Biashara ya kukopesha pesa ni moja kati ya
biashara kongwe kabisa duniani, miaka kwa miaka binadamu wamekuwa wakiazimana
pesa kwa malengo mbalimbali tofauti. Hata kabla ya fedha kuvumbuliwa watu
walikuwa wakikopeshana vitu au bidhaa mbalimbali wengine wakichaji riba(chajuu)
na wengine walikopeshana tu hivyohivyo pasipo kudai chochote toka kwa mkopaji,
mkopaji alitakiwa kurejesha kiasi kilekile alichokopa.
Ni miaka ya hivi karibuni tu au tuseme karne
chache zilizopita biashara hii ilikuja kuchukuliwa rasmi na mabenki lakini hata
pamoja na hivyo bado watu mmojammoja na vikundi kama vile vya upatu, saccos na
viccoba wanaendelea na biashara hii. Uzuri wa biashara hii ni kwamba mtu
unaweza ukaingiza kipato pasipo kufanya kazi kubwa sana endapo utaisimamia vizuri.
Biashara za kukopeshana pesa zipo za aina mbili;
· Mikopo
isiyokuwa na riba
· Mikopo
yenye riba
1.Mikopo
isiyokuwa na riba
Katika aina ya kwanza ya mikopo ndiyo
iliyokuwa kongwe zaidi na ipo ya aina nyingi mojawapo ni ile ambayoi hufanyika
zaidi baina ya watu mitaani katika vikundi visivyokuwa rasmi maarufu kama MCHEZO,
michezo ya upatu sifa yake kubwa ni kutokuwa na riba isipokuwa mingine huwa na
faini pale mkopaji anapochelewesha kulipa kwa wakati.
Lengo kubwa la mtu kucheza mchezo ni ili
kuweza kupata mtaji au fedha kwa ajili ya kutimiza lengo fulani na kisha fedha
hizo kuja kuzirejesha taratibu, lakini pia mchezo unamsaidia mtu kujijengea
nidhamu ya utunzaji wa pesa kwani anapokuwa akiwachangia wenzake ni sawa na
kuweka akiba kwa ajili ya matumizi yake ya baadae.
Kwahiyo kimsingi kabisa upatu lengo lake ni
zuri sana na wala halina shaka yeyote isipokuwa madhara yake ambayo ndiyo
tutakayokwenda kuyajadili na kuyafahamu kinagaubaga.
2.Mikopo
yenye riba
Hii ni biashara kama zilivyokuwa biashara
nyingine zozote zile, ila tu bidhaa inayouzwa ni pesa ili ikatumike kutengeneza
fedha zaidi. Biashara ya kukopesha fedha kwa riba hufanywa na makundi
yafuatayo;
1) Watu
binafsi maarufu kama, MIKOPO YA RIBA MITAANI
2) Vikundi
vilivyosajiliwa kama vile SACCOS, VICCOBA nk.
3) Mabenki
na taasisi nyinginezo kubwakubwa za fedha.
Kabla hatujakwenda rasmi kuona NI KWANINI MIKOPO YA RIBA MITAANI, MICHEZO YA UPATU
NA BAADHI YA SACCOS NI HATARI MTU KUJIUNGA, hebu kwanza tuone mikopo
inavyofanya kazi….
……………………………………...........
Mpenzi
msomaji wa makala hizi, makala hii tutajifunza leo Mei 8 2020 katika Group la
MICHANGANUO ONLINE na CHANNEL YA TELEGRAM saa 3 usiku mpaka saa 4 na kiingilio chake ni shilingi elfu
10 tu.
Ukishalipia
tunakutumia masomo na semina zote tulizojifunza tangu mwezi January,
vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara pamoja na kukuunganisha na group hilo.
Utapata pia fursa ya kujifunza semina na masomo mengine yote yajayo kila siku kwa miezi
yote iliyobakia mpaka mwaka huu wa 2020 umalizike tutakapohitimisha programu ya
mwaka mzima. Aidha Semina za michanganuo ya biashara zinazolipa haraka zinaanza tena
wiki hii hatua kwa hatua.
Namba
za malipo ni 0712202244 au 0765553030 na jina hutokea Peter Augustino Tarimo, baada ya kulipia tutumie namba unayotumia
wasap au anuani yako ya email pamoja na kutuma ujumbe wa “NIUNGANISHE NA GROUP
LA MICHANGANUO-ONLINE NA OFFA ZOTE” kwa namba 0765553030
0 Response to "KWANINI MIKOPO YA RIBA MITAANI, MICHEZO YA UPATU NA BAADHI YA VICOBA SI SALAMA KUJIUNGA?"
Post a Comment