Unapomuuliza mtoto au mwanafunzi katika shule yeyote ile kuwa angependa kuja kuwa nani hapo baadae atakapomaliza masomo yake, atakujibu haraka sana na moja kati ya majibu anayoweza kukupa ni haya yafuatayo;
· Nataka
kuja kuwa mwanasheria.
· Nitakuja
kuwa dokta.
· Nataka
nije kuwa Rais kama Dokta John Pombe Magufuli
· Mwandishi
wa habari, mtangazaji.
· Nataka
kuwa mwalimu
· Nataka
niwe Rubani wa ndege
· Nataka niwe mwanamuziki kama Diamond
· Nataka niwe mwanamuziki kama Diamond
· Nitakuwa
mtaalamu wa kompyuta
· Nataka
nije niwe injinia
· Nitakuwa
Polisi, Mwanajeshi nk.
Sababu kubwa za kuchagua kuwa katika fani au kazi tofauti
ni Mapenzi(Passion) waliyokuwa nayo watoto katika kazi ama fani husika. Shauku
waliyokuwa nayo katika kutimiza kitu fulani kwenye fani hizo, wanataka waje
kufanya kitu tofauti sana lakini pia kuna lengo jingine la mwisho ambalo ni
kujipatia kipato kitakachowawezesha kuishi. Ingawa kujiingizia kipato ni moja
ya malengo yao katika kuchagua fani, lakini siyo sababu kuu hasa inayopewa kipaumbele cha kwanza
katika kuchagua fani wakati huo. Hatima ya kila kitu ni kuja kupata kipato cha
kuendeleza maisha lakini kuna malengo mengine muhimu pia.
SOMA: Njia za kuingiza kipato cha ziada nje ya kazi yako.
SOMA: Njia za kuingiza kipato cha ziada nje ya kazi yako.
Mtoto au mwanafuzni husukumwa zaidi na ubora wa
kukamilisha ndoto yake hiyo na jinsi atakavyoweza kuwa kinara kwenye hiyo fani
miongoni mwa wenzake au watu wengine, kipato siyo kipaumbele peke yake. Lakini
pamoja na nia hiyo njema, katika maisha ya kawaida tunachokuja kukishuhudia
baadae ni kinyume kabisa na jinsi tulivyotamani tuje kuwa.
Mtoto yuleyule anapokuja kuingia katika maisha ya kazi
husahau kabisa matamanio (mapenzi) yake ya utotoni na kujikuta akichukua
muelekeo tofauti kabisa ambao wala hakuutegemea. Anasahau malengo mengine yote
na kuanza kusaka kipato cha muda mfupi badala ya ya ubora kwenye fani
aliyotamani kuwa tokea utotoni. Hamasa ya kile anachokifanya inakuwa haipo tena
anabakia kufanya kazi ni kazi tu ilimradi imuingizie kipato. Kipato sasa
kinageuka kuwa ndiyo lengo lake la msingi kuliko kitu kingine chochote kile.
SOMA: Kwanini ni rahisi zidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?
SOMA: Kwanini ni rahisi zidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?
Ni kitu gani hufanyika mpaka hali hii kutokea ukubwani?
Ikiwa utaamua kuwauliza wengi wa watu hawa wataishia kukupa majibu mbalimbali
na mengi yakiwa katika mtindo wa lawama kwa vitu na watu mbalimbali. Wengine
watatoa lawama kwa Waajiri wao wakidai kuwa waajiri hao huwapunja mishahara,
wanawabana mno kiasi kwamba wanashindwa kutumia ubunifu waliokuwa nao nk.
Wengine utawasikia wakiwalaumu wateja wao na kusema, hawataki kununua bidhaa
zao au wananunua kwa bei ya chini. Wengine watatoa lawama zao kwa mfumo wa
elimu na serikali kwa ujumla wakisema elimu waliyoipata haiwezi kuwafanya
watimize ndoto zao, ni duni na haikuwaandaa vizuri kukabiliana na soko la ajira
lililopo au kazi walizochagua kuzifanya.
Lakini ukweli halisi ni kwamba, watu tumekuwa tukipenda
kupitia njia za mkato mno katika maisha. Watu tunapenda kuwa na mambo mazuri
pasipo kutoa jasho na ili kujiridhisha nafsi zetu tunaamua kufanya kazi yeyote
ile itakayotuwezesha kulifikia lengo la mwisho ambalo ni kujipatia kipato(riziki)
wakati kipato kinatakiwa kuwa ni matokeo ya kazi ile uliyoichagua kufanya kwa
mapenzi.
SOMA: Jinsi ya kupanga malengo ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi.
SOMA: Jinsi ya kupanga malengo ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi.
Ukimuuliza mtu ni kwanini anafanya kazi fulani atakujibu
anaifanya ili kupata kipato cha kuendeshea maisha yake, hautamsikia tena
akisema ni mapenzi aliyonayo kwenye kazi hiyo ndiyo yanayomchochea kuifanya
kama alivyokuwa akifikiria wakati akiwa bado mtoto. Mtu wakati anapokuwa mtoto
angali bado shuleni husukumwa zaidi na mapenzi ya dhati kwenye fani, anapokuja
kuingia katika hali halisi baada ya masomo husukumwa na mahitaji ya muda mfupi
ambayo ni pesa au kujikimu kimaisha.
Na anapokuwa akipata mahitaji hayo ya muda mfupi
hubadilisha kabisa muelekeo wake aliokuwa nao mwanzoni, hafanyi tena kazi kwa
mapenzi kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo tokea utotoni za kuwa mahiri katika
fani aliyochagua.
Kwahiyo ili mtu uweze kuwa kama vile ulivyotaka uwe
wakati ulipokuwa mtoto ni lazima uhakikishe kwanza unaishikilia ndoto yako
kikamilifu na kudumu nayo, kumbuka hakuna kitu chochote kinachoweza kupatikana
kirahisi na ni lazima ukutane na vikwazo vingi njiani, kikubwa tu ni kwamba “usifuate
njia ya mkato”
SOMA: Unawezaje kuyakabili magunu, maanguko na mikasa ya kutisha maishani kama hii?
SOMA: Unawezaje kuyakabili magunu, maanguko na mikasa ya kutisha maishani kama hii?
Wakati ukifanya kazi kwa bidii na maarifa kutimiza ndoto
yako ya kuwa kili ulichotaka kuwa tangia utotoni, moja kwa moja pia na malengo
yako kifedha yatakuwa yakitimia pasipo hata wewe mwenyewe kujua na wakati
mwingine unaweza kuingiza pesa nyingi kuliko kama vile ungeliamua kutumia njia
za mkato.
.................................................
Ndugu msomaji wa makala hii, nakukaribisha kwenye group letu la Watsap la masomo kila siku pamoja na semina kila mara. Masomo yanahusiana na mzunguko wa fedha katika biashara zetu na mifukoni mwetu wenyewe kwa ujumla. Semina zinahusiana na jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara na kwa kila semina huwa tunaandika mchanganuo 1 wa biashara yenye fursa kubwa hatua kwa hatua.
Kujiunga kuna kiingilio cha sh. elfu 10 na unapata masomo yote yaliyopita, semina, vitabu na michanganuo mbalimbali ikiwemo ya kuku aina zote na kilimo cha matikiti maji. Unapewa bure kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali ambacho kina masomo ya kila aina ya ujasiriamali na namna ya kuandaa michanganuo ya biashara. Vitu unavyotumiwa punde tu baada ya malipo ni hivi vifuatavyo na kisha kila siku unaendelea kupokea masomo kupitia wasap au email yako;
SIMU: 0712202244
Whatsap: 0765553030
Unaweza pia ukajipatia vitabu mbalimbali vya ujasiriamali kutoka kwetu katika lugha ya kiswahili kwa kutembelea ukurasa wetu wa vitabu wa; Smart Books Tanzania
Kwenye group leo tarehe 19 August siku ya Jumapili tutakuwa na somo la fedha lisemalo;
"CHANGAMOTO KUBWA 3 NA MBINU ZA KUBAJETI FEDHA KIDOGO KWENYE BIASHARA MPYA INAYOANZA"

0 Response to "JE, UPO KWENYE KAZI AU FANI ULIYOTAMANI KUWA TANGU ULIPOKUWA MTOTO MDOGO?"
Post a Comment