Wajasiriamali tumezoea dhana kwamba Mpango wa
biashara ni kitu kinachohitajika tu pale tunapokwenda katika taasisi za fedha
au benki kuomba mikopo kwa ajili ya kuendelezea biashara zetu. Lakini kitaalamu
mpango wa biashara ni zaidi ya hivyo.
Mpango wa biashara au mchanganuo wa biashara
kama wengi tulivyozoea kuuita ni muhimu sana katika suala zima la usimamizi wa
biashara unayokusudia katika kupanga malengo yaliyokuwa wazi ya kampuni au
biashara yako na kuelezea kikamilifu jinsi utakavyoyafikia malengo hayo.
Mchanganuo wa biashara siyo tukio la mara
moja bali ni andiko linaloweza kupitiwa mara kwa mara na kufanyiwa marekebisho
kila wakati inapohitajika kulingana na mabadiliko nayo yanavyotokea katika
biashara. Biashara inafanana na kitu kinachoishi, hubadilika, kukua na hata
wakati mwingine hufa. Ni njia bora kabisa ya kuelezea ni wapi biashara yako
inakoelekea.
Katika uandaaji wa mchanganuo wako wa
biashara yapo maeneo ambayo yanatakiwa kupewa umuhimu wa kipekee ili kuweza
kuunganisha sehemu nyingine zote za mpango huo na kuleta maana au uhalisia
unaotarajiwa. Maeneo hayo ni haya yafuatayo;
1. UTAFITI
Tenga muda wa kutosha kufanya utafiti wa kina
kuihusu biashara yako kufahamu mambo
mbalimbali(facts) ili mwisho wa siku utakapokuja kuziunganisha sehemu zote na
sura za mchanganuo wako ziweze kuleta mantiki.
2. DHANA/MAKISIO(ASSUMPTIONS)
Tengeneza makisio ya kina(detailed
assumptions). Msingi mkubwa wa mpango wa biashara wowote ule uliokuwa mzuri
unasimama juu ya dhana imara ambazo zitakuwezesha kufanya makisio yako kwa
usahihi. Makisio au dhana hizo ni sawa na dira inayokuongoza katika kujua
matokeo ya wakati ujao au kukuwezesha ‘kuigiza’ vile biashara yako itakavyokuwa
hapo baadae.
Mjasiriamali unapotengeneza makisio/dhana
zako unatakiwa kufanya hivyo ukizingatia vitu muhimu vitatu ambavyo ni;
1. Mauzo
2. Gharama
zinazobadilika
3. Gharama
zisizobadilika(za kudumu)
Katika vitu hivyo vitatu unatakiwa uonyeshe
ni kwanini vimekuwa kama vilivyo, kwa mfano dhana kwenye mauzo yako unaweza
ukaonyesha miezi fulani ni makubwa pengine kutokana na kwamba ni msimu wa
mavuno au sikukuu nk. Pia dhana katika gharama unaweza ukakisia ni asilimia
fulani ya mauzo kulingana na utafiti wako ulivyoufanya, uzoefu na hesabu za
kipindi cha nyuma au biashara nyingine zinavyofanya kwenye sekta hiyo.
Unapoweza kuunganisha na kuhusianisha vyema
dhana zako na malengo yako itakusaidia pia katika kuweka mikakati mahsusi ya
masoko na kubaini ni rasilimali kiasi gani zinazohitajika ili kutimiza malengo ya
biashara hiyo uliyojiwekea. Kila kitu katika mchanganuo wako wa biashara
kinatakiwa kufungamana pamoja na kuhusiana.
3. MAHITAJI
YA KUANZIA(KIANZIO)
Eneo hili ni nyeti sana wakati wa maandalizi
ya mchanganuo wa biashara yeyote ile. Haitoshi tu kusema kwamba, tunahitaji
shilingi 20,000,000 bali ni muhimu pia kuelezea kwa undani hiyo milioni
ishirini itatumika kwa ajili ya vitu gani, onyesha gharama mbalimbali za kuanzia kama vifaa, gharama za awali, eneo,
mtaji wa kazi, jumla yake ni kiasi gani. Hii itamfanya msomaji wa mchanganuo
wako kuona kweli ulifanya utafiti wa kutosha. Onyesha pia na chanzo cha
mahitaji hayo ni nini(Mtaji ulikoutoa)
4. TAARIFA
REJEA.
Taarifa rejea au vyanzo ulivyotoa taarifa za
kutengeneza mchanganuo wako kwa mfano, upembuzi yakinifu, utafiti wa soko,
taarifa za washindani wako na taarifa juu ya sekta uliyopo. Hii ni kama vile
ushahidi wa kutia nguvu kile unachokieleza katika mchanganuo wako. Msomaji anategemea
kuona alama(tanbihi) inayoelekeza chanzo cha maelezo yako.
Toa maelezo mafupi na yenye kueleweka kwa urahisi
kwani wadau wengi mfano wakiwemo watu wa mabenki hawapendi maelezo marefu sana
yasiyokuwa na tija, wanachotaka ni ukweli(facts) tu.
5. USIMAMIZI
WA RASILIMALI WATU
Eneo hili ni wajasiriamali wengi hawalipi
uzito unaostahili wanapoandika michangauo ya biashara zao, wakati ukweli ni
kipengele muhimu sana ambacho ndicho kilichokuwa na changamoto kubwa zaidi kwa
mjasiriamali wa leo hasa unapoajiri wafanyakazi katika soko la ajira
lisilotabirika. Ni lazima uonyeshe kwa usahihi ni kwa jinsi gani utavutia
wafanyakazi walio na ujuzi
watakaohudumia biashara yako.
Unatakiwa pia uonyeshe mchoro wa mfumo wa
utawala pamoja na mahitaji ya rasilimaliwatu kama vile mikakati ya kuajiri
wafanyakazi wa kudumu au vibarua wa muda mfupi.
6. OMBA
USAIDIZI KUTOKA NJE.
Ni jambo la busara kuandaa mwenyewe mpango wa
biashara yako kwa kuwa ni wewe mwenyewe ndiye unayeijua biashara yako vyema
kuliko mtu mwingine yeyote yule, lakini unashauriwa hata kama umeandaa mwenyewe
baada ya kumaliza kuandika basi umtafute mtu unayemuamini atakayekusaidia
kuupitia mchanganuo huo ili kama kuna makosa au udhaifi mwingine wowote ule akushauri
kuurekebisha au kuboresha.
…………………………………………….
Mpenzi
msomaji wa makala hizi, napenda kukujulisha pia kwamba katika GROUP letu la
WHATSAP la MICHANGANUO ONLINE, masomo ya kila siku usiku saa 3 yanayohusiana na
Michanganuo
na Mzunguko wa fedha bado yanaendelea kama kawaida na kuelekea nusu
ya pili ya mwaka huu tunatarajia kuwa na semina kabambe za kuandika hatua kwa
hatua michanganuo ya zile biashara zenye fursa kubwa ya kuleta faida haraka.
Leo
hii tarehe 22 July ndani ya Group tutakuwa na somo la pesa lisemalo, “SEHEMU 6
SALAMA ZAIDI ZA KUTUNZIA FEDHA ZAKO, JE CHINI YA GODORO NA VIBUBU NAZO ZIPO?”
Karibu
usikose somo hili na kila siku kwa masomo mengine mazuri yatakayokupa uelewa
mpana zaidi wa pesa. Kiingilio ni shilingi elfu 10 tu kwa muda wote na
tunakutumia offa ya vitu mbalimbali vikiwemo vitabu maarufu 2 vya michanganuo
kwa kiingereza na Kiswahili pamoja na semina zilizopita na michanganuo kamili
mbalimbali. Ukitaka kulipia unaweza kutuma pesa moja kwa moja katika moja ya
namba hizo hapo chini au
Tuwasiliane
kwa,
SIMU:
0712202244
WATSAP:
0765553030
Peter
Augustino Tarimo
0 Response to "JINSI YA KUANDAA MCHANGANUO WA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, MAENEO 6 MUHIMU YA KUZINGATIA"
Post a Comment