Kila mara huwa tunajiuliza swali hili
kichwani, “ Nitatumia mbinu zipi ili kufanya matokeo ya kile ninachokifanya
kuwa bora na chenye tija zaidi kuliko vile nilivyozoea kufanya?” Na hata ikiwa
pengine hujawahi kujiuliza swali hilo, ni wakati muafaka sasa wa kujiuliza
swali hili muhimu sana maishani. Ili kuweza kupata majibu ya swali hilo
unapaswa kwanza kujibu maswali haya mengine mawili madogo yanayofuata hapa
chini;
1. Je,
unaelekeza nguvu zako katika mambo sahihi?
2. Unazijua
nguvu zako ziliko au umezitawanya katika maeneo tofauti?
Tangu ulipokuwa mtoto mdogo bila shaka
utakuwa umewahi kusikia ama kujifunza medhali(msemo) huu kutoka kwa wazazi, walezi
au hata kutoka kwa waalimu wako wa lugha ya Kiswahili kwamba; Usikimbie na kuku wengi, utaambulia manyoya”
Msemo huu kama ulivyokuwa na maana miaka hiyo iliyopita mpaka leo na hata kesho
haitakaa ipoteze maana yake, itabakia kuwa vilevile kwamba; kulenga mambo mengi
mno kwa wakati mmoja hakuwezi kutusaidia kupata matokeo bora kabisa maishani.
Haitoshi tu kudai unafanyia kazi mambo
machache, lakini pia mambo hayo machache ni sahihi kwako? Hapa ndipo linapoingia
suala la nguvu au uwezo uliokuwa nao. Ni kitu gani ambacho ukikifanya basi
unasema, “ Ndiyo nimefanya” Kile kitu unachokiweza zaidi kushinda vitu
vingine. Kufanya kitu cha namna hiyo ni lazima matokeo yake yawe ni ya
kushangaza(Great!)
Moja ya siri kubwa zaidi ya mtu kuishi maisha
yaliyojaa furaha ni kitendo cha kufanya shughuli au kile kitu akipendacho
maishani, iwe ni kazi, biashara, au shughuli nyingine yeyote ile inayomuwezesha
kuishi.
Mtaalamu mmoja katika kanuni yake ya 80/20
aliyoiita Pareto anasisitiza juu ya umuhimu wa kuelekeza nguvu katika yale
mambo machache yanayotupatia tija kubwa zaidi na kuachana ama kuyapunguza yale
mambo au shughuli zisizokuwa na faida ya maana.
Mtaalamu huyo anataja mfano wa
watu wa mauzo (salespeople) ambao anasema huitumia vizuri sana kanuni hiyo ya
80/20 kwa kulenga zaidi katika asilimia 20% ya wateja wao wanaowapatia mapato
asilimia 80% na kutokujisumbua kabisa au kupoteza muda mwingi na wale wateja
asilimia 80% ambao mchango wa mapato yao kwao ni mdogo sana.
Wajasiriamali wajanja mara zote hutambua na
kuweka juhudi katika yale mambo machache tu yanayowapa matokeo yaliyokuwa bora
kabisa hasa ikiwa mjasiriamali bado yupo katika hatua zake za mwanzo na
rasilimali alizokuwa nazo ni chache. Kwa wajasiriamali wakubwa au
wafanyabiashara ambao tayari wameshakuwa na mitaji ya uhakika wanaweza wakaamua
kulenga mambo mengi kwa wakati mmoja na wakafanikiwa kwani tayari wanao uwezo
wa kutumia nyenzo au rasilimali mbalimbali kutekeleza majukumu ya biashara zao.
0 Response to "NJIA WAJANJA WANAYOITUMIA KUPATA MATOKEO BORA ZAIDI KWA KILA WANACHOKIFANYA MAISHANI"
Post a Comment