Katika safu yetu ya USHAURI, leo msomaji wetu kutoka Mbinga aliuliza swali lifuatalo,
Naomba kufahamu ikiwa chakula hiki cha kuku wa kisasa kama naweza kuwalisha kuku wa kienyeji bila madhara yeyote. Je ipo tofauti yeyote kwenye utengenezaji wa chakula kwa ajili ya kuku wa kisasa na wa kienyeji?
MAJIBU.
Virutubisho vinavyohitajika katika mwili wa kuku wa kisasa
ndivyo hivyohivyo vinavyohitajika katika mwili wa kuku wa kienyeji, hivyo kuku
wa kienyeji anapokula chakula kilichotayarishwa kwa ajili ya kuku wa kisasa
hawezi akadhurika na tena iwapo utampa kwa kiasi kinachostahili ndio atakua
vizuri na kunenepa kuliko hata angejitafutia mwenyewe chakula kwa kuchakura
ardhini.
Tofauti kubwa iliyokuwepo kati ya ulaji wa kuku wa
kienyeji na ule wa kuku wa kisasa ni kwamba kuku wa kienyeji kijenetiki ni
mstahimilivu zaidi anapokosa virutubisho vya kutosha katika mwili wake kuliko
kama ilivyokuwa kwa kuku wa kisasa. Pia kuku wa kienyeji anao uwezo wa kula
chakula cha aina moja kwa muda mrefu, nikimaanisha chakula kilichokuwa na
virutubisho vya aina moja tu, tuseme labda wanga kwa muda mrefu na asiweze
kudhurika au kuonyesha dalili yeyote ya kudumaa kama ilivyo kwa kuku wa kisasa.
Kisayansi siyo kuku tu peke yao, hata viumbe wengine
hususani wanyama, ndege, samaki na hata wadudu, wanahitaji virutubisho(viini-lishe)
muhimu vikuu vitano kusudi waweze kuishi na kukua vyema. Virutubisho hivyo ni;
Wanga, Protini, Mafuta, Vitamini na madini pamoja na maji. Kwahiyo kuku awe ni
wa kienyeji au wa kisasa anahitaji kupata makundi yote haya matano ya viinilishe
ili aweze kuishi na kukua vizuri kama inavyostahili.
Suala la chakula kwa ajili ya kuku vifaranga(starter),
kuku wanaokua(growers), kuku wa nyama(broiler mash) na kuku watagaji(layers
mash) na hata finishers hili huzingatia zaidi mahitaji maalumu ya kundi husika
kulingana na umri wake. Kwa mfano vifaranga starter mash, mchanganyiko wake wa
viinilishe protini huzingatiwa zaidi na kwa kiwango kikubwa kutokana na vifaranga
miili yao kuhitaji protini zaidi kwa ajili ya ukuaji wa haraka.
Ni hivyo hivyo na kwa kuku wa mayai wanaotaga, chakula chao
ratio yake inatakiwa vitamin na madini kupewa kipaumbele kikubwa hasa madini ya
chokaa kutokana na mahitaji ya utengenezaji wa kaka la yai kuhitaji kwa wingi
vitu hivyo. Lakini yote kwa yote chakula kwa ajili ya kuku wa aina yeyote ile
wawe ni wa kienyeji, wa kisasa, vifaranga au wa mayai ni lazima katika
mchanganyiko wa chakula chake makundi yote matano ya vyakula yawemo.
SOMA: Baada ya kufanya utafiti, sasa naanza kuadika mpango wa biashara yangu ya kuku wa mayai ya kienyeji.
Kwa mfano
1. Wanga hupatikana kutokana
na vyakula kama vile mahindi, mchele, mtama, mihogo, viazi, magimbi, viazi
vikuu, ngano, uwele, nk.
2. Protini
hutokana na vyakula vyote vya asili ya nyama kama mabaki ya nyama, ngozi na
damu. Vyakula vyote vyenye asili ya baharini kama dagaa, mabaki ya samaki nk. Wadudu
kama mchwa, funza, senene na kumbikumbi, Vyakula vyote vya jamii ya
mikundekunde kama soya, kunde, maharage mbaazi na choroko.
3. Mafuta
ni vyakula kama vile, mashudu ya alizeti, mashudu ya ufuta, karanga, nyonyo,
machicha ya nazi nk. Hata hivyo kuna vyakula vingine utakuta vina mafuta na
wanga kwa wakati mmoja au mafuta na
protini.
4. Vitamini
na madini, utakuta vyakula kama vile, chokaa, chumvi, mbogamboga na matunda ya
aina mbalimbali.
5. Maji
ya kutosha pia ni muhimu sana kwa kuku wa aina zote wawe ni wa kisasa au wa
kienyeji.
Kuku kwa asili hujitafutia chakula mwenyewe kwa kuchakura
chini na kula mimea mbalimbali ambapo anapata makundi yote ya virutubisho
vinavyotakiwa mwenyewe. Sayansi ya kutengeneza chakula cha kuku kisasa
ilitokana na binadamu kuanza kuwafuga kuku kwa kuwafungia ndani ya mabanda.
Fomula ya mchanganyiko wa makundi ya vyakula mbalimbali
huchukua nafasi ile ya kuku kujichagulia mwenyewe chakula. Kuku anapochakura
anajua kwa usahihi kabisa(automatic) ale kiasi gani cha wanga, protini na
madini bila hata ya kupangiwa na mtu yeyote kutokana na jinsi vile mwili wake
anavyojisikia ukihitaji virutubisho hivyo.
Lakini hata ikiwa kuku atakosa virutubisho sahihi
inavyostahili yeye atakula tu chochote anachokipata ilimradi ameshiba hata
ikiwa ni chakula cha aina moja tu. Kwa kuku wa kienyeji unaweza usione madhara
yake mara moja lakini kwa kuku wa kisasa wataonyesha kudumaa haraka sana.
Asante sana msomaji wa blogu yetu kutoka Mbinga Mkoani Ruvuma, naamini swali lako nimejitahidi kulijibu.
Ikiwa una swali au changamoto yeyote ya ujasiriamali unaweza kuituma hapa tukakushauri, ushauri mdogomdogo ni bure hatuchaji chochote na tunapoamua kuuweka hapa katika blogu hatutaji jina la mtu aliyeomba ushauri labda kwa ridhaa yake mwenyewe.
Asante sana msomaji wa blogu yetu kutoka Mbinga Mkoani Ruvuma, naamini swali lako nimejitahidi kulijibu.
Ikiwa una swali au changamoto yeyote ya ujasiriamali unaweza kuituma hapa tukakushauri, ushauri mdogomdogo ni bure hatuchaji chochote na tunapoamua kuuweka hapa katika blogu hatutaji jina la mtu aliyeomba ushauri labda kwa ridhaa yake mwenyewe.
……………………………………………………….
Ndugu msomaji wangu, ikiwa ulikuwa bado hujasoma mchaganuo wetu
bunifu wa kuku wa kienyeji, tafadhali nakusihi sana siyo wa kukosa kwani
utaweza kufahamu mbinu nyingi sana unazoweza ukazitumia katika kuongeza idadi
ya mayai ya kuku wa kienyeji kutoka idadi ya kawaida ya mayai 45-60 kwa mwaka
hadi mayai 200 kwa mwaka, pia utapata mbinu za kumfanya kuku wa kienyeji akue
haraka pamoja na teknolojia rahisi sana na nzuri ya kuchanganya chakula cha
kuku hata ikiwa huna fedha za kununulia mashine ya gharama kubwa.
Mchanganuo huo unapatikana ndani ya kifurushi cha michanganuo 3,
kiitwacho, MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS ambacho bei yake(softcopy) ni shilingi
elfu 10 tu. Ndani kuna michanganuo mingine 2 ya kuku wa kisasa wa mayai na kuku
wa nyama.
Ukinunua kifurushi hiki tunakupatia offa ya kitabu chetu maarufu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI(softcopy), masomo, semina zote
zilizopita pamoja na kuunganishwa katika GROUP la masomo ya kila siku la
MICHANGANUO-ONLINE
SIMU: 0712202244
WHATSAPP: 0765553030
Nashukuru sana kwa huduma yako nzuri ya uelimishaji.
ReplyDeleteNaomba unisaidie jambo moja .kwamba ni chanjo gani ambayo kuku wa nyama au bloilers huwaga wanachanjwa ili wasipatwe na mlipuko wa magonjwa