Habari
za saa hizi mdau, karibu kwenye somo hili linalohusu mikakati mbalimbali na mbinu
Mjasiriamali anazoweza akazitumia katika kuikwamua biashara yake kipindi kukiwa
na hali ngumu kifedha. Na wala haijalishi unajua jinsi ya kujiwekea akiba,
unapozuka mdororo wa kiuchumi ni lazima uchukue hatua hizi ndogondogo tu
vinginevyo kutajiri utakusikia kwa wenzako.
Mfano
mzuri wa kipindi cha hali ngumu kifedha ilikuwa ni hivi majuzi kwenye lile
janga la UVIKO 19, mambo yalikuwa hayaendi kama ilivyotarajiwa na wengi hivyo
kila mtu akawa ana haha kutafuta mbinu mbalimbali za kuhakikisha anafanikiwa
kujitoa kwenye mkwamo ule kiuchumi
Siri ya kufanikiwa katika kipindi kigumu kiuchumi ni vitu vidogovidogo watu wengi hupuuzia na muda hali inapokuwa ngumu siyo lazima iwe ni nchi nzima inaupitia hapana, bali wafanyabiashara mmojammoja nao kwa nyakati tofauti hukumbwa na vipindi vigumu, biashara zinatoka polepole na mzunguko wa pesa unakuwa mdogo.
Kuna nchi ambazo hali imewahi kuwa mbaya pesa ikaporomoka thamani hadi watoto wakatumwa madukani kununua mkate mmoja tu na lundo la hela kama uonavyo pichani hapo juu
Hali
inapokuwa hivyo mjasiriamali hana budi kutafuta mbinu na mikakati
itakayomuwezesha kujinasua na wimbi hilo hatimaye mtiririko wake wa fedha
kurudi kuwa tena chanya. Mbinu na mikakati hiyo 5 ni hii hapa chini;
1.Wekeza zaidi Kwenye Utafutaji wa
Masoko
Wakati
kipindi kama hicho washindani wako wanahangaika kubana matumizi kila idara
ikiwemo ile idara nyeti ya masoko, wewe tafuta zaidi njia ya kuwekeza kwenye
kutafuta masoko ili usonge mbele na kukamata sehemu kubwa zaidi ya soko na
hivyo fedha zaidi kuingia. Kwani kuwekeza ni nini? Maana yake siyo lazima
uwekeze pesa tu la hasha, uwekezaji unaweza kuwa katika muda ama rasilimali
nyingine pia.
2. Wabaini Wafanyakazi Wasiokuwa na Tija
Kwenye Biashara yako.
Kwa
kawaida katika kipindi kigumu ni rahisi sana kumbaini mfanyakazi yule
asiyekuingizia faida kutokana na sababu kwamba hata gharama unazoingia kumlipa
yeye unaona kabisa mwisho wa siku haziwezi zikarudi. Ikiwa mfanyakazi wako
hakuingizii faida na badala yake wewe ndiyo unaingia gharama kubwa zaidi juu
yake, mpe kwanza onyo na nafasi ya mwisho ya kujirekebisha na endapo
hatajirekebisha usiendelee kumlea mwache aende zake.
3.Anzisha Biashara Nyingine Inayoongeza
thamani zaidi Katika hali ya Soko Iliyopo.
Itakuwa
vizuri zaidi ikiwa huduma au bidhaa hiyo mpya itawalenga wateja walewale
uliokuwa ukiwauzia zamani. Ili uweze kulimiliki soko vizuri zaidi wakati wa
hali ngumu kipesa unaweza ukaamua kuachana na ile biashara inayosuasua ukabakia
tu na ile inayotoka vizuri. Hii ni njia nyepesi ya kutajirika kwa haraka kuliko
kuendelea kubana fedha ukihofia zitapotea.
4. Shikamana zaidi na Wateja wako kwa Kuwapa
Matokeo Bora zaidi na Faida ya Kweli.
Chunguza ni faida zipi wateja wanazozipata kutokana na bidhaa au huduma zako kisha uangalie ni kwa jinsi gani unavyoweza ukaongeza faida hizo. Ni lazima utafakari kwa kina juu ya biashara yako kwani wakati mwingine mdororo wa kiuchumi ni matokeo ya wafanyabiashara na makampuni kujisahau wakaachana na misingi ya biashara na kukumbatia zaidi upande wao, faida, thamani na upanuzi wa biashara zao badala ya kujali faida anayoipata mteja. Jifunze njia ya kuwekeza zaidi kwa mteja kwani ndiyo msingi wa mafanikio makubwa kibiashara..................................................
.........................................
5. Mbinu
moja ya 5 na muhimu sana haijatajwa hapa, unaweza
kuipata kwenye somo kamili unapojiunga
na kundi letu la Michanganuo-online,
mahali ambapo panapatikana masomo ya kipekee kabisa zaidi ya 100
yasiyopatikana kwingine kokote.
Ili kujiunga na group hili ada ya mwaka ni sh.
elfu 10 ambapo unatumiwa muda huohuo offa ya vitabu na michanganuo jumla vitu
14 (cheki orodha pale chini). Ndani
ya group mbali na masomo ya kila siku tunakuwa pia na semina za kuandika
michanganuo ya biashara bunifu zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida haraka.
Baada ya malipo tuma ujumbe usemao; “NATAKA
OFFA MPYA YA VITU 14 NA KUUNGWA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO”
Namba zetu za malipo ni 0712202244 au 0765553030
jina ni Peter Augustino Tarimo
ORODHA
YA VITU 14 VYA OFFA HII HAPA CHINI;
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa Kiswahili
2.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 tu - kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani, hutumika
vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
5.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
6.
COMPILLATION: Masomo 30 ya fedha
usiyoweza kuyapata popote, mengine 70 utayapata kwenye group kila siku - kwa Kiswahili
7.
MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji
Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
8.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa
kiingereza
9.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa Kiswahili
10. MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili
11. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiswahili
13. MCHANGANUO: Kiwanda cha mvinyo na juisi ya Rosella –Choya Investment – kwa kiswahili
14. MCHANGANUO: Kilimo cha Tikiti maji:- Kibada Watermelon Fruits – kwa kiswahili
SOMA NA
HIZI HAPA:
1.Biashara ndogo ya mtaji wa 80,000/= niuze nini kupata faida ya
haraka?
2. Jinsi ya kuweka akiba kila mwezi ukitumia vyanzo vya pesa
usiyotarajia kabisa kuipata
3. Siri ya kufanikiwa biashara ya kuuza vinywaji baridi vyenye
faida
4. Biasharaya kuuza dagaa mchele na samaki wa maji chumvi
kiubunifu: mchanganuo
0 Response to "MBINU NA MIKAKATI YA KUIKWAMUA BIASHARA YAKO KATIKA HALI NGUMU KIPESA ILI KUFANIKIWA"
Post a Comment