Kabla hujaamua kwa dhati kabisa kwamba
unataka kuanzisha biashara ya ufugaji wa kuku kibiashara ikuletee faida, ni
lazima kwanza ufanye utafiti wa kina(upembuzi yakinifu) katika masuala yote
yale yanayohusiana na aina ya biashara ya kuku unayotaka kufanya. Inawezekana
unataka kufuga kuku wa nyama, kuku wa mayai, kuku wa kienyeji au hata kuku
chotara aina ya kroiller nk.ilimradi umetaka kufuga kuku kama biashara
vinginevyo unaweza ukawa unapoteza muda wako bure na mtaji(fedha) ulizozipata
kwa tabu.
Baada ya kufanya utafiti wako, sasa utaweza
kuandaa mpango wa biashara yako ya ufugaji wa kuku uliochagua kufanya na mpango
wa biashara siyo lazima uandike mreefu sana hapana, unaweza tu kwa kutumia
ukurasa mmoja wa karatasi ukapanga ni nini unachokusudia kukifanya, gharama
zitakazohitajika ni zipi na makisio ya mapato yake na faida(kile unachotarajia
kupata) ni kiasi gani.
Bila ya kupoteza muda, hebu tuone moja kwa
moja ni maswali yapi unayopaswa kuyajibu unapofanya utafiti wa biashara ya
ufugaji wa kuku;
VIFARANGA
1) Gharama
na upatikanaji wa vifaranga ukoje?
2) Utanunua
sehemu gani vifaranga?
3) Bei ya
kila kifaranga ni shilingi ngapi?
4) Gharama
ya usafiri kama utawatoa mbali ni kiasi gani?
5) Je
Utaanza na vifaranga wa siku moja, wiki au kuku wa muda gani?
CHAKULA
1) Utatengeneza
chakula cha kuku mwenyewe au utanunua kilichotengenezwa tayari madukani?
2) Kuna
maduka au kampuni zinazouza chakula cha kuku karibu na mradi ulipo?
3) Bei
ya mfuko mmoja wa chakula cha kuku ni shilingi ngapi?
4) Kuna
gharama zozote za usafirishaji wa chakula?
VIFAA
MBALIMBALI NA BANDA
1) Unalo
banda au utakodisha?
2) Gharama
za banda ni kiasi gani?
3) Mahitaji
ya vifaa vya kulishia na maji pamoja na bei zake ni kiasi gani?
4) Utahitaji
vitalu vingapi?
5) Gharama
za vitalu ni kiasi gani?
6) Ni
wapi utapata matandazo na kwa gharama kiasi gani?
7) Utapata
wapi huduma za chanjo na dawa?
MASWALI
YA SOKO
1) Ni wapi
utauza kuku/mayai?
2) Utawauzia
kina nani? Ni majirani, mashuleni, sokoni, viwandani, au katika maduka makubwa?
3) Ni
kina nani wanaofuga kuku sawa na utakaofuga wewe na bei zao huwa zikoje?
4) Kwanini
watu wanunue kutoka kwako?
5) Bei
yako itakuwa shilingi ngapi?
6) Utakuwa
na uwezo wa kuuza kiasi gani cha kuku au mayai kwa mwezi, msimu au kwa mwaka?
7) Utajuaje
kama utaweza kuuza kiasi hicho?
Maswali haya ndiyo yatakayokuwezesha kuweka
mpango wa biashara yako ya ufugaji wa kuku iwe ni kuku wa mayai, kuku wa nyama,
kuku wa kienyeji ama kuku chotara.
…………………………………………………
Ndugu
msomaji, biashara ya ufugaji wa kuku ni moja kati ya biashara zilizo na fursa
kubwa kutokana na uwezo wake wa kuzalisha faida kubwa ndani ya kipindi
kifupi.Lakini ili kuweza kunufaika na fursa hii kubwa mfugaji yeyote yule hana
budi kuwa na taarifa zote sahihi juu ya aina ya ufugaji kuku anaotaka kuufanya
hasa hasa katika upande wa gharama mbalimbali zinazohitajika.
Tuna
kifurushi cha michanganuo mitatu 3 ya ufugaji wa kuku kijulikanacho kama MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS, kuku wa
mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji. Michanganuo hii inaweza kuwa msaada
mkubwa kwa mtu anayetaka kufuga kuku kibiashara au hata ambaye ameshaanza
kufuga tayari na angependa kuboresha mradi wake kuwa wa kisasa zaidi.
Kifurushi
hiki kinapatikana kama softcopy kwa njia ya e-mail na bei yake ni shilingi elfu
10 tu. Unaponunua tunakupa na offa ya vitu vingine mbalimbali pamoja na kuwa
mwanachama wa kudumu katika GROUP la masomo ya kila siku
la MICHANGANUO ONLINE. Offa hiyo ni hii hapa chini;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Masomo
11 ya semina kamili ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
3. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
4. Mfululizo
wa Tafsiri ya kitabu mashuhuri cha THINK & GROW RICH kwa Kiswahili.
5. Kuunganishwa
na blogu ya kulipia ya michanganuo bure.
6. Vielezo(Templates)
za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
7. Masomo
yote yaliyopita katika group la whatsapp la MICHANGANUO NA MZUNGUKO WA FEDHA.
8. Mfumo
mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha
mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo
msaidizi kudokoa hata senti 5
9. Somo
muhimu sana la mzunguko wa fedha.
10. Ukurasa
mmoja wa mchanganuo.
Ikiwa utahitaji kifurushi hicho unaweza kulipia moja kwa moja sh. elfu 10 kupitia namba zetu, 0712202244 au 0765553030 au WHATSAPP 0765553030 kisha tuma ujumbe kutujulisha nasisi tutakutumia kila kitu muda huohuo. Ikiwa hutumii whatsapp hamna shida kwani masomo tunatuma pia kupitia email na blogu ya private.
0 Response to "UTAJUAJE KAMA BIASHARA YAKO YA UFUGAJI WA KUKU ITAKUPA FAIDA?"
Post a Comment