Siyo njia zote tunazotumia kubana matumizi ni
sahihi kwetu. Jinsi ya kudhibiti matumizi wakati mwingine tunajikuta tunatumia
mbinu ambazo badala ya kutupeleka katika
hali bora zaidi kiuchumi ndio zinazidi kutudidimiza kwenye umasikini.
Kuzifahamu mbinu hizo potofu kutakuwezesha kuzikwepa na hata kukufanya uchukue
tahadhari katika njia zako unazozitumia kuzisimamia vyema fedha zako au kwa
lugha nyingine ni kuacha matumizi mabaya ya pesa na kushika matumizi bora ya
pesa.
Kila mtu anayetaka kufanikiwa kimaisha hasa katika eneo la kiuchumi au kifedha hana
budi kujiwekea akiba na hatimaye akiba hiyo kuitumia katika uwekezaji kwenye
biashara au vitegauchumi vitakavyomuingizia fedha. Utajiri ni matokeo ya mtu
kutumia kidogo kuliko kile anachoingiza(nidhamu ya matumizi ya pesa), kuhakikisha
unatumia mbinu sahihi za utunzaji au usimamiaji wa pesa ili hatimaye kiasi cha
fedha unachoingiza kiwe kingi kuliko kile unachotoa ni jambo la msingi sana.
MBINU
ZENYEWE ZA UTUNZAJI WA FEDHA ZINAZOWEZA KUKUPELEKA KWENYE UMASIKINI BADALA YA
KUKUTAJIRISHA NI HIZI ZIFUATAZO;
1.Kununua
kwa promosheni(punguzo kubwa la bei!) ukitarajia kupata vitu vingi kwa bei
rahisi.
Huu ni mtego kwa watu wengi wanaonunua vitu
na hata wale wajanja usioweza kuwadhania kama wanaweza kuingia mkenge kama huo.
Baadhi ya wauzaji wengi kwenye maduka na wale wanaotembeza vitu mitaani kuna
wakati hujidai wanauza bidhaa zao kwa punguzo kubwa la bei kumbe hawana lolote,
kwa mfano wanaweza kukutangazia kwamba ukinunua vitu 10 unapata na vitano juu
yake bure! Kumbe hujui bei waliyokuuzia ni ileile ya kawaida. Unajikuta
umeuziwa dazani nzima ya bidhaa wakati hukuwa na haja navyo vyote. Kanuni ya
pesa inashauri kununua tu kile kitu unachohitaji na wala usihadaiwe na
promosheni zisizokuwa na msingi.
Wengine watakuambia kuwa bidhaa fulani
zimebakia chache sana kusudi tu upaparike na kutaka kununu kwa wingi kwa hofu
kuwa bidhaa hizo zinaweza zikamalizika stoo muda mfupi ujao.
2. Kuzima
mara kwa mara taa unapokuwa ukitoka na kuingia chumbani ukidhani unaokoa fedha
unazotumia kulipa bili ya umeme kumbe
siyo.
Kuzima na kuwasha mara kwa mara taa hasa hizi
za kisasa(energy server na tube lights),
kunazidisha gharama zaidi kuliko kuokoa kwani taa hizi zina tabia ya kula umeme
mwingi pindi ziwashwapo hivi halafu ndipo hupunguza kiwango cha ulaji umeme
baada ya dakika kadhaa.
Vilevile taa hizi zina tabia nyigine ya
kuungua haraka zinapozimwa na kuwashwa kila mara. Inatakiwa baada ya kuzima
ukae angalao dakika 15 ndipo ziwashwe tena, hivyo ikiwa utarudi chumbani chini
ya muda huo ni bora ukaiacha iendelee kuwaka wakati unapotoka nje, utakuwa
umeokoa pesa.
3. Akiba
kwako ni mabaki ya kile unachotumia.
Huweki akiba mpaka fedha zinazotumika kwa
matumizi yako ya kawaida zibakie. Ina maana kama hamna mabaki na akiba inakuwa hakuna,
akiba unaifanya kitu cha ziada. Usishangae kama unayo tabia hii kuona kwamba
hutakaa uweke akiba maisha yako yote. Badala yake unashauriwa kutenga kabisa
kiasi ulichojiamulia kuweka akiba kama ni asilimia 10%, 15% au asilimia yeyote
utakayopanga kabla hata hujafanya matumizi mengine ya aina yeyote yale.
4.
Kubana matumizi kupitiliza.
Unafikiri kwamba namna ya kutumia pesa vizuri
ili ufanikiwe haraka basi inakubidi uishi kama ‘Mtauwa’. Ndiyo unaweza
ukajinyima karibu kila kitu kisichokuwa muhimu ili uweke akiba lakini mbinu hii
siyo endelevu hata kidogo katika matumizi ya fedha, hautachukua muda mrefu
kabla haujakata tamaa na kuachilia mbali kuweka akiba. Utakuta labda mtu alizoe
kunywa chai asubuhi au kinyaji chake chupa moja au mbili jioni, kisha ghafla tu
from no where unamwambia aache kabisa kunywa kwa lengo la kubana matumizi aweke
akiba. Itakuwa ni jambo gumu sana kwa mtu kama huyo.
Ni muhimu kwa ajili ya mafanikio yako
kiuchumi kwamba unaweka mipango madhubuti kabla ya kuhakikisha unafanya
matumizi pale tu panapohitajika kufanya na kujiwekea akiba kiasi unachoweza
kuweka. Hata ikiwa utaweka akiba kidogo sana na ikiwa kweli umedhamiria kuweka
kila mara ukazoea itaongezeka haraka kuliko ulivyotegemea.
Ni bora kuweka akiba kila siku shilingi elfu
moja na ukadumu ukifanya hivyo kuliko kujilazimisha kuweka akiba shilingi elfu
10 kila siku na kisha kuishia kukata tamaa na kuacha siku chache. Unashauriwa
kujiwekea lengo linalotekelezeka utakalodumu nalo(kiasi). Kujaribu kubana kila
kitu unachokipata hakuna tofauti na kutokubana matumizi kabisa kwani utafanya
hivyo kwa muda mfupi tu na kisha kurudia maisha yako ya zamani ya kuponda mali.
5.
Kuachana na shughuli zote za kijamii kama harusi na misiba ili ubane matumizi
vizuri.
Unaweza ukafikiria labda kwa kufanya hivyo
itasaidia lakini kumbe ndiyo umejipalia mkaa. Ingawa kweli shughuli nyingi za
kijamii zina gharama, lakini kuziacha kabisa ili eti ubane matumizi utakuja
kulipa gharama kubwa zaidi ya hizo unazokwepa. Mbinu hii itakufanya ujisikie
mpweke na uliyetengwa na jamii inayokuzunguka kiasi kwamba hutaweza kamwe kufurahia
mazingira ya ushirikiano unaouhitaji ili kutimiza malengo yako ya kujiwekea
akiba.
Badala yake tafuta njia zisizokuwa za gharama
kubwa za kushirikiana na jamii kwa mfano badala ya kuwaalika ndugu, jamaa na
marafiki mkutanoni katika hoteli au kumbi za gharama kubwa, waalike vikao vyenu
nyumbani na uwaandalie vyakula na vinywaji mwenyewe. Wajulishe ndugu, jamaa na
marafiki zako malengo yako na watakuwa tayari hata kukuusapoti badala ya kuwakwepa.
5. Kutokutembea
kabisa na pesa taslimu mfukoni.
Unajidanganya kuwa usipobeba hela mfukoni
ndio hautapata vishawishi vya kutumia lakini kumbe hujui kwa kufanya hivyo
unazidisha kujijengea tabia ya kutokuwa makini ni wapi fedha zako zinakokwenda,
ni sawa na mbuni kuficha kichwa chake
mchangani huku kiwiliwili kikiwa nje. Fedha mfukoni ni rafiki yako mkubwa
hasa ukiwa unataka kujenga tabia ya umakini katika matumizi ya fedha. Kutembea
bila pesa mfukoni pia hakutaweza kukufundisha jinsi ya kuepuka madeni kwani
hiyo ndiyo njia nzuri zaidi ya kukufanya uingie madeni yasiyokuwa na msingi.
Unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unatenga
kabisa kiasi cha fedha kinachohitajika kufanya manunuzi ya siku hiyo kabla
hujatoka nyumbani na kuhakikisha hutakwenda kinyume na bajeti hiyo kabisa hata
ushawishike vipi. Hii itakujengea nidhamu nzuri zaidi kuliko kujidanganya
unatoka mifukoni huna kitu.
6. Kukwepa
kupanga bajeti kabisa.
Watu wengine hudhani kwa kutokuweka bajeti kabisa
kutasaidia katika kuwapa utulivu wa nafsi na akili hivyo sula la kuweka akiba kufanyika
vizuri zaidi lakini kumbuka kuweka akiba kamwe hakuwezi kufanyika pasipo juhudi
za makusudi na zinazoonekana.
7.
Kufungua akaunti nyingi mno za benki na katika benki tofauti.
Kufikiria kwamba ukiweka fedha zako kwenye
akaunti na benki tofauti kutasaidia katika utunzaji mzuri wa fedha zako siyo
sahihi. Watafiti wamegundua kwamba watu huweka zaidi akiba fedha zao na kutumia
kidogo pale wanapokuwa na akaunti moja tu ya benki. Unapokuwa na akaunti
nyingi hasa kwenye benki tofauti ni
rahisi zaidi kupoteza malengo na kushindwa kusimamia ni wapi fedha zako
zinakokwenda.
………………………………………………
Masomo
kama haya na mengine mazuri zaidi tumewahi kuyafudisha katika group la whatsap
la MICHANGANUO ONLINE, ni masomo mengi sana sasa yamefika kitabu kizima. Unaweza
kuyapata masomo hayo(PDF) kwa njia ya email yako pamoja na offa ya vitu vingine
mbalimbali kwa sh. Elfu 10 tu. Unapata pia fursa ya kujiunga na group hilo kwa
ajili ya masomo mengine zaidi yajayo na semina.
SIMU: 0712202244
WASAP: 0765553030
0 Response to "NJIA 7 UNAZOTUMIA KUBANA MATUMIZI LAKINI KUMBE ZINAKUZIDISHIA UMASIKINI"
Post a Comment