Vile vile mtu nayefanya kazi(mwajiriwa) na yule
aliyejiajiri mwenyewe kupitia biashara ni watu wawili tofauti kabisa na ujumbe
au ushauri unaoweza kumpatia mmoja kati ya hao huwezi ukautumia ujumbe huohuo
kumpatia mwenzake, hautaweza kumsaidia. Nasema hivi kwasababu sisi tunaoandika
makala hizi za ujasiriamali kuwaelimisha watu mbalimbali, huwa wakati mwingine
tunafanya makosa pale tunapodhani kwamba wasomaji wetu au hadhira
inayotufuatilia ina mahitaji yanayofanana.
Mfano niliwahi kuandika makala moja katika group la
whatsapp isemayo, “KUKOPESHA SIYO KWA AJILI YA BIASHARA NDOGO NDOGO BALI
BIASHARA KUBWA” nikiwa namaanisha kwamba biashara ndogo inapojiendesha kwa
kukopesha wateja huwa haikawii kufa kutokana na mzunguko wake wa pesa kuwa
mdogo, lakini kwa biashara kubwakubwa kukopesha wateja ndiyo tabia yake kubwa
na watu huweza kukaa na deni hata mwezi, miezi miwili nk. ndipo huja kulipa.
Katika kitabu pia nilichoandika kiitwacho, MIFEREJI 7 YA
PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA, nilieleza kwamba Mifereji ya pesa ni
kile kipato mtu unachopata nje ya shughuli zako za msingi. Shughuli ya msingi
hapa ni kama vile ajira au biashara uliyokuwa umeshaianzisha siku nyingi na inakuletea
tayari mapato. Kwa hiyo huwezi ukasema unaanzisha mfereji wa pesa wakati huna
bado shughuli iliyokwishaanza kuonyesha mafanikio, hapa ndipo unapata pointi
yangu kwamba, “Mifereji ya pesa ni kwa ajili ya wale waliofanikiwa na wajasiriamali
wadogo kabisa ambao ndio wanaanza wanapoteza muda wao bure kujaribu kuanzisha
mifereji mingi ya kipato”, nilikuwa namaana hiyo.
Pia ukurasa wa pili wa kitabu hicho nikaaandika tena
hivi, “Watu matajiri kanuni hii wao huitumia vizuri zaidi na huwa inawasaidia
kuliko masikini, hebu fikiria ni tajiri gani chini ya jua anayemiliki kamradi
kamoja?” Ikiwa hauna biashara ya msingi au kazi ambayo tayari
inakuingizia kipato, wewe mifereji ya kipato siyo ya kuhangaika nayo
itakupotezea muda, nguvu na malengo yako bure, ni bora ukatafuta kwanza kazi au
biashara moja, ukaweka nguvu zako zote pale mpaka itakapoanza kuleta mafanikio
ndipo ufikirie kuanzisha kitu kingine.
Ninachotaka uelewe hapa ndugu msomaji siyo kingine bali, “UMUHIMU WA LENGO(FOCUS)
KATIKA KUFANIKISHA KWANZA JAMBO LOLOTE LILE KWA UFANISI MKUBWA KABLA
HUJAHANGAIKA NA MAMBO MENGINE YANAYOWEZA KUKUTOA KWENYE LENGO LAKO KUU
Ndio maana pale mwanzoni nikaanza kwa kusema kwamba, siyo
kila mtu atahitaji ushauri unaofanana na wa mwenzake na biashara inapokuwa bado
ni ndogo inahitaji mtu kuwa na malengo machache utakayoweza kuyafanyia kazi barabara kuliko
kuwa na utitiri wa malengo(vipaumbele vingi) ambayo hatimaye vitakufanya
utawanye nguvu na rasilimali chache ulizokuwa nazo na kisha kushindwa
kufanikisha hata lengo moja kati ya hayo mengi.
SOMA: Salamu zangu mwaka 2018
Bila shaka unaona matajiri au watu waliofanikiwa kimaisha
wakiwa na miradi mingi(Mifereji ya pesa). Usifikiri eti walipoanza walikuwa
hivyo hapana, walielekeza kwanza nguvu katika mradi au shughuli moja tu mpaka
walipohakikisha imezaa matunda yanayoonekana ndipo sasa wakaanzisha mifereji
mingine ya kuwaingizia kipato. Watu wengi wanaoanza biashara hufanya sana kosa
hili la kudhani kwamba wanaweza wakaanzisha mifereji ya kipato kabla biashara
ya msingi haijatengemaa vya kutosha.
Hali ndivyo ilivyo pia kwa wale walioajiriwa , kama
unafanya kazi mahali inakubidi unapoanzisha mfereji wako wa kipato
basi(biashara ya pembeni) basi uhakikishe unachukua tahadhari kubwa sana, muda
wa kuifanya biashara hiyo usije ukaingiliana na muda wako wa kazi ya msingi
kwani utajikuta napo unatawanya nguvu kama tulivyoona kwenye biashara na
matokeo yake ni kuharibika kwa vyote viwili, kazi na mfereji ulioanzisha.
Kumbuka unahitaji
nguvu nyingi sana na shabaha ili uweze kufanikiwa katika jambo moja,
unadhani basi utaweza kufanikiwa kirahisi katika mambo mengi kwa nguvu hiyohiyo
moja uliyokuwa nayo?
Watu wengi hulalamika na kusema kuwa kanuni ya mifereji
ya pesa haitekelezeki kirahisi, lakini huwa nawaambia kwamba kanuni hii ili
iweze kutekelezeka vizuri mtu unapaswa kwanza uwe tayari una kazi/biashara
inayokuingizia fedha zitakazokuwezesha kusapoti hiyo mifereji mipya
itakayoanzishwa pamoja na kukuwezesha wewe menyewe kuishi vinginevyo ukiwa
unafikiria leo utakula nini hata mawazo ya hiyo mifereji yenyewe ya pesa sijui
kama yataibuka akilini.
HITIMISHO
Elekeza kwanza nguvu zako zote na malengo kwenye eneo au
shughuli ile inayokupatia fedha, acha mambo mengine yote mpaka uhakikishe
kwanza umefanikiwa katika eneo/kazi/biashara hiyo ndipo ufikirie kuanzisha
vitegauchumi vingine. Kufanikiwa hapa simaanishi mafanikio makubwa sana hapana,
bali ule uwezo wa kuendesha hiyo mifereji mingine kwa kutumia mapato ya hiyo
shughuli yako ya msingi.
………………………………………………
Mpenzi msomaji wa makala hizi nachukua fursa hii
kukujulisha kwamba mwanzoni mwa mwaka huu tuliahidi katika group la michanganuo,
MICHANGANUO ONLINE kwamba tutakuwa na michanganuo bunifu 12 sawa na miezi yote
12 ya mwaka 2018.
Mpaka sasa hivi michanganuo tuliyojadili katika group ni
3 tu. Kuelekea nusu ya mwaka uliobakia miezi mingine 6 tumebadilisha mikakati
kidogo, badala ya kuwa na masomo ya kila siku ya mzunguko wa fedha, tuta ‘focus’
zaidi katika hiyo michanganuo 9 iliyobakia. Hivyo tutakuwa na semina(siyo kila
siku) zitakazohusu namna ya kuandika michanganuo hiyo bunifu hatua kwa hatua
kwa kina kabisa.
Dhamira yetu na malengo tuliyoanza nayo January vipo
palepale wala hakuna kilichotetereka kwani makala za FEDHA(Mtiririko wa pesa)
badala yake tutazihamishia hapa katika blogu ya jifunzeujsiriamali kila siku.
Ila Masomo yaliyokwishapita ambayo sasa yamefikia vitabu 2 tutaendelea kuwapa
free washiriki wapya wanaojiunga na group hilo. Ikiwa hujajiunga bado na group
jiunge sasa ni sh. Elfu 10 tu, kwani semina zilizobakia hatutaziweka katika
vitabu tena, ikipita imepita. Pia bei ya kujiunga na group kwa washiriki wapya
itapanda kuanzia mwezi wa 9 na kuwa sh. Elfu 20.
JIANDAE KWA MCHANGANUO WA BIASHARA BUNIFU INAYOLIPA MWEZI
HUU WA JULY, NDANI YA GROUP LA WATSAP LA MICHANGANUO-ONLINE
Peter Augustino.
0 Response to "MIFEREJI YA KIPATO NI KWA WALIOFANIKIWA, KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NI KUPOTEZA MUDA, NGUVU NA MALENGO BURE"
Post a Comment