Baadae katika maisha nilipokuja kuwa nimewachunguza
maelfu ya watu niligundua kwamba, MAWAZO MENGI HUFA KABLA HAYAJAZALIWA NA
HUHITAJI PUMZI YA UHAI KUPULIZIWA NDANI YAKE KUPITIA MIPAGO KAMILI YA VITENDO
VYA HARAKA: Muda wa kulilea wazo upo wakati ule wazo hilo linapozaliwa. Kila
dakika linayoishi lipatie fursa nzuri ya kupona. Hofu ya lawama ipo chini ya
maangamizi ya mawazo mengi ambayo kamwe hayawezi kufikia hatua ya mipango na vitendo.
Watu wengi wanaamini kwamba mafanikio ya mali
ni matokeo ya bahati. Kuna dalili ya
msingi kwa imani hii, lakini wale wanaotegemea moja kwa moja kwenye bahati
karibu mara zote hukatishwa tamaa kwasababu hawatilii maanani kigezo kingine
muhimu ambacho ni lazima kiwepo kabla mtu hajawa na uhakika wa mafanikio. Ni
ujuzi ambao kupitia huo ndipo bahati inaweza kupatikana.
Chunguza watu 100 utakaokutana nao, waulize
ni kitu gani wanachopendelea zaidi katika maisha na 98 kati yao hawataweza
kukuambia. Ikiwa utawabana wakupe jibu, baadhi yao watasema, ulinzi, wengi
watasema ni pesa, wachache watasema furaha, na wengine watasema umaarufu na nguvu na bado wengine watasema kukubalika
kijamii, urahisi wa maisha, uwezo wa kuimba,
kucheza au kuandika, lakini hakuna hata mmoja kati yao atakayeweza kuelezea vitu hivi au hata ishara
kidogo ya mpango ambao wanategemea kufikia haya matamanio yasiyokuwa wazi.
Matajiri hawashawishiwi na matamanio,
wanashawishika tu na mipango kamili inayosaidiwa na shauku kamili, kupitia
msimamo thabiti.
Jinsi
ya Kukuza Msimamo.
Kuna hatua rahisi nne zinazosababisha tabia
ya uvumilivu. Hazihitaji kiasi kikubwa cha akili, wala kiwango fulani cha elimu
na lakini huhitaji muda au nguvu kidogo. Hatua hizo muhimu ni;
1. LENGO
DHAHIRI LIKISAIDIWA NA SHAUKU KUBWA KWA AJILI YA KULITIMIZA
2. MPANGO
KAMILI ULIOELEZWA KATIKA WAKATI ULIOPO
3. AKILI
ILIYOFUNGWA KABISA DHIDI YA VISHAWISHI VYOTE HASI NA VYENYE KUKATISHA TAMAA,
ukiwemo ushauri hasi wa ndugu, marafiki na jamaa.
4. USHIRIKIANO
WA KIRAFIKI NA MTU MMOJA AU ZAIDI AMBAYE ATAKUTIA MOYO KUFUATA MPAKA MWISHO
VITU VYOTE VIWILI MPANGO NA LENGO
Hatua hizi nne ni muhimu kwa mafanikio katika
nyanja zote za maisha. Lengo zima la kanuni 13 za falsafa hii ni kukuwezesha
kuchukua hatua hizi nne kama suala la tabia.
Ni
hatua ambazo waweza kudhibiti hatima yako kiuchumi.
Ni
hatua zinazoleta uhuru na kujitegemea kifikra.
Ni
hatua zinazoleta utajiri katika kiasi kikubwa au kidogo
Ni
hatua zinazoongoza njia ya kuelekea madaraka, umaarufu na kutambulika kidunia.
Ni
hatua zinazohakikisha bahati.
Ni
hatua zinazobadilisha ndoto kuwa katika kitu halisi.
Ni
hatua ambazo husababisha pia katika kuishinda hofu, kukata tamaa na kutokujali.
Kuna malipo mazuri kabisa kwa wale wote
wanaochukua hizi hatua nne. Ni upendeleo wa kuandika tiketi yako mwenyewe na ya
kufanya maisha kutoa zawadi yeyote inayoombwa. Ni nguvu gani ya siri hutoa kwa
watu wenye msimamo, uwezo wa kukabiliana na magumu?
Ubora wa msimamo hutengeneza katika akili
yako aina fulani ya shughuli za kiroho, kiakili, au kikemikali ambazo hukupa
uwezo wa kuzifikia nguvu za kiungu? Uwezo usiokuwa wa kawaida hujitupa wenyewe
katika upande wa mtu ambaye bado anapambana baada ya kushindwa vita, huku dunia
nzima ikiwa kinyume naye?
Maswali haya na mengine yanayofanana nayo
yanaibuka katika akili yangu kama nilivyowachunguza watu kama kina Henry Ford,
ambao walianza tokea mwanzoni na kujenga himaya kubwa ya kiviwanda wakiwa
hawana chochote kingine njiani walipoanza zaidi ya msimamo. Au Thomas A. Edison
ambaye kwa elimu ya chini ya miezi 3 alikuwa mgunduzi aliyeongoza
duniani na kubadilisha msimamo kuwa mashine inayozungumza, mashine ya picha
zinazotembea pamoja na taa ya balbu, achilia mbali mamia mengine ya uvumbuzi
ulio na manufaa alioufanya.
Nilikuwa na upendeleo wenye furaha wa
kuwachunguza wote awili, Bwana Edison na Bwana Ford mwaka hadi mwaka kwa
kipindi kirefu, na fursa ya kuwachunguza kwa karibu. Kwahiyo nazugumza kutokana
na uzoefu halisi wakati ninaposema kwamba sikupata sifa mbadala ya msimamo kati
yao wote wawili ambayo hata kwa mbali ilichangia chanzo kikubwa cha mafanikio yao
ya kushangaza.
Kama mtu anafanya uchunguzi usiokuwa na
upendeleo juu ya watu hawa waliofanikiwa ataishia katika hitimiisho
lisiloepukika kwamba, msimamo, msisitizo wa juhudi na ukamilifu wa lengo ndio
vyanzo vikubwa vya mafanikio yao.
MWISHO WA SURA YA 9
0 Response to "MAWAZO MENGI HUFA KABLA HAYAJAZALIWA, KUPONA YANAHITAJI MIPAGO NA VITENDO "
Post a Comment