Msomaji wetu mmoja kutokea kule mkoani Morogoro aliuliza swali hili lifuatalo, nami bila kupunguza wala kuongeza neno naliweka hapa kama ifuatavyo,
"Ndugu mshauri napenda sana kufuga kuku lakini nimeshindwa kuamua nianze na kuku wa aina gani, tafadhali ningeomba unijulishe kati ya kuku wa kisasa wa nyama na wale wa kisasa wa mayai ni wepi waliokuwa na faida zaidi ili nianze kwanza na hao ndipo baadae nikipata uwezo niweze kufuga na hao wengine pia. Asante sana nategemea jibu zuri toka kwako."
MAJIBU.
Kutoa jibu moja tu kwamba ni kuku wa aina gani, kati ya kuku wa kisasa wa nyama na kuku wa kisasa wa mayai ni yupi kati yao aliye na faida zaidi au wanaolipa zaidi siyo rahisi kabla kwanza ya kuchunguza mazingira mazima ya biashara ya ufugaji wa makundi hayo mawili ya kuku, gharama, muda na vitu mbalimbali vinavyohusika katika mchakato mzima tangu unawaingiza bandani mpaka unaanza kupata faida.
"Ndugu mshauri napenda sana kufuga kuku lakini nimeshindwa kuamua nianze na kuku wa aina gani, tafadhali ningeomba unijulishe kati ya kuku wa kisasa wa nyama na wale wa kisasa wa mayai ni wepi waliokuwa na faida zaidi ili nianze kwanza na hao ndipo baadae nikipata uwezo niweze kufuga na hao wengine pia. Asante sana nategemea jibu zuri toka kwako."
MAJIBU.
Kutoa jibu moja tu kwamba ni kuku wa aina gani, kati ya kuku wa kisasa wa nyama na kuku wa kisasa wa mayai ni yupi kati yao aliye na faida zaidi au wanaolipa zaidi siyo rahisi kabla kwanza ya kuchunguza mazingira mazima ya biashara ya ufugaji wa makundi hayo mawili ya kuku, gharama, muda na vitu mbalimbali vinavyohusika katika mchakato mzima tangu unawaingiza bandani mpaka unaanza kupata faida.
Hebu kwanza tuanze na kutizama kila upande,
sifa zake, muda kuanzia wakiwa vifaranga wa siku moja mpaka wanapofikisha umri
wa kuleta faida, gharama pamoja na vihatarishi mbalimbali.
KUKU
WA NYAMA (BROILERS)
Kuku wa nyama ni kuku wanaofugwa maalumu kwa
ajili ya nyama. Muda wao tangu wakiwa vifaranga wa siku moja mpaka kuuzwa ni
mfupi, wiki 4 mpaka wiki 8 tu, kwa hiyo ndiyo kusema kwamba kama unataka faida
ya harakaharaka basi kuku wa nyama ndiyo suluhisho lake.
Uzuri(Faida)
za kufanya biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama.
· Kuku
wa nyama pia huhitaji uwekezaji mdogo lakini mapato yake ni makubwa
unapolinganisha na muda wake.
· Faida
nyingine unapowalinganisha na kuku wa mayai kwa upande wa magonjwa, kuku wa
nyama wanayo nafuu moja kwani kutokana na kipindi chao cha kuishi kuwa kifupi
sana hata unapotokea mlipuko wa ugojwa hasara yake siyo kubwa sana kwani
unakuwa bado hujawekeza fedha nyingi sana hasa kwenye chakula.
· Wanao
uwezo mkubwa wa kubadilisha chakula wanachokula kuwa nyama haraka na hivyo
ukuaji wao pia ni wa haraka.
· Hauhitaji
kiasi kikubwa sana cha madawa na chanjo kutokana na muda wake kuwa mfupi.
Ubaya(Hasara)
za kufanya biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama.
· Hatari
kubwa ya kufa kwa magonjwa hasa wanapokuwa vifaranga.
· Wanahitaji
uangalizi wa karibu mno na hula chakula kingi katika muda mfupi.
· Kuku
wa nyama usipokuwa makini sana na soko wanaweza kukusababishia hasara kubwa
endapo muda wa kuwauza utafika na wakose mtu wa kuwanunua haraka.
· Ili
uweze kupata faida inayoonekana inakubidi mtaji wa kuanzia usiwe chini sana
angalao uanze na vifaranga 100 kwenda juu na hata makampuni au wauzaji wenyewe
wa vifaranga na mawakala wao huwa wanaanzia kuuza viaranga 100 kwenda juu.
KUKU
WA MAYAI.
Hawa ni kuku wanaofugwa kwa ajili ya
uzalishaji wa mayai aidha kwa ajili ya kula tu(mayai yasiyorutubishwa na jogoo)
ama kwa ajili ya kutotolesha vifaranga(mayai yatokanao na matetea waliopandwa
na jogoo).
Uzuri
au faida za biashara hii ya ufugaji wa kuku wa mayai.
· Hatari
ndogo ya kufa kwa magonjwa hasa wanapokuwa wameshafikisha umri wa kuanza
kutaga.
· Kuku
wa mayai wana faida endelevu na ya uhakika kwa kipindi kirefu kila siku kuanzia
wanapoanza kutaga mpaka wanapofikisha wastani wa umri wa miaka 2 wanapokuwa
wameanza kuzeeka.
· Mayai
yakichelewa kuuzika kwa siku kadhaa hayawezi kuongeza gharama kama ilivyokuwa
kwa kuku wa nyama ilimradi tu yasizidi wiki mbili mpaka 3 muda yanapoanza kuharibika.
Ubaya(Hasara)
za kufanya biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai.
· Kuku
wa mayai wanahitaji kiasi kikubwa cha mtaji kwani unahitaji kuwekeza fedha nyingi
zaidi ya miezi minne kabla haujaanza kuuza mayai.
· Hasara
huwa kubwa ukitokea mlipuko wa ugojwa kipindi wameshaanza kutaga.
· Huhitaji
madawa na chanjo nyingi.
Unaweza pia ukalinganisha uzuri wa biashara
ya kuku hawa kwa kutumia kigezo cha wastani wa faida inayopatikana ndani ya
kipindi fulani mfano kipindi cha mwezi au mwaka mmoja ukitumia idadi sawa ya
kuku. Kwa mfano hapa mimi nitatumia idadi ya kuku 100 kuona kwamba katika
kipindi cha mwezi mmoja wastani wa faida katika kila kundi ni kiasi gani.
Ni hesabu rahisi ambayo sitatumia gharama
zote bali nitatumia zile gharama kubwa na muhimu kama chakula tu, gharama
nyinginezo nitachukulia kwamba hazibadiliki kwa pande zote 2 (I assume to remain
constant on both parties)
WASTANI
WA FAIDA KWA KUKU WA NYAMA KWA MWEZI
Gharama(Chakula)
kwa kuku mmoja
Wiki ya 1 mpaka ya 3, starter kg 1.1
Wiki ya 3 mpaka ya 6, Finisher kg 3.4
Jumla wiki zote 6 kuku 1 atakula wastani wa kg 4.5
Kuku
100 watakula kg 4.5 x 100 kg 450 sawa na mifuko 9 ya kilo
50, kila mfuko wastani wa sh. Elfu 45
Hivyo Kuku 100 kwa wastani watakula chakula cha sh. 405,000
kwa wiki 6
Mauzo
ya kuku
Kuku 100 @ sh. 6000 = 600,000
Faida
Faida kwa wiki 6 = 195,000. Kwa wiki 1 =
32,500
Kwa mwezi au wiki 4 =
Sh.
130,000
WASTANI
WA FAIDA KWA KUKU WA MAYAI KWA MWEZI
Gharama
za chakula kwa kuku mmoja.
Wiki ya 1 mpaka ya 8 starter gramu 1,760
Wiki ya 8 mpaka ya 18 Grower, gramu 14,900
Wiki ya 18 mpaka wiki ya 90 layers gramu 65,520
Jumla kuku mmoja atakula gramu, 82,180 sawa
na kilo 82.2
Kwa
kuku wote 100 watakula kilo 82.2 x 100 = kg 8,220 sawa na mifuko
164.5 ya kilo 50 kila mmoja. Mfuko mmoja = sh. 45,000
Hivyo kuku wa mayai 100 katika muda wote wa
wiki 90 watakula chakula cha wastani wa
sh.
45,000 x 164.5 =
7,402,500
Mapato
Mauzo
ya mayai kwa wiki 72 au siku 504 za utagaji
Kila siku wastani wa mayai 85 x siku 504 =
mayai 42,840
Sawa na trei 1,428. Kila trei bei yake ni sh.
9,000
Jumla ya mauzo ya mayai ni sh 9,000 x 1428
12,852,000
Mauzo
ya kuku waliokwishazeeka
Wastani wa kuku 95 x sh.7000 = 665,000
Jumla
ya mapato yote ya mradi ni sh. 12,852,000 + 665,000 =
13,517,000
Faida
Faida
kwa kipindi chote cha wiki 90 ni’
Mapato
yote – Gharama zote
13,517,000 - 7,402,500 =
6,114,500
Faida kwa wiki moja = 6,114,500 gawa kwa wiki
90 = 67,930
Faida kwa mwezi mmoja au wiki 4 = 67,930 x 4
=
Sh.
271,720
HITIMISHO
Kwa haraka haraka ukitazama matokeo ya hesabu
hapo juu utagundua ya kwamba kuku wa mayai wastani wa faida yake kwa mwezi ni
kubwa shilingi 271,720 kushinda wenzao kuku wa nyama shilingi 130,000 kwa mwezi.
Wastani wa faida kwa kuku wa mayai ingawa ni kubwa kwa mwezi lakini hupatikana
baada ya kipindi kirefu tofauti na kuku wa nyama ambao huchukua kipindi cha
wiki chache tu.
Kwahiyo kabla hujahitimisha kwamba ni kuku
aina gani wenye faida zaidi, unapaswa kujipima katika vigezo vifuatavyo
kutokana na jibu la swali hili kuwa na majibu tofauti kulingana na mtu na
mazingira yake aliyonayo.
Muda
ulio nao.
Jichunguze ikiwa labda kama upo bize sana na
mambo mengine mengi. Kwa mfano biashara ya kufuga kuku wa mayai haitaweza
kufanikiwa wala kuwa na faida kwako ikiwa kama huna muda wa kutosha kuwahudumia
katika kipindi chote cha miaka 2 kwa hiyo chaguo lako kama huna muda ni kufuga
kuku wa nyama(broilers)
Kiasi
cha mtaji uliokuwa nao.
Kuku wa mayai wanahitaji mtaji mkubwa wa
kuanzia pamoja na uwekezaji katika vifaa mbalimbali utakavyohitaji kama
mabanda, vitalu, vyombo nk. na fedha hizi hazitakiwi eti ukazitafute wakati
ukiwa umeshaanza vifanga wakiwa bandani hapana. Unapaswa kuwa nazo zote mfukoni
au benki. Kama mtaji wako ni wa wasiwasi usije ukadhubutu kuanzisha biashara ya
ufugaji wa kuku wa mayai labda uanze na idadi ndogo sana ya kuku kulingana tu
na mtaji uliokuwa nao.
Nguvu
kazi iliyopo.
Je utaajiri mtu/watu au utaendesha biashara
ya ufugaji wa kuku mwenyewe?. Ni kina nani watakaokusaidia? Kwakuwa kuku wa
nyama wanachukua kipindi kifupi sana ni rahisi kuendesha mradi hata kama ni wa
idadi kubwa ya kuku ukiwa mtu mmoja peke yako lakini kwa upande wa kuku wa
mayai ni lazima utahitaji wasaidizi. Kwahiyo kama huna msaidizi wa uhakika siyo
vizuri kuanzisha biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai, unaweza kuja kula
hasara.
Na mwisho kabisa ni kwamba ikiwa unao uwezo
wa kutosha katika vigezo vyote vilivyoainishwa hapo juu unaweza pia ukaamua
kufuga aina zote 2 za kuku, kuku wa mayai(Layers) sambamba na kuku wa nyama(Broilers).
Natumaini ndugu yangu uliyeuliza swali hili majibu haya yatakuwa yamekupa mwanga wa kuamua ni kuku wa aina gani utakaoanza nao dhidi ya wengine, siwezi moja kwa moja kukushauri uanze kufuga aina gani kwa kuwa mazingira na uwezo wako siwezi kujua yapoje, hivyo ni juu yako wewe mwenyewe kuamua kulingana na vigezo nilivyokuanishia hapo kwenye majibu ya swali hili.
ASANTE SANA.
Peter A. Tarimo
Mshauri na mwandishi.
Natumaini ndugu yangu uliyeuliza swali hili majibu haya yatakuwa yamekupa mwanga wa kuamua ni kuku wa aina gani utakaoanza nao dhidi ya wengine, siwezi moja kwa moja kukushauri uanze kufuga aina gani kwa kuwa mazingira na uwezo wako siwezi kujua yapoje, hivyo ni juu yako wewe mwenyewe kuamua kulingana na vigezo nilivyokuanishia hapo kwenye majibu ya swali hili.
ASANTE SANA.
Peter A. Tarimo
Mshauri na mwandishi.
……………………………………………………
Je, unataka kuanzisha biashara ya ufugaji wa
kuku lakini hujui ni gharama na mahitaji kiasi gani vinatakiwa? Usije
ukadanganywa kwamba eti ukifuga kuku unahesabu faida tu hapana, kuna gharama
mbalimbali pia unazopaswa kuzijua kabla na njia unazoweza kuzitumia kusudi
uweze kupata faida kubwa. Kuyajua maswala hayo yote unahitaji kufanya utafiti
na kuandaa mpango wa biashara yako ya ufugaji wa kuku hata bila ya kuandika
kwenye karatasi, unaweza kupanga kichwani kwako tu ilimradi ufahamu ni jinsi
gani unavyopanga.
Kwa kusoma michanganuo iliyokwishaandaliwa
tayari unapata picha halisi ni jinsi gani uandae mpango wako. Tuna michanganuo
ya kuku wa aina zote, kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji ambayo
inaweza kuwa msaada mkubwa kwako katika kuandaa mradi wako mwenyewe.
Chakufanya tu ni wewe kutuma malipo ambayo ni
shilingi elfu 10 kwenye namba 0712202244 au 0765553030 na sisi tunakutumia
kifurushi chenye michanganuo yote 3 muda huohuo. Jina hutokea Peter Augustino
Tarimo.
Woow ushauli mzur lakin nilihitaji kufahamu kuwa ni fedha kiasi gan inapaswa kuwa nayo unapohitaj kuanzà
ReplyDelete