Ni jambo la kutia moyo sana siku hizi kuona
idadi ya wanawake wanaoingia kwenye ujasiriamali au kuanzisha biashara zao ikiongezeka
kwa kwa kasi ya kuridhisha. Na ongezeko hilo la wanawake wajasiriamali
halionekani hapa Tanzania tu bali Afrika Mashariki nzima na Dunia kwa ujumla.
Lakini hata hivyo mwelekeo huu wa
kutia moyo kusema ukweli haumaanishi kwamba ndio wanawake na wanaume sasa wana
uwanja uliokuwa sawia kwa asilimia mia moja kwenye sekta ya ujasiriamali. Bado
zipo changamoto mahsusi zinazoendelea kuwakwaza wanawake kwasababu tu wao ni
wanawake. Bila ya kupoteza muda mwingi hebu moja kwa moja tuzione hizo
changamoto;
1.VIKWAZO
KATIKA KUVIFIKIA VYOMBO VINAVYOTOA MIKOPO NA MITAJI
Mfumo dume uliokita mizizi karibu
katika kila sekta ya maisha kwenye jamii, sekta ya fedha nayo haijasalimika.
Taasisi nyingi za kifedha au zile zinazokopesha wajasiriamali wadogo na wakubwa
zimetawaliwa kwa kiasi kikubwa na wanaume ambao ndio watoaji maamuzi muhimu. Na
kwa bahati mbaya sana wanaume hao wengi hawako tayari kabisa kuwaona wanawake wakipata
fursa sawa na wao.
Matokeo yake wanawake hujikuta
katika nyakati ngumu wanapogundua kwamba hawapewi umuhimu unaostahili pale
wanapokwenda kutafuta au kuomba mikopo kwa ajili ya kukuzia biashara zao.
Wanawke wanajikuta wakiendelea kufanya ujasiriamali na mtaji mdogo waliokuwa
nao jambo linalowazuia wasione mafanikio ya haraka kama ilivyo kwa wenzao
wanaume. Namna ya kukuza mtaji imekuwa ni changamoto ya kwanza mjasiriamali
mwanamke anayokutana nayo wakati akifikiria jinsi ya kuwa mjasiriamali.
2.UNYANYASWAJI
KIJINSIA.
Changamoto hii ndiyo iliyokuwa
ikipewa kipaumbele kikubwa zaidi na vyombo mbalimbli vya habari kote duniani
hasa hasa katika zile nchi zilizoendelea kiasi cha kufikia hatua ya watu wengi
maarufu kama wasanii na waigizaji wa sinema wakubwa kule Hollywood Marekani
wakajikuta wakiwajibika kwa vitendo vyao vya ukatili wa kijinsia walivyokuwa
wamezowea kuwafanyia mabinti wanaokwenda katika kiwanda hicho cha filamu
Hollywood kusaka umaarufu.
Hizo ni habari njema hata hapa
Tanzania tunapaswa kuiga mfano. Unyanyasaji wa kijinsia upo karibu katika kila
sekta kuanzia sekta za burudani, siasa, media, fedha nk. na wanawake mara zote
ndio ambao wamekuwa wahanga wa ukandamizaji huo. Unyanyasaji wa kijinsia una
sura nyingi kuanzia unyanyasaji kwa kutumia maneno kama vile matusi na maneno
ya kuvunja moyo, kunyimwa fursa, vipigo na hata kulazimishwa kufanya vitendo
vya mapenzi bila ridhaa ya mwanamke mwenyewe.
3.UWIANO
BAINA YA BIASHARA NA FAMILIA
Siyo wanawake wajasiriamali tu
peke yao wanaokumbana na changamoto hii bali hata na wale wanawake walioko
kwenye ajira pia na wao hili huwasumbua sana. Kubalansi muda wa kulea watoto na
familia wakati huohuo wakihakikisha biashara au kazi inaendelea vizuri ni
mtihani mkubwa na kwa mwanamke hili huwa gumu zaidi kutokana na sababu kwamba
jamii hasa zile za Kiafrika zimejijengea kasumba kwamba kazi za kulea familia
ni spesho tu kwa mwanamke. Waswahili husema mshika mawili moja humponyoka,
mwanamke inabidi achague kwa wakati ule aliopo ni kipi muhimu zaidi ya kingine,
kwa mfano ana mtoto mchanga itambidi kwanza biashara aiweke pembeni au amtafute
mlezi.
4.KUKOSA
UUNGWAJI MKONO
Hii hasahasa ni kwa wanawake wale
walioko katika nafasi za juu kama mameneja, viongozi nk. wakati mwingine
hujikuta wapweke sana kwani ni vigumu zaidi kwao kupata wanawake wenzao wa
kuiga mfano(mentors) kutokana na idadi ya wanawake waliokuwa juu kuwashinda wao
kuwa ndogo mno nah ii imetokana na sekta nyingi nafasi za juu kutawaliwa n
wanaume ambao kama kawaida yao wengi hawapendi kuwaona wanawake wakiwa katika
nafasi za maamuzi kama wao au juu kuwashinda.
Angalau siku hizi wanawake kidogo
kidogo wanaanza kutapa nafuu kutokana na ujio wa mitandao ya kijamii ambapo
wanawake wenyewe wanakuwa na uwezo wa kuwasiliana na wanawake wenzao hata
walioko mbali kutiana moyo ili waweze kusonga mbele zaidi ikiwa ni pamoja pia
na kujenga mitandao ya kibiashara.
………………………………………………………
· Kwa vitabu bora kabisa vya ujasiriamali
tembelea; SMART BOOKS TZ.
· Kwa hudumazetu mbalimbali ikiwemo
kuandikiwa mpango wa biashara yako nk. fungua, HUDUMA ZETU.
· Kwa michanganuo maarufu 3 ya kuku aina
zote(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) Lipia shilingi elfu 10 kupitia namba ya simu,
0712202244 utumiwe katika email yako muda huohuo. Kwa mawasiliano zaidi unaweza
kuwasiliana nasi kwa njia ya WHATSAP namba, 0765553030
0 Response to "KILA MWANAMKE MJASIRIAMALI HUKUTANA NA CHANGAMOTO HIZI KUBWA 4 KWENYE SAFARI YAKE"
Post a Comment