Kawaulize
wafanyabiashara au wajasiriamali wote wakubwa waliokwishafanikiwa walioanzia
chini kabisa namna walivyopata mitaji yao, hakika utastaajabu watakavyokueleza
jinsi walivyoungaunga kwa shida wakijihatarisha katika mambo mengi kuanzisha na
kupanua biashara hizo huku wakikataliwa na karibu kila mtu anayestahili
kuwasaidia
Ndugu Jamaa na Marafiki.
Mara leo kaenda kwa ndugu huyu ili angalao amkopeshe senti kidogo akaongeze mtaji wake lakini ndugu huyo naye anaanza kumsimulia shida zake kibao, wakati mwingine hata si kama uwezo hana bali tu anahofia akimkopesha fedha zitapotea tu kutokana na kwamba biashara mpya anazijua, alishapitia huko, haiaminiki sana, zina hatari kubwa ‘risky’.
Benki.
Kukataliwa siyo kwa ndugu, jamaa na marafiki tu peke yake. Mjasiriamali huyu anapojaribu kutia mguu wake benki anapokewa na lundo la majibu ya kumshangaza,
“Tutakukopesha pesa tu endapo historia yako kifedha ni nzuri na una akaunti na sisi miezi sita kabla, bila kusahau dhamana zisizohamishika kama vile nyumba, kiwanja au mdhamini mwenye mali hizo”. Usisahau pia kutuletea lesemi yako ya biashara, TIN namba yako na kitambulisho cha Taifa au cha kupigia kura
Lakini mjasiriamali anakumbwa na mshangao mkubwa na kujikuta akizungumza peke yake ndani ya jengo la benki kama aliyepatwa na uendawazimu vile,
“Sasa jamani kama ningelikuwa na hiyo historia nzuri kifehda na mali zisizohamishika huku benki ningefika kutafuta kitu gani?
Hajui jinsi ya kupata TIN wala leseni ya biashara online, hajawahi pia hata kufungua mtandao wa Tausi kujaribu maombi ya leseni ya biashara mtandaoni. Mikopo kwa vijana wajasiriamali, wanawake na walemavu anaisikia lakini hajui hata pa kuanzia ni wapi. Anakosa majibu ya kila swali anaamua kutoka nje amejiinamia kichwa kimechanganyikiwa.
Wateja.
Binafsi katika harakati zangu za kuvinadi vitabu vyangu vya ujasiriamali mtandaoni, siku moja, nikasema hebu na mimi nijaribu kuvitangaza katika forum moja hivi maarufu kwamba nauza vitabu vya ujasiriamali vinavyomwezesha mtu kupata mafanikio upesi, si unajua tena lugha za kibiashara unatakiwa upambe kidogo.
Wachangiaji kwenye lile jukwaa walilipuka kunishuti maswali makali, wengi wao si kwa lengo la kutaka kununua vitabu byangu hapana, bali walitaka tu kujua ikiwa mwandishi nilikuwa na jina au sikuwa, mmoja aliniuliza hivi;
“ Mwandishi wa vitabu hivi ni nani? Unaweza pia kunidokeza kidogo kuhusu mafanikio yake ya kimaisha? Hata kama siyo tajiri napenda kujua mambo aliyopitia ili kukusanya uzoefu unaompa credibility kubwa kuhusu mada hii nyeti hasa wakati huu wa kubana matumizi. Ukifanya hivyo nitanunua vitabu 1 – 2”
Kwa kweli japo nilishukuru wengine walikuwa na lengo zuri la kutaka nitoe maelezo ya kina juu ya vitabu vyangu lakini nilibakia nikijiuliza maswali mengi bila ya majibu.
Nilijaribu kujitetea kwa kuwauliza hivi;
“kwani waandishi wakongwe majina makubwa huzaliwa wakiwa nayo au waliyapata baada kwanza ya wateja kuwaamini kwa kununua kazi zao?”
Maanake sasa niliona hii inageuka kuwa kama ile simulizi maarufu ya YAI NA KUKU ni kipi kilianza kabla ya kingine, unahitaji kwanza wateja wachache ili kujenga kuaminika kwako, lakini pia ili kupata wateja unahitaji kwanza kuaminika kwa kiasi fulani.
Wafanyakazi.
Usije ukajidanganya kuwa eti kwa kuwa watu wana shida sana ya ajira basi ukianzisha tu biashara yako mpya hivi utaweza kupata wafanyakazi wenye uzoefu na ujuzi kirahisirahisi, hilo sahau mpendwa. Wafanyakazi makini wenye sifa zao huuliza kwanza hivi;
“Biashara yenyewe ina uzoefu gani, inaaminika? Uhakika wa kudumu kazini miaka miwili, mitatu upo? Manake nisije nikaenda kazini leo na kesho, keshokutwa nikaambiwa kazi hamna kampuni imekufa”
Wafanyakazi hawakumbuki kwamba hata zile kampuni au biashara wanazoona zimekwishajijengea majina wakati zinaanza ni wafanyakazi walioamua kuchukua hatari na kuamua kufanya kazi wakazikuza mpaka pale zilipopata majina makubwa.
Sina lengo la kumuogopesha mjasiriamali mdogo anayetaka kuanzisha biashara ashindwe kuvuka hatua hii muhimu na ngumu ambayo kila mfanyabiashara huipitia, lakini ninachotaka kueleza hapa ni kwamba...........
VITU
14 VYA OFFA NI HIVI HAPA CHINI:
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu
za BIASHARA, jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika
kila kitu. – kwa Kiswahili
2.
KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 tu - kwa kiswahili
3.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri
Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili
4.
KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN ni maarufu sana duniani, hutumika
vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza
5.
KITABU: Siri za upishi wa chapati
laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili
6.
COMPILLATION: Masomo 30 ya fedha
usiyoweza kuyapata popote, mengine 70 utayapata kwenye group kila siku - kwa Kiswahili
7.
MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji
Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili
8.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa
kiingereza
9.
MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane
Restaurant –kwa Kiswahili
10. MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili
11. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiingereza
12. MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini
Broilers –kwa kiswahili
13. MCHANGANUO: Kiwanda cha mvinyo na juisi ya Rosella –Choya Investment – kwa kiswahili
14. MCHANGANUO: Kilimo cha Tikiti maji:- Kibada Watermelon Fruits – kwa kiswahili
0 Response to "KUANZISHA BIASHARA WAJASIRIAMALI WAPYA HUKATALIWA NA KILA MTU, WATEJA, BENKI NA HATA WAFANYAKAZI"
Post a Comment