Ukweli kwamba mtu unaweza ukafanikiwa haraka
katika biashara yako bila ya kuwa na mtaji mkubwa ni jambo gumu lakini pia ni
jambo linalowezekana kabisa. Kuna watu wengi waliowahi kutumia mazingira ama
fursa hii ya kujenga mtandao(networking) na wajasiriamali waliofanikiwa na
wakapata mafanikio ya kushangaza.
Hata hivyo mafanikio katika biashara au
uwekezaji yanategemea vigezo vingi ikiwa ni pamoja na hiki cha kujenga ukaribu
ama mtandao na wajasiriamali mashuhuri waliofanikiwa katika biashara au sekta
unayotamani kubobea. Miongoni mwa vigezo hivyo ni hivi nitakavyovitaja hapa
chini;
1. Uwezo
wako wa kujenga mtandao na watu hasa wale waliokuwa na uzoefu wa kutosha na biashara
ile unayotaka kuifanya.
2. Uwezo
wako wa kujenga biashara yenye faida na inayoweza kujitanua kwa urahisi.
3. Uwezo
wako wa kuendelea kubakia kuwa mvumilivu huku ukikataa kushindwa.
4. Kiasi
cha muda na rasilimali unazotumia katika kujifunza ili kuwa mahiri katika sekta
yako(eneo ulipo)
5. Uwezo
wako wa kukopa kwa riba kidogo na kuutumia mkopo huo kwa faida.
6. Uwezo
wako wa kuwa na mali(asseti) zinazokuingizia fedha badala ya zile
zinazokuondolea fedha(Liabilities)
7. Utayari
wako wa kujifunza kutoka kwa wale walio na uzoefu.
8. Jinsi
unavyoweza kukabiliana na wasiwasi, kukatishwa tamaa, kushindwa na kukataliwa.
9. Bahati.
Leo hii usiku Group letu la masomo ya kila
siku ya fedha na michanganuo, MICHAGANUO ONLINE, tutakwenda kukizungumzia kwa
undani kabisa moja kati ya vigezo vya mafanikio makubwa kibiashara vilivyotajwa
hapo juu, kipengele cha kwanza cha kujenga ukaribu au mtandao(networking) na
wajasiriamali au watu mashuhuri katika sekta unayofanyia biashara yako.
Kwa mfano unaweza ukawaza na kudhani kwamba
ni jambo lisilowezekana kabisa wewe kama mjasiriamali mdogo kuwafuata na kuzungumza
na wafanyabiashara wakubwa kabisa nchini wenye uwezo ukabadilishana nao mawazo,
kweli siyo jambo rahisi hata kidogo na ugumu huo hautokani na wajasiriamali hao
kujiona wako juu hawahitaji kuzungumza na watu wadogo hapana, wanapenda sana
kujenga mitandao na watu wa kawaida lakini tatizo ni kwamba, wale wanaohitaji
kujenga nao mitandao ni wengi mno.
Ratiba zao ziko ‘tight’ kiasi kwamba
haiwezekani kabisa kusema wamsikilize kila mtu anayetaka kujenga nao ukaribu.
Ndio maana ukifika maofisini mwao wakati mwingine utaishia tu kuzungumza na
masekretary wao, huwezi ukaonana nao ana kwa ana sembuse kujenga nao mitandao.
Sasa swali ni je, utawezaje wewe kama
mjasiriamali mdogo kujenga ukaribu(mtandao) na wajasiriamali wakubwa
waliofanikiwa katika kukuwezesha haraka kibiashara?
Kumbuka wajasiriamali hao wanao uwezo mkubwa
siyo kifedha tu bali zaidi ni katika uzoefu waliokuwa nao. Kuwa tu karibu nao
hata kama hawatakupa pesa inatosha kabisa kukufanya wewe uzione fursa ambazo
kabla usingeliweza kuziona.
Watu wengi tunakosea kufikiri kwamba, mtu ni
lazima kwanza uwe na pesa ndipo uweze kupata pesa, lakini ukweli siyo kila
wakati inakuwa hivyo. Kuna fursa nyingine kama hii ya kujenga mtandao na
wajasiriamali wakubwa wenye uzofu inayoweza kumuinua mtu haraka kimtaji.
Karibu sana kwenye GROUP letu tujifunze
pamoja kila siku. Hili siyo somo la kukosa hata kidogo.
Ni kwa jinsi gani unavyoweza kujenga mtandao na wajasiriamali wakubwa kabisa waliofanikiwa wakati huna kitu mfukoni na wakati huohuo ukawafanya wakupe siri za wewe kuweza kutoka pale ulipo kimtaji na kibiashara ndiyo mada kuu ya siku ya leo.
Ni kwa jinsi gani unavyoweza kujenga mtandao na wajasiriamali wakubwa kabisa waliofanikiwa wakati huna kitu mfukoni na wakati huohuo ukawafanya wakupe siri za wewe kuweza kutoka pale ulipo kimtaji na kibiashara ndiyo mada kuu ya siku ya leo.
Wanaojiunga na programu hii baada ya kulipia
kiingilio shilingi elfu 10, huwa tunawatumia na offa ya vitu vyote vifuatavyo
bila gharama nyingine zozote zile za ziada;
WHATSAPP: 0765553030
SIMU: 0712202244
JINA: Peter Augustino Tarimo
0 Response to "UKARIBU NA WAJASIRIAMALI MASHUHURI WALIOFANIKIWA KUNAVYOWEZA KUKUINUA KIMTAJI(NETWORKING)"
Post a Comment