Swali huyu kijana alilonitumia Whatsap
lilikuwa kama hivi, bila kuongeza wala kupunguza nukta;
Kak, naomba msaada ako mimi ni mchanga
katika biashara naomba unikochi vizuri nmetok shule si zamani sana bado sielew
kitu.
Ata kwa mazungumzo mwanzo itakuwa vizur
Naitaj kuwa Billionaire
Wakati mwingine maswali wanayouliza vijana
hasa wale walio katika umri wa kumaliza masomo yao ya vyuo au mashuleni
yanaweza kukuchekesha au hata wakati mwingine ukafikiria pengine wanatania au
ni “wendawazimu” lakini ikiwa na wewe uliwahi kupitia umri wa ujana na kukutana
na changamoto hizi huwezi kamwe kuwabeza au kuona ni wendawazimu.
SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma, naomba ushauri, nina wakati mgumu.
SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma, naomba ushauri, nina wakati mgumu.
Vijana hasa wanaomaliza shule na vyuo
mbalimbali hupendelea sana kujua siri ya kuwa tajiri ni nini, kanuni za kuwa
tajiri na hata jinsi ya kupata pesa haraka. Kwa ujumla wanakuwa na hamu kubwa
ya kupata mafanikio katika maisha yao. Huu ndio umri sahihi binadamu anaotamani
kujua jinsi ya kufanikiwa biashara ama chochote kile atakachokifanya kwa
haraka(kwa spidi ya umeme).
Kwa hiyo maswali kama haya ikiwa wewe ni mtu
unayedili na maswala ya ushauri kwa vijana yategemee kwa asilimia kubwa sana na
ni haki yao ya msingi kupatiwa majibu sahihi na wale tuliowatangulia ama yeyote
mwenye uwezo wa kutoa majibu sahihi hata ikiwa mtoa majibu siyo Bilionea, kwani
siyo jambo rahisi kila kijana aweze kumfuata Bilionea au tajiri na kumuomba
amfundishe njia alizopitia mpaka akatajirika, ingawa pia ni vizuri zaidi kijana
akamuuliza bilionea moja kwa moja kama itawezekana.
MAJIBU
KWA SWALI LA KIJANA WETU NI HAYA HAPA
Nisingependa nirudie kuandika tena upya
makala(post) za zamani, lakini kwakuwa swali hili linanitaka hivyo,basi
nitaandika kwa ufupi kabisa dondoo muhimu tu zinazopatikana katika makala moja
isemayo, UNAPENDA KUWA KAMA BAKHRESA, MENGI, DEWJ NA ROSTAM?, Makala hii ina
maelezo ambayo yanatosha kabisa kujibu swali la kijana wetu huyu na dondoo hizo
ni hizi hapa;
1.
Anza na Ndoto au Maono.
2.
Jijengee akilini mtazamo wa mafanikio.
3.
Ongeza ufahamu wako juu ya biashara unayoifanya.
4.
Buni wazo la biashara lenye uwezo wa
kulipa haraka.
5.
Tafuta mtu wako wa mfano(Mentor)
6.
Anzisha biashara.
7.
Unda timu imara kwenye biashara yako.
8.
Tafuta mtaji wa kuendeshea biashara yako.
9.
Endesha biashara yako katika mfumo wa kampuni.
10.
Wekeza katika biashara(vitegauchumi)
vingine.
Ukitaka uwe Bilionea ni lazima ufuate kanuni
au njia hizo walizopitia mabilionea wengine wote duniani wakiwemo hata na wale
wanaopatikana hapa Tanzania. Mabillionea wote duniani wana vitu fulani
vinavyofanana ambavyo hujikuta wamevifanya iwe walikuwa wanajua au hata
hawajui. Kwa undani zaidi unaweza ukasoma makala hiyo.
Na siyo hivyo tu peke yake, ili mtu kuwa
tajiri(Bilionea) wa ‘kutupa’ ni lazima kwanza kabla ya yote uwe na
SABABU(KWANINI) unataka kuwa Bilionea. Niliwahi kuandika pia katika makala nyingine
isemayo, KWANINI KUFANIKIWA KIFEDHA SI DHAMBI NA KILA MTU ANASTAHILI AFANIKIWE? nikazitaja sababu kadhaa za watu kutaka kutajirika au kumiliki fedha nyingi
ambazo kwa kifupi nilisema ni hizi hapa;
1. Kuondokana
na mnyororo wa umasikini uliotesa kizazi chao tangu mababu.
2. Kugusa
maisha ya watu wengine(Kusaidia)
3. Kuwaridhisha
wapenzi wao-mtu anaamua ‘kufight’ kufa na kupona atajirike kisa tu mridhishe
mpenzi wake au kutaka kuoa katika familia fulani.
4. Kuwa
na uwezo wa kusikilizwa na karibu kila mtu hata serikali.
Kwa ujumla unahitaji NGUVU ITAKAYOKUSUKUMA KATIKA KUUTAFUTA HUO UBILIONEA. Njia za mtu
kuwa bilionea au kutajirika siyo siri tena wala siyo lazima mtu umfuate Bill
Gates, au Bilionea mwingine yeyote akakufundishe. Ugumu upo tu kwenye
utekelezaji wake. Ukiweza kutekeleza kwa vitendo njia hizo, Ubilionea ni haki
yako kama tu zilivyokuwa haki nyinginezo zile za binadamu na hakuna kiumbe
chini ya jua atakayeweza kukuzuia kuupata.
.......................................................................
Kama bado hukuwa umesoma kitabu mashuhuri cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pata nakala yako(softcopy) kwa shilingi elfu 10 tu. Au Hardcopy kwa shilingi elfu 22 Ukiwa Dar es salaam. Mikoani tunatuma kwa sh. elfu 30 katika basi.
SIMU: 0712202244,
WASAPP: 0765553030
.......................................................................
Kama bado hukuwa umesoma kitabu mashuhuri cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pata nakala yako(softcopy) kwa shilingi elfu 10 tu. Au Hardcopy kwa shilingi elfu 22 Ukiwa Dar es salaam. Mikoani tunatuma kwa sh. elfu 30 katika basi.
SIMU: 0712202244,
WASAPP: 0765553030
0 Response to "KUWA BILIONEA NAWEZA KUTUMIA NJIA ZIPI?"
Post a Comment