CHUNGUZA WATU WENYE MAFANIKIO MAKUBWA KIMAISHA NA KIUCHUMI, UTAGUNDUA WALITUMIA KANUNI HII MUHIMU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

CHUNGUZA WATU WENYE MAFANIKIO MAKUBWA KIMAISHA NA KIUCHUMI, UTAGUNDUA WALITUMIA KANUNI HII MUHIMU

SURA YA 10, FIKIRI UTAJIRIKE/THINK & GROW RICH

Nguvu ni muhimu kwa ajili ya mafanikio katika kutafuta pesa. Mipango ni mfu na haina maana kama hamna nguvu ya kutosha ya kuibadilisha kuwa katika vitendo. Sura hii itaelezea njia ambayo mtu binafsi anaweza akapata nguvu na kuitumia.

Nguvu inaweza kuelezewa kama “Maarifa yaliyoratibiwa na kuongozwa kwa akili” Nguvu kama neno hili lilivyotumika hapa, linamaanisha juhudi zilizoratibia za kutosha kumwezesha mtu kubadilisha shauku kuwa katika kipimo chake cha fedha. Juhudi zilizoratibiwa hutolewa kupitia uratibu wa juhudi za watu wawili au zaidi ambao hufanya kazi kuelekea lengo kamili katika roho ya masikilizano.

NGUVU INAHITAJIKA KWA AJILI YA UKUSANYAJI WA FEDHA! NGUVU NI MUHIMU KWA AJILI YA KUZITUNZA FEDHA BAADA YA KUWA ZIMEKUSANYWA!

Ngoja tuhakikishe jinsi nguvu inavyoweza kupatikana. Ikiwa nguvu ni maarifa yaliyoratibiwa, hebu tuchunguze vyanzo vya maarifa.

1. NGUVU KUU ISIYOKUWA NA MIPAKA
Chanzo hiki cha maarifa kinaweza kufikiwa kupitia njia zilizoelezwa katika Sura ya 6 kwa msaada wa Ubunifu unaojenga

2. UZOEFU ULIOKUSANYWA.
Uzoefu uliokusanywa wa binadamu(au ile sehemu yake ambayo imeratibiwa na kurekodiwa) Unaweza kupatikana katika maktaba yeyote ile ya umma iliyoandaliwa vizuri. Sehemu muhimu ya uzoefu huu uliokusanywa unafundishwa katika mashule na vyuo, ambapo umepangiliwa na kuratibiwa.

3. MAJARIBIO NA UTAFITI.
Katika uwanja wa sayansi na karibu katika kila nyanja nyingine za maisha watu hukusanya, kuanisha na kuratibu matukio mapya ya kweli kila siku. Hiki ni chanzo ambacho mtu anaweza kukirudia wakati maarifa yanapokuwa hayapatikani kupitia uzoefu uliokusanywa. Hapa pia ubunifu wa kujenga ni lazima utumike mara nyingi.

Maarifa yanaweza yakapatikana kutoka katika chanzo chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu. Yanaweza kubadilishwa kuwa katika nguvu kwa kuyaratibu kwenda katika mipango kamili na kwa kuelezea hiyo mipango katika vitendo.

Uchunguzi wa vyanzo vikubwa vitatu vya maarifa utagundua mara moja ugumu ambao watu wangeweza kupata ikiwa wangetegemea juhudi zao wenyewe tu- katika kukusanya maarifa na kuyalezea kupitia mipango kamili katika vitendo. Kama mipango yao inaeleweka, na ikiwa inafikirisha kwa kiasi kikubwa, ni lazima kwa ujumla wawaambukize wengine kushirikiana nao kabla hawajaweza kuchomeka katika mipango yao kiungo muhimu cha nguvu.

Kuongeza Nguvu Kupitia “Ushirika”(master mind)

“Ushirika” unaweza ukaelezewa kama ushirikiano wa maarifa na juhudi katika roho ya masikilizano(mapatano), kati ya watu wawili au zaidi kwa ajili ya kufikia lengo kamili”

Hakuna mtu mmoja anayeweza kuwa na nguvu kubwa bila ya kujihusisha na ushirika. Katika Sura ya 7, maelezo yalitolewa kwa ajili ya uundaji wa mipango kwa lengo la kuitafsiri shauku kuwa katika kipimo chake cha fedha. Ikiwa utafuata maelekezo haya kwa uvumilivu na akili na kutumia upendeleo katika uchaguzi wa “kundi lako la kushauriana” lengo lako litakuwa limetimia nusu yake kabla hata haujaanza kuliona.

Hivyo unaweza kutambua vizuri fursa zisizoshikika za nguvu iliyopo kwako kupitia kundi la kushauriana lililochaguliwa vyema, hapa tutaelezea sifa mbili za kanuni ya ushirika, mojawapo ina asili ya kiuchumi, na nyingine ni ya kiroho. Sehemu ya kiuchumi ipo wazi, faida zake kiuchumi zinaweza kutengenezwa na watu wanaozungukwa na mawaidha, ushauri, na ushirikiano binafsi wa kundi la watu waliotayari kuwapa msaada wa hali na mali katika roho ya masikilizano kamili.

Aina hii ya ushirikiano wa kutegemeana umekuwa ni msingi wa karibu kila utajiri mkubwa. Uelewa wako wa ukweli huu mkubwa unaweza hatimaye kuamua hali yako kiuchumi.

Upande wa kiroho wa kanuni ya ushirika ni ya kidhahania zaidi, ngumu zaidi kueleweka kwasababu inahusiana na nguvu za kiroho ambazo binadamu kwa ujumla hawana uelewa nazo vizuri. Unaweza ukashika ushauri muhimu kutoka katika kauli hii;
‘Hakuna akili mbili zilizowahi kuja pamoja pasipo halafu kutengeneza nguvu ya tatu isiyoonekana wala kushikika ambayo inaweza ikapendwa na akili ya tatu. Kumbuka ukweli kwamba kuna viasili viwili tu vinavyojulikana katika Ulimwengu mzima – Nishati na Maada. Maada inaweza ikagawanyika katika vipimo vya molekyuli, atomu na electrons. Kuna vipimo vya maada vinavyoweza kutenganishwa na kuchunguzwa.

Halikadhalika, kuna vipimo vya nishati.

Akili ya binadamu ni aina ya nishati, sehemu yake moja ikiwa na asili ya kiroho. Akili za watu wawili zinaporatibiwa katika roho ya masikilizano, vipimo vya kiroho vya nishati za kila ubongo  hutengeneza udugu ambao hubeba upande wa kiroho wa ushirikianoa. Kanuni ya ushirika au zaidi sehemu yake ya kiuchumi, kwa mara ya kwanza nilijulishwa na Andrew Carnegie. Ugunduzi wa hii kanuni ulihusika na uchaguzi wa kazi yangu maishani.

Kundi la kushauriana la Bwana Carnegie lilikuwa na watu wapatao 50 ambao walimzunguka yeye mwenyewe kwa lengo kamili la kuzalisha na kutafuta soko la chuma cha pua. Alihusisha utajiri wake wote na nguvu alizozipata kupitia ushirika huu. Chunguza rekodi za mtu yeyote aliyepata utajiri mkubwa na wengi wa wale waliojikusanyia utajiri wa kawaida, na utagundua kwamba walitumia kanuni ya ushirikiano kwa kujua au kwa kutokujua.

itaendelea................


 UKIPENDA KUFUNGUA SEHEMU NA SURA ZILIZOPITA BONYEZA HAPA


0 Response to "CHUNGUZA WATU WENYE MAFANIKIO MAKUBWA KIMAISHA NA KIUCHUMI, UTAGUNDUA WALITUMIA KANUNI HII MUHIMU "

Post a Comment