Unaweza ukafikiria labda elimu na vitabu vya mafanikio binafsi, Self Help
books ni jambo la juzijuzi tu, lakini kumbe hapana siyo hivyo. Hebu fikiria
mwaka 1969 Aliyekuja kuwa Rais wa Afrika ya kusini isiyokuwa na ubaguzi wa
rangi Hayati Nelson Mandela alimwandikia mkewe Winnie Madikizela Mandela barua
ifuatayo(orijino ipo chini yake) wakati akiwa kifungoni katika gereza la kisiwa
cha Robben Island.
Juu ni sehemu ya barua Nelson Mandela aliyomwandikia mkewe
Winnie kumpa pole kwa ugonjwa wakati alipokuwa gerezani Robben Island
Juu ni barua
hiyo original.
|
Katika barua hiyo Mandela alikuwa akimpa mkewe pole
kutokana na tatizo la kuzimia mara kwa mara lililokuwa likimsumbua, tatizo hili
lilikuwa likisababishwa na tatizo jingine la moyo ambalo Mandela katika barua anasema alikuwa anafahamu kuwa Winnie alikuwa
nalo. Hata hivyo Mandela akashukuru kwamba Daktari wa familia alikuwa
akilishughulikia tatizo hilo kwa karibu na kwamba tatizo tayari lilikuwa
limeshapatiwa ufumbuzi. Mandela aliomba aendelee kupewa taarifa za matokeo ya
vipimo kutoka kwa daktari huyo na akamtakia mkewe uponaji wa haraka na kila la
heri katika maisha.
Katika aya iliyofuatia, Mandela alipendekeza kwa mkewe vitabu
2 ambavyo vingemfaa na kumpa tulizo wakati huo mgumu, vitabu alivyopendekeza
mkewe akavisome katika maktaba za manispaa ya mji ni, THE POWER OF POSITIVE THINKING na
THE RESULT OF POSITIVE THINKING, vyote vikiwa vimeandikwa na mwandishi
mwanasaikolojia wa Kimarekani aitwaye Norman Vincent Peale. Alimwambia kuwa yeye
hajaweka umuhimu mkubwa kwenye suala la
dini mwandishi analojadili bali yeye zaidi anazingatia yale maoni mwandishi
aliyozungumzia kuhusiana na masuala ya kimwili na kisaikolojia katika kitabu
hicho.
Mandela akinukuu kutoka katika vitabu hivyo alimsisitizia
Winnie pointi muhimu kwamba, “Tatizo
kubwa halipo katika ulemavu wa mtu bali lipo zaidi katika mtazamo wake kuelekea
ulemavu huo, Mtu anayesema nitapona ugonjwa huu na kuishi maisha ya furaha,
tayari kwa kusema hivyo anakuwa ameshapona nusu yake”
Karibu na mwisho wa barua hiyo, Madiba alimsifia mkewe
kwa kumwambia hivi; “Katika vipaji ulivyokuwa navyo, kinachonivutia zaidi mimi ni ujasiri
wako na kujitambua, Hii hukufanya wewe kuwazidi wengine na mwishowe itakuletea mafanikio makubwa. Endelea kulitunza hili muda wote akilini….”
0 Response to "KUMBE NELSON MANDELA ALIKUWA MPENZI WA VITABU VYA ELIMU YA MAFANIKIO!"
Post a Comment