Kuweka kumbukumbu za biashara ni jambo rahisi iwe wewe ni
mjasiriamali mdogo au mkubwa, unayekaa mwenyewe kwenye biashara au uliyemwajiri
mfanyakazi akuuzie. Tatizo linakuja kwenye usimamiaji na ufuatiliaji wa hesabu
hizo kila mara. Wajasiriamali wengi huona kama ni kazi ngumu kufuatilia hesabu
kila siku na mwishowe huamua kuacha mambo yaende kiholela na hapo ndipo huja
kulia na kusaga meno baadae.
SOMA: Biashara ndogo kwa wajasiriamali zinazoendana na wakati tulio nao sasa.
SOMA: Biashara ndogo kwa wajasiriamali zinazoendana na wakati tulio nao sasa.
Ikiwa mjasiriamali anaendesha biashara peke yake bila
msaidizi, ufuatiliaji wa hesabu hauwezi kuwa na changamoto nyingi lakini mara
tu utakapoajiri msaidizi changamoto nazo huibuka. Njia za kawaida za uwekaji wa
kumbukumbu za mahesabu ya biashara ni zilezile hazibadiliki. Unaweka kumbukumbu
za matumizi yote na mapato ya kila siku kisha baada ya kipindi fulani tuseme
labda siku, wiki au mwezi unakuja kufanya tathmini umepata faida kiasi gani.
Unaweza pia ukafanya tathmini ya hesabu nyingine kama vile mtiririko wa fedha
taslimu na mizania ya biashara.
Uwekaji wa kumbukumbu na hesabu za biashara umeelezewa
kwa undani sana katika kitabu cha “MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI”
ambacho nadhani kila mtu hapa kwenye Group la Michanganuo-online anayo nakala
yake. Somo hilo lipo katika ukurasa wa 351 mpaka uk. wa 375 ni somo refu kwenye
hicho kitabu. Vile vile katika kitabu kingine cha “MAFANIKIO YA BIASHARA YA
DUKA LA REJAREJA” katika ukurasa wa 50 –
73 kimeelezea vilevile kwa kirefu namna ya kuweka kumbukumbu na kukokotoa
hesabu katika biashara ya rejareja hususani duka.
SOMA: Biashara ya duka inavyoweza kukutoa kimaisha ukiwa mjanja.
SOMA: Biashara ya duka inavyoweza kukutoa kimaisha ukiwa mjanja.
Lakini leo hii hasa si lengo langu kuyarudia masomo hayo
kama yalivyoelezwa katika hivyo vitabu na hata mahali kwingineko, bali nia
yangu hasa ilikuwa ni kujibu swali au ombi la msomaji ambaye pia ni mwanagroup
mwenzetu humu(hajaniruhusu kutaja jina
lake lakini) aliyeniomba niandike kidogo kuhusiana na suala zima la
udhibiti wa hesabu kwenye biashara ndogo ya uuzaji wa maziwa, mdau huyu anacho
kioski chake cha kuuzia maziwa mbali na shughuli zake za msingi na amemwajiri
kijana, sasa inamuwia vigumu katika kudhibiti mapato kila siku inapofika jioni.
SOMA: Kama adui mkubwa wa fedha zako ni wewe mwenyewe, utumie njia gani ili ziweze kuwa salama?
SOMA: Kama adui mkubwa wa fedha zako ni wewe mwenyewe, utumie njia gani ili ziweze kuwa salama?
Kama nilivyotangulia kusema awali kwamba, “Ikiwa
kama huwezi kudhibiti hesabu za biashara yako, basi ni bora uifunge au kuachana
nayo kabisa”-Peter Augustino. Hapa nitaeleza kanuni muhimu sana
ambayo ndiyo itakayokuwa muarobaini katika kudhibiti mapato ya biashara yako.
Nitaelezea kwanza mahsusi(specifically) kwa biashara ya huyu mwenzetu ya uuzaji
maziwa na kisha nitaelezea kwa ujumla ili hata kama kuna mtu anataka ‘kuiapply’
kanuni hiyo katika biashara nyingine yeyote ndogo basi aweze kufanya hivyo.
Kwa kuwa biashara ya maziwa………………
…………………………………………………
Mpenzi
msomaji katika blogu hii, makala hii nzima tutajifunza leo kwenye Group la
watsap la MICHANGANUO-ONLINE, masomo kama haya huwa tunajifunza kila siku saa 3
mpaka saa 4 usiku. Katika group hilo pia tunakuwa na semina za mara kwa mara
juu ya uandaaji wa mipango ya biashara mbalimbali zilizo na fursa kubwa ya
kuleta faida.
Ili
kujiunga na Group lipia kiingilio sh. Elfu 10 kupitia namba zetu
0712202244 au 0765553030 kisha tuma anuani yako ya email
kwa sms ikifuatiwa na maneno, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”
Unapojiunga
pia unapata masomo yote yaliyopita, semina pamoja na vitu mbalimbali kama ifuatavyo;
0 Response to "JINSI YA KUSIMAMIA HESABU KATIKA BIASHARA NDOGO UNAYOMWACHIA MFANYAKAZI"
Post a Comment