Hata hivyo watu wengine huiweka biashara ya
urembo katika kundi lake na biashara ya vipodozi kwenye kundi jingine kulingana
na wanavyoona. Wanahusisha urembo na vitu vya kuvaa kama vile hereni, bangili,
mikufu, kucha nk. huku wakihusisha vipodozi na bidhaa zote za ngozi, nywele na
manukato mfano losheni, cream na pafyumu.
Kitaalamu, vipodozi ni kitu chochote kile
kinachoweza kutumiwa katika kufanya muonekano wa mtu uwe wa kuvutia zaidi au
kuwa na harufu nzuri. Vitu hivyo ni pamoja na bidhaa mbalimbali za mwili na ngozi
kama vile sabuni, lotion, krimu, dawa za mswaki, perfume, make-ups nk.
Sidhani kama kuna binadamu leo hii duniani anaweza akadai hatumii kipodozi cha aina yeyote ile na kama basi atakuwepo binadamu wa namna hiyo basi atakuwa hana tofauti na sokwe mwitu au nyani wanaoishi katika misitu minene kule congo na Brazili
SEKTA
YA BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI NCHINI TANZANIA
Kutokana na ongezeko la kipato kwa watu wa
tabaka la watu wa kati nchini Tanzania, matumizi ya bidhaa za urembo na
vipodozi yameongezeka tangu mwanzoni mwa miaka ya 90 na kuendelea mpaka hivi
sasa. Ukuaji huo unakadiriwa kuwa ni wa kiwango cha asilimia 8% kwa mwaka. Hata
hivyo matumizi ya vipodozi na urembo Tanzania kwa kiasi kikubwa watu wamekuwa
wakitumia vipodozi bandia ambavyo siyo halisi na hatari kwa afya zao.
Vipodozi hivyo bandia huingia nchini kutoka
nchi za China, Jamhiri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC), Zambia na Kenya. Lakini
pia vipodozi halisi(Original) hupatikana katika maduka machache makubwa, Saluni
kubwa kubwa, baadhi ya maduka ya madawa, maduka makubwa ya kisasa kama shopping
malls na supermarkets pamoja na kwa watu wanaoagiza vipodozi hivyo moja kwa moja
kutoka ng’ambo au Dubai.
Juhudi kubwa za serikali chini ya mamlaka zake
mbalimbali kama vile TRA na TFDA kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitoa elimu kwa
wananchi dhidi ya vipodozi hivyo haramu na juhudi hizo sasa zimeanza kuonyesha
kuzaaa matunda ingawa bado kuna mahitaji makubwa ya vipodozi hivyo
yanayochangiwa na urahisi wa bei pamoja na matokeo yake ya muda mfupi. Vipodozi
haramu au bandia vina tabia ya kuonyesha matokeo ya haraka hasa vile vya
kutakatisha ngozi ambapo kwa mtu asiye na uelewa hudhani ndiyo vizuri kutumia.
KWANINI
BINADAMU TUNAPENDA KUTUMIA VIPODOZI AU KUJIREMBA?
Bila shaka yeyote ile leo hii ulivyoamka
asubuhi ulipokuwa ukioga au kufua nguo zako ulitumia sabuni kama siyo ya unga
ni sabuni ya kipande. Na ikiwa sijakosea pia baada ya kuoga, ulijipaka mafuta
hata kama ni baby care au Ashes, au ulijipaka losheni au cream. Hukuishia hapo
bado uliendelea kujipaka deodorant kwapani na kujipulizia pafyumu inayonukia
kwenye nguo zako nzuri ulizovaa. Na ikiwa wewe ni mwanamke basi mambo yalikuwa
ni moto zaidi kwani uliweka na makeup, lipstic na vitu vingine kibao.
Sasas basi, ni kwanini binadamu huwa
tunafanya jambo hilihili kila siku? Jibu ni rahisi sana, TUNAPENDA KUONEKANA NA KUJISIKIA VIZURI” Kuonekana na kujisikia
vizuri ni hitaji la msingi sana kwa binadamu karibu sawa kabisa na ilivyokuwa
kwa chakula au malazi. Sababu hii ndiyo hufanya vipodozi na vifaa vya urembo
kuwa ni bidhaa au huduma zinazonunuliwa haraka karibu sawa na bidhaa za chakula
zinavyotoka haraka.
Kila mtu hata masikini kabisa anayeishi chini
ya dola moja kwa siku anapenda kuonekana na kujisikia vizuri, tunapenda urembo
na utanashati. Lakini mbali na kujisikia na kuonekana vizuri pia vipodozi
hutusaidia katika suala zima la usafi, kutufanya tujiamini zaidi mbele ya
wenzetu na hivyo kwa kiasi kikubwa kuamua ni kwa kiwango gani tunachoweza
kuwashawishi watu wengine na jinsi watu wengine nao wanavyotuchukulia. Hivyo
biashara ya urembo na vipodozi ni biashara iliyo na fursa kubwa sana duniani
kote, Afrika na Tanzania kwa ujumla.
SABABU
MBALIMBALI ZA ONGEZEKO LA WATU KUTUMIA VIPODOZI ZINATAJWA KUWA NI HIZI
ZIFUATAZO;
1. Vipodozi
kuwa ni mahitaji ya msingi ya kila siku, kila mtu siku hizi
hutumia vipodozi. Urembo na mitindo huwezi tena ukavitenganisha na maisha ya
binadamu ya kila siku.
2. Kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na kipato kwa watu wa daraja la
kati na la chini Tanzania.
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka
2012, idadi ya watu imeongezeka kutoka milioni 34 mwaka 2002 mpaka kufikia watu
milioni 44.9 mwaka 2012 sawa na kasi ya ongezeko la asilimia
2.7 kwa mwaka. Inakadiria Tanzania bara kuwa na
idadi ya watu wapatao milioni 63.3 mwaka 20125. Aidha umasikini wa kipato
umepungua kutoka asilimia 33.6 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka
2012.
3. Idadi
kubwa ya vijana chini ya miaka 25
Vijana ndio watumiaji wakubwa wa bidha za urembo kwa
mfano Tanzania katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, vijana wa umri chini ya miaka
17 walikuwa ni asilimia 50.1% ya watu wote wanaopatikana nchini sawa na watu
milioni 22.5. Duniani idadi ya vijana chini ya umri wa miaka 25 ni bilioni 1.2 na kati ya hao asilimia 90% wapo katika nchi
zinazoendelea Tanzania ikiwa miongoni mwazo.
4. Wanawake
kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kipato na wa kununua vitu.
Katika jamii za Kiafrika na hata sehemu
nyingi duniani mwanamke anakabiliwa na shinikizo kubwa zaidi ya mwanaume la kuwa
na muonekano wa kuvutia(urembo). Hii ndiyo sababu kubwa ya bidhaa za vipodozi
za nyele, ngozi, kucha na make-up kuwa ndiyo zinazoongoza duniani kuuzwa kwa
kiasi kikubwa zaidi ya aina nyinginezo za vipodozi. Katika miaka ya hivi
karibuni kumekuwa na mwamko mkubwa wa wanawake kutaka usawa na wanaume katika nyanja
mbalimbali zikiwemo ajira na hata katika elimu.
Matokeo yake ni kwamba wanawake wengi sasa
wana uwezo mkubwa wa kununua vitu mbalimbali vikiwemo vipodozi. Pia wanawake
pamoja na kujinunulia wenyewe vipodozi huwa wananunuliwa pia na wapenzi wao,
waume au ndugu na jamaa zao katika familia kama zawadi. Hivyo biashara ya
urembo wa wanawake ni kubwa na iliyo na soko la uhakika.
AINA
MBALIMBALI ZA VIPODOZI, UREMBO NA BIDHAA ZA USAFI.
Sekta hii ya vipodozi au urembo tunaweza
tukazigawanya katika makundi mbalimbali yafuatayo kulingana na aina na matumizi
yake mbalimbali.
1. Bidhaa za urembo za nywele.
Kundi hili lina bidhaa kama vile, nywele za bandia, shampoo,
conditioners, rangi mbalimbali na dyes, relaxer na bidhaa mbalimbali za mitindo
ya nywele. Wadau wakubwa katika kundi hili ni saluni za kike na za kiume na
wanawake majumbani wanaozitumia bidhaa hizo wakiwa wenyewe au na mashog zao.
Wanaume nao pia hawako nyuma katika sekta hii ya nywele kwani utakuta wakiweka
dreads, wave na hata Afro katika masaluni mbalimbali ya kiume.
2.Bidhaa za Ngozi.
Kundi hili la vipodozi vya ngozi ndilo kubwa na lililo na aina nyingi
zaidi ya bidhaa kushinda makundi mengine. Karibu asilimia 30% ya vipodozi vyote
vinavyouzwa sokoni hutokana na kundi hili mfano ni “skin moisturizers”, “cleansers”,
“toners”, “ant-acne” bidhaa za urembo wa ngozi ya miguu na bidha nyingine za
usoni(facial). Watu wana ngozi tofauti
tofauti, wengine ngozi zao ni kavu, wengine ngozi zenye mafuta na wengine ngozi
zao zina mzio kwa baadhi ya bidhaa zinazotumiwa.
3. Make up
Make up zinajumuisha bidhaa zote zinazotumika kurembesha na kutia rangi
usoni au urembo wa ngozi ya uso, kwenye macho, midomo na kucha. Kundi hili nalo
limegawanyika katika bidhaa za aina mbalimbali mfano kuna lipstick, foundation,
mascara, eyeliners, bidhaa za urembo wa kucha kama vile rangi za kucha pamoja
na make up removers.
4. Bidhaa za usafi na chooni.
Katika kundi hili la vipodozi tunakutana na bidhaa zote zinazotumika
katika usafi wa mwili na kujiweka vizuri na siyo lazima ziwe ni za urembo.
Bidhaa zinazopatikana katika kundi hili pia ni zile zinazotoka haraka sana na
kuwa na mahitaji makubwa mfano sabuni za kuogea na kufulia za maji na za miche,
cream za kunyolea, hair removal(depilatories), deodorants, karatasi za
chooni(toilet paper), taulo za kike(ped) na nyiginezo nyingi zinazotumika
katika usafi wa mwili.
5. Manukato.
Kundi la Manukato ni miongoni mwa bidhaa za urembo zinazouzika kwa kiasi
kidogo zaidi lakini cha kushangaza ndiyo kundi lenye faida kubwa zaidi pengine
kushinda makundi mengine. Manukato yanajumuisha mchangayiko wa mafuta na vitu
vyote vinavyonukia ambavyo huupa mwili wa binadamu harufu ya kupendeza. Kuna
pafyumu, Eau de Toilette, airfreshner, aftershave nk.
JINSI UNAVYOWEZA KUNUFAIKA NA
FURSA KUBWA ILIYOKUWEPO KATIKA SEKTA HII YA UREMBO NA VIPODOZI NCHINI TANZANIA.
Pasipo kujali unao mtaji kiasi gani au ni uelewa kiasi gani uliokuwa nao
kuhusiana na biashara hii ya urembo(jinsi ya kuanzisha biashara ya urembo), unaweza
ukaanzisha na kunufaika na fursa kubwa iliyopo katika biashara hii kwa
kuifanyia nyumbani kwako, kutembeza mitaani au kufungua eneo lako.
Zipo njia kuu mbili ambazo unaweza ukaanzisha biashara yako mwenyewe ya
urembo au vipodozi nazo ni hizi hapa chini;
1. Kutengeneza bidhaa zako
mwenyewe za vipodozi na urembo.
Ingawa soko limesheheni bidhaa za aina nyingi za urembo na vipodozi kutoka sehemu mbalimbali duniani, hata hivyo bado kuna mahitaji makubwa ya vipodozi hasa vinavyotokana na mimea ya kiasili ya kiafrika.
Kuna watu wengi siku hizi ambao hawapendi kabisa vipodozi vinavyotokana na kemikali za
kizungu bali wanapenda urembo wa asili, aidha
vipodozi vingi kutoka ng’ambo vimetengenezwa kwa ajili ya kukidhi
mazingira na mahitaji ya ngozi za watu wa mabara zinakotengenezwa, Waafrika
tuna mahitaji yetu maalumu ambayo hayawezi kufikiwa na bidhaa hizo hivyo
ukiweza kutengeneza vipodozi vinavyokidhi mahitaji ya ngozi nyeusi unakua
umetengeneza fursa kubwa ya kuingiza fedha.
Afrika tuna miti na mimea mingi ambayo inaweza ikatumika katika
kutengeneza bidhaa za urembo, kuna miti na matunda kama vile ubuyu, ukwaju,
limao, alovera, na mengine chungu nzima. Haijalishi bidhaa yako itakuwa mpya
sana au utaamua tu kuongeza ubunifu kidogo kwenye bidhaa zilizopo sokoni tayari
lakini kikubwa hapa ni wewe kuwa mbunifu katika kuitafutia soko bidha yako(marketing) kuanzia jinsi ya kufanya
biashara ya urembo, jinsi utakavyoifungasha, maandishi utakayoweka juu ya nembo yako na hata
matangazo utakayotoa katika vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo mtandao wa
intaneti.
Hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla kuna makampuni na watu binafsi ambao
wamenufaika sana na fursa hii, wanatengeneza pesa nyingi na bidhaa zao za asili
zinapendwa mno. Mtu yeyote pi anaweza akaanzisha biashara ya vitu vya urembo au
bidhaa yake(kipodozi cha asili) na akauza kwani fursa bado ni kubwa.
2. Kuuza bidhaa za watengenezaji wengine
mbalimbali.
Hii sasa ndiyo njia ambayo watu wengi tumeizoea hapa kwetu, kufungua
biashara ya kuuza urembo na vipodozi mbalimbali kutoka nje ya nchi na hata vile
vinavyotengenezwa hapa hapa nchini kwa kuwa msambazaji au muuzaji wa rejareja
wa vipodozi.
Unaweza ukaanza kama muuzaji wa rejareja au ukaamua kuagiza kutoka nje
yanchi na kuja kuuza jumla kwa wauzaji wengine. Wauzaji wa vipodozi vya jumla
huvitoa au kuagiza nje ya nchi kama vile Dubai, China, Ulaya, Amerika ya
kaskazini, Mashariki ya kati na hata kutoka nchi za Kenya, DRC, Zambia na
Afrika ya Kusini.
Kwa wale wauzaji wa rejareja kuna walio na maduka maalumu ya vipodozi,
saloon za kike na za kiume, maduka ya dawa, masoko mbalimbali ya wazi na maeneo
watu wanayopenda kwenda kununua vitu kwa urahisi kama stendi au pembezoni mwa
barabara.
Kutegemeana na eneo utakalochagua kuweka biashara yako ya vipodozi,
mikakati yako ya soko, na kiwango cha ushindani uliopo, biashara hii ya
vipodozi au urembo inaweza kuwa ni biashara iliyo na faida kubwa kwako na
ambayo inaweza kukufanya utajirike ndani ya kipindi kifupi.
............................................................................
Mpenzi msomaji wa blogu hii ya jifunzeujasiriamali, napenda kukujulisha kuwa masomo na semina zetu za kila siku ndani ya GROUP LA WHATSAPP LA MICHANGANUO-ONLINE bado zinaendelea kila siku usiku saa 3-saa 4 tukijadili masomo mbalimbali yahusuyo michanganuo ya biashara zinazolipa pamoja na mzunguko wa fedha katika biashara zetu. Group linakaribia watu 100 sasa na kumbuka kuna ukomo wa idadi ya watu hivyo ni muda wa kuwahi mapema kabla nafasi hazijajaa.
Ada ya kujiunga na Group ni shilingi elfu 10, na namba zetu sa SIMU ni 0712202244, WHATSAPP ni 0765553030
Ada ya kujiunga na Group ni shilingi elfu 10, na namba zetu sa SIMU ni 0712202244, WHATSAPP ni 0765553030
Vitu mbalimbali unavyopewa mara unaojiunga tu ni hivi vifuatavyo;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Masomo
11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
3. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
4. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
5. Mfululizo
wa Tafsiri ya kitabu mashuhuri zaidi cha pesa, FIKIRI UTAJIRIKE
6. Kuunganishwa
na blogu ya kulipia ya michanganuo bure.
7. Vielezo(Templates)
za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
8. Masomo
yote yaliyopita katika group kuhusu MICHANGANUO NA MZUNGUKO WA FEDHA.
9. Mfumo
mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM)
unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake
pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
10. Somo
muhimu sana la mzunguko wa fedha.
11. Ukurasa
mmoja wa mchanganuo.
Hello
ReplyDeleteHow are you?
Delete