza ufugaji wako na baadae kupata faida ya kutosha, unaweza sasa ukajenga mabanda kwa kutumia vifaa imara zaidi na vya kudumu.

……………………………………………………..
Ndugu msomaji wa blogu hii napenda kukujulisha kwamba masomo katika Group letu la Whatsapp, email na blogu ya private yanaendelea kila siku, jana tulikuwa na somo muhimu sana la Michanganuo lililohusu Jinsi ya kukokotoa kiasi cha mauzo yanayorudisha gharama zote za mradi(BREAK EVEN SALES), ni somo washiriki wengi walikuwa wameomba tulirudie kwa kina japo lilishafundishwa siku za nyuma. 

Hesabu hii katika mchanganuo wa biashara ni muhimu sana kwani inaainisha uhusiano mkubwa uliopo baina ya gharama na mauzo ya bidhaa au huduma. Kwa kanuni rahisi kabisa mtu unaweza kukokotoa hesabu hiyo bila hata kuhitaji utaalamu wowote. PDF ya somo hili ipo na tumeiweka katika listi ya vitu(items) zile 13 tunazorusha kwa washiriki wapya wanaojiunga na group. Kwa hiyo ikiwa ulikosa somo hilo bado una fursa ya kulisoma pindi utakapojiunga na group.

Leo hii Jumapili ratiba ya group inaonyesha tutakuwa na masomo 2, moja  linahusu Fedha na la pili ni tafsiri ya Kiswahili ya kitabu cha THINK & GROW RICH na tutakuwa na sehemu ya pili ya sura ya 10 kuhusu Kundi la kushauriana(Master Mind Group)

Karibu sana ujiunge, ada ni shilingi elfu 10, na unakuwa mwanachama wa kudumu. Unaweza ukalipia moja kwa moja kupitia simu ya mkononi namba, 0712202244  au  0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo kisha ukatuma meseji kuwa tukuunganishe na kukutumia items. Namba yetu ya whatsapp pia ni 0765553030

ASANTE SANA JUMAPILI NJEMA.


1 Response to "UJENZI WA MABANDA YA KUKU ISIWE KIKWAZO CHA WEWE KUANZISHA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU"