Unapokuwa chuoni au shuleni ni tofauti kabisa
na maisha halisi ya mtaani unapokuwa umemaliza masomo na kuanza kazi au
biashara. Mambo uliyokuwa ukifikiria unakuta mengine ni kinyume kabisa. Kwa
hiyo unatakiwa ufahamu namna ya kukabiliana na hali kama hiyo.
Hapa chini nimeorodhesha baadhi ya dondoo
zinazoweza kumsaidia mtu yeyote anayejiandaa kuanza maisha baada ya kuhitimu
masomo yake. Kumbuka wakati wa kumaliza masomo ndiyo muda muhimu sana wa
kuhakikisha ndoto zako unazisimamia vizuri, hapa ndipo unaanza safari nyingine
pengine ngumu zaidi ya ile uliyomaliza. Karibu tusome pamoja.
1.JIEPUSHE
KABISA KWANZA NA MIKOPO
Vijana wengi wanapenda sana kumiliki magari,
subiri kwanza magari yapo siku zote, usikimbilie kukopa kisa tu na wewe
uonekane unamiliki gari kali. Ukitaka kununua gari au kitu chochote kile
kitakachogharimu fedha nyingi basi jiwekee kwanza akiba kidogokidogo mpaka pale
pesa hizo zitakapotimia ndipo ununue.
Tumia ile kanuni ya kujilipa mwenyewe kwanza kila
mwezi, itakusaidia sana katika kutimiza shauku yako hiyo kali(ndoto)
badala ya kukimbilia benki au taaasisi za fedha. Kwanza kumbuka unalo deni
tayari kama ulisoma kwa mkopo sasa madeni juu ya madeni ni ya nini?
2.KUBALI
KUFANYA MAKOSA.
Watu wengi unaowaona leo hii wakiwa na
mafanikio makubwa kama wangelikubali kusikiliza sauti za watu zilizokuwa
zikiwaambia wanafanya makosa, sidhani kama leo wangekuwa pale walipo.
Hawakukatishwa tamaa kirahisirahisi na makosa yao. Funga masikio endelea
kuboresha na kurekebisha taratibu.
3.USIIONEE AIBU HALI ULIYOKUWA NAYO.
Unapaswa kuyakubali maisha kama yalivyo. Kwa
mfano usione haya kutembeza bidhaa zako mtaani ukiziuza kisa eti unaogopa
kuonekana na wale wanaokufahamu, wala usiogope kutembea kwa miguu wakati wa
kwenda kazini ikiwa ofisini siyo mbali sana na unakoishi.
4.USIJARIBUI
KULINGANISHA MAISHA YAKO NA YA MTU MWINGINE YEYOTE YULE.
Watu mashuhuri au wenye uwezo unaojaribu
kujilinganisha nao, niamini wana matatizo yao kama ulivyokuwa na ya kwako.
Wanasumbuliwa na matatizo nkibao kwenye mahusiano yao, wana matumizi makubwa
kwenye bajeti zao na hata jamii nzima hutegemea mambo makubwa zaidi kutoka kwao
kuliko kama ilivyokuwa kwa watu wa kawaida. Huo ni mzigo tosha na hivyo
kujaribu eti kujilinganisha nao kamwe hautapata amani ya nafsi
5.KUWA
MAKINI SANA UNAPOONA MAFANIKIO YANAKUJIA KIRAHISIRAHISI.
Mara nyingi mafanikio ya namna hiyo ni kama
yanakutega vile. Ni lazima kwanza kabla ya kufanikiwa uanguke kwa namna moja au
nyingine, vinginevyo hautajua thamani ya mafanikio hayo. Au inawezekana
mafanikio hayo yamekutokea kwa bahati na sibu tu. Hebu fikiria ikiwa mbele ya
safari utakuja kuanguka na isikutokee tena bahati na sibu, maisha yako
yatakuwaje?
6.FANYA
KITU CHAKO MWENYEWE.
Bila ya kujali kitu hicho ni kidogo au
kikubwa kiasi gani, lakini cha muhimu anzia chini kabisa na jifunze namna ya
kukitafutia soko mwenyewe, wala haijalishi unapoanzisha kitu hicho una ajira au
hujaajiriwa wewe anzisha tu. Hii itakupa funzo muhimu sana maishani
litakalokuja kukusaidia huko mbele ya safari, litakupa ujasiri na kujiamini
kwamba hata likitokea jambo lolote baya katika ajira au shughuli uliyokuwa nayo
basi unaweza kuingia mstari wa mbele mwenyewe(front) na kuanza mapambano.
7.JAMBO
MOJA LINAPOKWAZA MIPANGO NA NDOTO ZAKO, ISIWE NDIYO MWISHO WA KILA KITU.
Usisimamishe mambo yako mengine yote kwa
ajili yake na badala yake jitahidi kuhamishia mawazo yako kwenye mambo mengine
chanya zaidi ndipo utaweza kuwa na maisha bora yaliyo na furaha na mafanikio.
8.SAIDIA
WATU WENGINE MARA NYINGI KADIRI UWEZAVYO.
Usiwaache katika dhoruba ya mateso kama unao uwezo
wa kuwaokoa kutoka wakati mgumu unaowakabili. Mara nyingi utakuja kulipwa kwa
njia moja au nyingine wakati ujao. Kumbuka safari yako bado ni ndefu na unao
muda mwingi mbele tofauti na mtu aliyekwishakaa muda mrefu mtaani, utakutana na
watu wengi baadae hujui kama unayemsaidia leo atakuja naye kukusaidia nini hapo
baadae.
9.USIJIHANGAISHE
KUFANYA KILA KITU KWA UKAMILIFU WA KIWANGO CHA HALI YA JUU SANA.
Unahitaji tu kutafuta suluhisho la kawaida,
mambo makubwa mara nyingi sana hutokana na mambo madogomadogo ya kawaida tu.
10.KUBALI
KUFELI KUPO NA KILA MTU HUFELI
Kila mtu katika muda wa maisha yake hapa
duniani hufeli wakati mmoja au mwingine, cha msingi ni mtu kutokukata tamaa na
kujaribu tena na tena baada ya kuanguka.
11.MWISHO
USISAHAU KUWA MAISHA NI MAGUMU USIPOKUWA MAKINI.
Haijalishi kama wewe ni nani, wala unazo
fedha kiasi gani, usipokuwa makini si ajabu siku moja ukajikuta maisha
yamegeuka chini juu kwako, jitayarishe kila wakati na kuwa makini. Ni nani
alijua watu kama kina Michael Jackson, Whitney Huston, Mc Hammer na mifano
mingine kibao hata hapa Tanzania wapo, watu hao wangekuja kujikuta katika
wakati mgumu kiuchumi kufikia hatua ya kujitoa uhai, wakati mwanzoni
walishashika pesa kufuru?
……………………………………………….........
Ndugu msomaji wa makala hizi, karibu pia
katika GROUP la masomo ya kila siku la WHATSAPP la MICHANGANUO-ONLINE kule
tunajifunza kila siku masomo yahusuyo fedha na michanganuo ya biashara. Pia
tunakuwa na semina za mara kwa mara za jinsi ya kuandika Michanganuo ya
biashara bunifu zinazolipa haraka. Kiingilio ni sh. Elfu 10 tu, tunakupatia na
offa ya vitabu na masomo mbalimbali yaliyopita.
Somo letu la leo tarehe 23 July 2018
litahusu, MBINU ZA KUIFANYA SIKU YAKO IONEKANE
INA MASAA 25 BADALA YA 26. Kumbuka masomo ni kila siku, ukitaka kulipia
tumia namba za simu 0712202244 au 0765553030 jina hutokea Peter Augustino
Tarimo kisha tuma namba ya whatsap au email yako na ujumbe usemao, ‘NIUNGANISHE
NA GROUP LA MICHANGANUO’
Ushauri wako ni mzuri Sana aisee ,,Mungu akubariki sana
ReplyDelete