Katika safu yetu ya vitabu vya mafanikio 300 vilivyowahi kusomwa zaidi duniani nakala maelfu kwa
melfu, leo tutakitazama kitabu kimoja kilichoandikwa na mwandishi Stefan Aarnio kiitwacho THE FIVE MILLION DOLLAR
BOOK(Kitabu cha dola milioni tano). Kitabu hiki kinazungumzia jinsi ambavyo mtu
unaweza ukatumia WATU, FEDHA na FURSA(dili) katika kufanikisha biashara ya
ardhi na majengo(real estate wealth) hata kama hauna kitu chochote kile
mifukoni.
Stefan anasema anawashangaa sana wawekezaji katika ardhi
& majengo wanaochipukia wanavyozitumia fedha zao. Mara nyingi wawekezaji
hao vijana ni wenye umri kati ya miaka 30 na 40 waliochoshwa na ajira zao
lakini wanaotengeneza kipato cha wastani kilekile kisichobadilika.
Kwa kuwa wanakuwa na ajira ya uhakika watu hawa wana
uwezo wa kupata mikopo kwa urahisi kutoka mabenki na taasisi mbalimbali za
kifedha kwa ajili ya kukamilisha shughuli yeyote ile ya kiuchumi. Wawekezaji
hawa wanakuwa wamekwisha choka na ajira za kukimbizana(rat race) na wako tayari
kujiingiza katika biashara za uwekezaji katika majengo na ardhi kwa kutumia
fedha zao wenyewe.
Kitu cha kusikitisha ni kwamba, aina hii ya wawekezaji
wapya wamekuwa kwenye ajira tangia wakiwa na umri wa miaka 18 mpaka kufikia
hatua hii kifedha na sasa wapo katika miaka yao ya 30 wakiwa tayari kuanza uwekezaji. Wawekezaji
hawa wamezowea kufanya vitu kwa njia ya polepole ilioyowachukua miongo kadhaa
kufikia pale walipo sasa kiuchumi. Muda ndiyo fedha ya kweli pekee maishani na
ili kufanya mambo haraka, ni sharti tukubali kuelimika. Elimu ndipo mahali
utajiri wote hutokea kwa sababu utajiri wote chanzo chake ni akili.
Haijalishi tumejiandaa kiasi gani au tulianza na kiasi
gani cha fedha, ukweli wa mambo ni kwamba katika biashara au uwekezaji kwenye
ardhi na majengo(real estate) mara nyingi tunaishiwa fedha njiani. Bila kujali
ni kiasi gani cha fedha au mkopo tuliokuwa nacho mara nyingi kiasi hicho
hufungwa kwenye mradi na mwishowe tunajikuta fedha zimekatika. Hili humtokea
kila mwekezaji, uwe Donald Trump au Warren Buffet. Mara nyingi kuna hatua
ambayo mwekezaji ni lazima atoke aende kutafuta mtaji wa kuendelea kuwekeza.
Stefan anaendelea kusema kwamba alianza kuwekeza akiwa na umri wa miaka 22 na faida kubwa zaidi aliyoipata
kwa kuwekeza akiwa na umri mdogo kiasi hicho ni kwamba hakuwa kabisa na fedha
taslimu, wala mkopo, wala kuaminika alipoanza. Ilimbidi ajifunze kupata fedha,
kusimamia kiasi chake kidogo cha mkopo na kuongeza zaidi kuaminika kwake.
Ilimbidi ajifunze mbinu za kucheza mchezo wa “FEDHA, WATU na FURSA” pasipokuwa
na fedha taslimu mfukoni tangia siku ya kwanza kabisa kwa kuwa alianza biashara
akiwa hana kitu.
Alikuwa kijana ‘mtundu’ aliyepata semina ya uwekezaji
kwenye ardhi na majengo yenye thamani ya dolla elfu mbili na kutaka kuifanya
ndoto yake kuwa kweli. Anasema shughuli zile za uwekezaji hazikunza mara moja
mpaka kwanza alipojifunza sheria za kutengeneza madili(fursa) na kutafuta fedha
za mtaji.
Sheria hizi zilimwezesha kutafuta fedha/mtaji kwa ajili
ya fursa/mikataba(deals) zake zote isipokuwa mktaba wa kwanza peke yake ambao
aliwekeza kiasi kidogo cha fedha kama dola 1200 hivi. Kwasababu alifahamu
misingi ya FEDHA, WATU NA FURSA, hajawahi tena kutoa fedha zake mfukoni kununulia biashara au ardhi na majengo
tokea hapo.
Wawekezaji wengi hudhani kwamba ‘fedha ni mfalme’ na
huogopa kutafuta fedha kwa ajili ya mikataba(deals). Ukweli wa mambo ni kwamba
fedha ni ‘takataka’, kila mtu anazo na ni bidhaa rahisi isiyokuwa na thamani
kama utaitumia pasipo akili. Fedh ni kigeugeu na ni rahisi kupatikana ikiwa
tutaelewa kanuni chache muhimu za pesa.
SEHEMU KUU 3 UNAPOTAKA KUFANYA MKATABA(DEAL)
Kuna sehemu kuu 3 wakati unapotaka kuweka sawa mpango wa
kupata fedha unazohitaji nazo ni hizi hapa;
1.FEDHA=Fedha zinahitajika kuanzishia biashara au
kununulia nyumba/ardhi
2. WATU=Timu itakayoendesha biashara au kusimamia
rasilimali
3. FURSA/MPANGO/BIASHARA(DILI)= Ni biashara au asseti
yenyewe
Wawekezaji wengi wachanga hwaelewi hizi sehemu za msingi
tatu katika uwekezaji kwenye ardhi na majengo na hupoteza muda mwingi
wakijaribu kutafuta pesa kupitia njia zisizokuwa sahihi. Kwa kufanya hivyo
huharibu kuaminika kwao na kuonekana kama wajinga katika mitandao ya wawekezaji
wakubwa.
NI VITU 3 MUHIMU UNAPOANZISHA BIASHARA YA AINA YEYOTE ILE
IKIWEMO HII YA ARDHI NA MAJENGO
Uimuuliza mtu yeyote swali hili atakujibu mara moja kuwa
jibu ni PESA. Ni kweli asilimia 100% kuwa pesa zinahitajika unapotaka kuanzisha
biashara eyote ile hata iwe ni ya kuuza juisi stendi au ya kujenga magorofa.
Lakini Stefan anaposema alianzisha bishara yake bila kuwa na pesa anamaanisha
kwamba alianzisha biashara yake kwa kutumia fedha za watu wengine(wawekezaji).
Pesa peke yake miongoni mwa viungo vingine 2 haina maana
ikiwa hakuna sehemu nyingine 2, WATU na BIASHARA/FURSA(Deal). Pesa zipo nyingi
kila mahali na zina tabia ya kutafuta mahali salama zinapoweza kuwekezwa ili
zizae.
Kiungo cha pili ambacho ni WATU au TIMU ndicho
kitakachoendesha na kusimamia biashara na huhusisha usimamizi na utaalamu wa
kiufundi wa biashara.
Kiungo cha tatu kinachohitajika ili biashara iweze kuanza
ni FURSA(DILI), unaweza pia ukakiita MPANGO au BIASHARA yenyewe. Dili laweza
kuwa ni biashra ya majengo na ardhi au hata biashara tu ya kawaida lakini ile
inayoweza kuleta faida. Lakini katika kitabu hiki cha THE 5 MILLION DOLLAR BOOK
kimezungumzia zaidi biashara ya ardhi na majengo(Real Estate). Dili ndiyo
kiungo muhimu zaidi katika biashara kwani ndicho huvutia viungo vingine vya
Pesa na Watu.
Mjasiriamali mwenye uwezo wa kuviunganisha viungo hivi
vyote 3 kwa weledi ndiye hufanikiwa na kupata faida kubwa katika biashara yeyote
ile ikiwemo biashara ya ardhi na majengo hata kama hana fedha kabisa mfukoni
huku pia akiwafanya wafadhili wake au wawekezaji aliowatumia pia kupata faida
kubwa.
Ukiweza kumiliki viungo 2 peke yake kati ya 3 ni rahisi
kupata kiungo cha 3 lakini ikiwa utamiliki kiungo kimoja tu peke yake itakuwa
vigumu sana kuweza kuvutia viungo vingine 2 na hivyo hutaweza kufanikiwa.
Hiyo ni sehemu tu ya kitabu hicho, The Five Million
Dollar Book” ambacho mwndishi wake Stefan Aarnio ameeleza hatua kwa hatua jinsi
yeye mwenyewe binafsi alivyoweza kumiliki utajiri mkubwa kupitia biashara ya
ardhi na majengo akiwa hana hata senti tano mfukoni. Ukikisoma kitabu hicho
chote unaweza kuanza mra moja biashara hii ya majengo hata ikiwa huna mtaji wa
fedha.
……………………………………….
Mpendwa
msomaji zile semina na masomo yahusuyo fedha na michanganuo ya biashara ndani
ya Group la whatsapp la MICHANGANUO ONLINE bado zinendelea kila siku usiku saa
3 kwa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu. Pia unapata offa ya masomo na semina
zilizopita, vitabu na michanganuo mbalimbali ikiwemo ya kuku. Lipi kupitia
namba 0712202244 au 0765553030 kisha utume anuani yako ya email na ujumbe wa “NIUNGANISHE
NA GROUP LA MICHANGANUO”
Somo
la leo kwenye Group litakuwa na kichwa cha habari kinachosema; KWANINI NI
HATARI KUKOPA AU KUWAKOPESHA NDUGU NA JAMAA WA KARIBU?
0765502844
ReplyDelete